Pesa haramu: Pablo Escobar, El Chapo na Bernie Madoff walivyotengeza pesa nyingi kupitia uhalifu

Chanzo cha picha, Getty Images
Pesa walizotengeza kupitia uhalifu ni nyingi sana na hata wakati mmoja zilizidi kiasi cha fedha katika bajeti ya baadhi ya nchi.
Watu hawa ,wengine ambao bado wapo hai ilhali wengine wamefariki wakati mmoja walionekana kuwa kileleni mwa taaluma zao za uhalifu .Ujanja wao na weledi wao kutafuta pesa na kukwepa mkono wa sheria ulionekana kama ushujaa na hadi leo katika baadhi ya nchi wangali wanachukuliwa kama 'mashujaa' .
Hatahivyo walikumbana na mauti yao katika hali ambazo pesa na mali walizokuwa wametengeza hazingeweza kuwasaidia .Hawa hapa baadhi ya wahalifu sugu waliokuwa na utajiri ambao walipata kupitia uhalifu na ulaghai.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pablo Escobar
Pablo Escobar alizaliwa huko Rionegro, Colombia mnamo 1949 na akaanzisha genge la kuuza dawa za kulevya huko Medellín mnamo miaka ya 1970.
Wakati wa kazi yake, genge hilo lilitoa wastani wa 80% ya kokeni iliyosafirishwa kwenda Marekani
Utajiri wake ulimwingiza kwenye orodha ya Forbes ya mabilionea wa ulimwengu kwa miaka saba.
Baada ya Marekani kutoa amri ya kukamatwa kwake ili ashtakiwe nchini humo , Escobar alipinga kukamatwa na genge lake lililenga wanasiasa, polisi na waandishi wa habari.
Baada ya kukamatwa mnamo 1991, Escobar aliwekwa ndani ya gereza la muundo wake mwenyewe, kwa jina Kanisa Kuu, ambapo aliendelea kusimamia kundi la Medellín
Kwa jumla, Escobar anafikiriwa kusababisha vifo vya takriban watu 4,000.
Lakini hali yake ya kuwapenda na kuwasaidia watu wake ilimfanya kuwa maarufu kati ya Wakolombia wengine ambao msaada wao aliuendeleza kwa kutoa pesa nyingi na kuwekeza katika vitongoji duni huko Medellín.
Pablo Escobar, mlanguzi wa dawa za kulevya aliyefariki bado anaonekana na Wakolombia wengi kama shujaa
Inasemekana kuwa wakati kilele cha nguvu zake katika biashara hiyo haramu Escobar alikuwa mtu wa saba kwa utajiri duniani huku kundi lake la Medellin likidhibiti asilimia 80 ya soko la kokeni ulimwenguni.zaidi ya miaka thelathini baada ya kifo chake ,Escobar yungali anatengeza pesa na huenda sehemu y mali yake bado ipo hadi leo
Septemba mwaka wa 2020 mpwa wa Escobar alisema alipata mfuko wa plastiki na pesa zenye thamani ya $ 18m (£ 14m) zilizofichwa kwenye ukuta wa nyumba moja ya mjomba wake.
Nicolás Escobar aliwaambia wanahabari wa Colombia "maono" yalimuonyesha mahali pa kutafuta pesa katika nyumba anayoishi katika jiji la Medellín.
Alisema haikuwa mara ya kwanza kupata pesa mahali ambapo mjomba wake alikuwa akijificha ili kuepuka kukamatwa, kwani Escobar aliripotiwa kuficha mali ya thamani ya mamilioni ya pesa
Alikufa katika ufyatulianaji wa risasi na polisi mwaka wa 1993.
Nicolás Escobar alikiambia kituo cha Televisheni cha Red + Noticias cha Colombia pia alikuwa amepata mashine ya chapa , simu za setilaiti, kalamu ya dhahabu, kamera na filamu ambayo bado haijatengenezwa.
Baadhi ya noti za miongo kadhaa zilikuwa zimeoza na hazitumiki tena, alisema Nicolás Escobar, ambaye amekuwa akiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mitano.
Katika mahojiano hayo, alisema aliandamana na mjomba wake mara nyingi, na kwamba aliwahi kutekwa nyara na watu wanaotafuta mahali alipo Escobar

Chanzo cha picha, EPA
Bernie Madoff
Bernie Madoff, ni bwenyenye wa Wall Street aliyeaibishwa baada ya kukiri kutelekeza moja ya utapeli mkubwa katika historia ya kifedha ya Marekani na amekufa gerezani akiwa na umri wa miaka 82 wiki moja iliyopita.
Kifo chake kilitangazwa na Ofisi ya Magereza.
Bwana Madoff alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 150 baada ya kukiri hatia mnamo 2009 ya kuendesha mpango wa kilaghai ambao ulilipa wawekezaji pesa kutoka kwa wateja wapya badala ya faida halisi.
Ulaghai wake huo wa ponzi uIlianguka wakati wa msukosuko wa kifedha wa 2008.
"Bernie, hadi kifo chake, aliishi na hatia na majuto kwa uhalifu wake," wakili wake Brandon Sample alisema katika taarifa.
"Ingawa uhalifu ambao Bernie alihukumiwa kufanya umefafanua ni mtu wa aina gani - pia alikuwa baba na mume. Alikuwa mzungumzaji laini na msomi. Bernie hakuwa mkamilifu. Lakini hakuna mtu aliye sawa." Taraifa hiyo iliongeza.
Bwana Madoff, mtoto wa wahamiaji wa Uropa ambaye alikulia New York, alianzisha kampuni yake ya jina Bernard L Madoff Investment Securities mnamo 1960.
Kampuni hiyo ikawa moja wapo ya wafanyabiashara wakubwa - wanunuzi wakiunganishwa na wauzaji wa hisa - na Bwana Madoff aliwahi kuwa mwenyekiti wa soko la hisa la Nasdaq.
Kampuni hiyo ilichunguzwa mara nane na Tume ya Usalama na Ubadilishaji ya Marekani kwa sababu ilipata faida kubwa kupindukia
Walimu wa shule, wakulima, fundi mitambo na wengine wengi pia walipoteza pesa.
"Tulifikiri alikuwa Mungu. Tuliamini kila kitu mikononi mwake," mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Elie Wiesel, ambaye wakfu wake ulipoteza dola milioni 15.2, alisema mnamo 2009.
Katika korti, Bwana Madoff alisema kwamba wakati alianza mpango huo mnamo miaka ya 1990, alitumai itakuwa kwa muda mfupi tu.
Alijitengezea kiasi kikubwa cha fedha na hakujua siku moja angezipteza kwa hatua moja hadi alipkamatwa na kufungwa jela

Chanzo cha picha, Getty Images
El Chapo Guzman
El chapo Guzman ambaye kwa sasa anahudumia kifungo cha jela nchini Marekani alijiundia sifa kwa kutoroka gerezani Zaidi ya mara moja katika hali za kutatanisha .Hata hivo kikubwa kumhusu ni jinsi alivyotengeza kiasi kikubwa cha apesa kupitia biashara haramu za ulanguzi wa dawa za kulevya
Alianza kujihusisha na uhalifu uliopangwa akiwa na umri wa miaka 15, wakati alipanda bangi katika shamba lake pamoja na binamu zake. Kisha, akachukua jina la utani "El Chapo" - jina la Mexico kumaanisha 'mtu mfupi', Lakini matamanio yake yalidhihirisha kimo chake cha kupungua (yeye ni ana kimo cha futi 5 na nchi 6 , au mita 1.64).
Akiwa na umri wa miaka 20, Guzmán aliondoka La Tuna kutafuta utajiri wake katika magendo ya dawa za kulevya. "Daima alipigania maisha bora," mama yake alisema.
Wazazi wake - Emilio Guzmán Bustillos na María Consuelo Loera Pérez - walipata riziki yao kwa kilimo. Baba yake alikuwa mfugaji rasmi lakini inaaminika alikuwa mkulima wa Opium , Malcolm Beith anaandika katika kitabu chake, The Last Narco.

Chanzo cha picha, Reuters
Ari ya Guzmán ya kufaulu katika biashara ilikuwa dhahiri tangu akiwa na umri mdogo. Angeweza kusaidia familia yake kwa kuuza machungwa kwa wakulima wadogo kwa pesa chache. Matamanio yake ya kutaka maisha mazuri pia yalionekana
Katika jarida podcast la Vice News , dada mdogo wa Guzman Bernarda alisema angevaa vito vya dhahabu bandia wakati wa kuwatembelea watu wa familia yake.
"Hata kama mtoto mdogo, alikuwa na matamanio," mama yake aliwaambia watengenezaji wa filamu mnamo 2014. Alikumbuka alikuwa na "pesa nyingi za karatasi" ambazo angehesabu na kurudia kuzihesabu .
Baada ya muda, kundi la Guzmán likawa moja ya biashara kubwa za dawa za kulevya zakuingia Marekani na mnamo 2009, aliingia kwenye orodha ya Forbes ya wanaume tajiri zaidi ulimwenguni akiwa nambari 701, na wastani wa mali yenye thamani ya $ 1bn (£ 709m).
Kadiri utajiri wake na himaya ilivyokua, ndivyo pia uchunguzi kutoka kwa mashirika ya sheria ya Marekani ulivyoendelea .Shirika la DEA lilikuwa likimfuata kwa miongo kadhaa .















