Tukiyakiuka mambo haya 9 huenda dunia ikaangamia

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Miaka 11,000 iliyopita kitu kisicho na kifani kwenye miaka 100,000 ya historia ya dunia kilitokea: hali ya hewa ya dunia ilikuwa imara. Kipindi chenye viwango vya joto vinavyotabiriwa katika hali iliyopewa jina Holocene iliwapa wanadamu fursa ya kuanza kufanya kilimo, kufuga wanyama na kubuni dunia ya sasa.

Hata hivyo, kwenye mchakato huo familia za viumbe hutoweka na tunaharibu mifumo ikolojia, tunachafua hewa maji na mchanga na kuchangia mabadadiliko ya hali ya hewa. Kwa namna nyingine tulilazimsiha kuingia katika kipindi kujulikanacho kama Anthropocene, kipindi ambapo wanadamu uhusika kwenye mabadiliko ya hali ya hewa.

Ni kwa muktadha huu ambapo kundi la wanasayansi wa kimataifa wakiongozwa na raia wa Sweden Johan Rockström kutoka Stockholm Resilience Center, walianza kuchunguza kuhusu ni hatari inayotukabili wakati tunaharibu mifumo ya usawa wa mambo ya asilia ya dunia.

Utafiti wao uliochapishwa mwaka 2009 ulitaja mambo tisa ambayo ni muhimu katika kuhakikisha utulivu wa dunia. Ikiwa hatutavuka mipaka hii, wanasema kuwa ubinadamu utaendelea kuwepo kwa vizazi.

Lakini kwa kwenda kinyume na jambo hata moja tu, tutajiweka kwenye hatari kwa kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa kwenye mfumo wote na kuchochea kuporomoka kwa jamii yetu.

Mipaka 9 ya dunia

Kati ya mipaka tisa, tayari tumevuka minne, kuna mitatu inayotajwa kuwa katika eneo salama kwa sasa na miwili mbayo bado haijulikani

1. Mabadiliko ya hali ya hewa

Moja ya mipaka minne ambayo tayari tumevuka ni ule maarufu kwa yote wa mabadiliko ya hali ya hewa.

Tangu yaanze maendeleo ya kiviwanda, viwango vya joto duniani vimeongezeka kwa nyuzi 1.1C. Kuongezeka huku ndiko kumechangia majanga yanayotokea kote duniani kama vile ukame na mafuriko

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataiafa, leo hii tuna majanga mara tano zaidi ya ilivyokuwa mwaka 1970 na gharama ya majanga hayo ni mara saba zaidi. Matokeo yake ni makubwa na vifo vingi. Wanasayansi wanasema ili kuzuia athari zitokanazo na mabadilikoa ya hali ya hewa kuwa hata mbaya zaidi, ni muhimu ongezeko la viwango vya joto kubaki kwenye nyuzi joto 1.5C.

Lakina ikiwa tutaendelea vile tulivyo sasa, ifikapo mwisho wa karne hiii ongezeko litafikia nyuzi 4.4C na itakuwa ni janga kubwa.

2. Kupotea kwa maisha ya dunia

Kinyume na mabadiliko ya hali ya hewa hali hii tayari tumeivuka na sasa tuko eneo hatari zaidi na kuongeza uwezekano wa kuwepo mabadiliko makubwa yasiyoweza kurekebishwa katika mazingira. Tumepita mipaka hadi watafiti wanaamini kuwa tuko katika awamu ya sita ya kutoweka kwa historia ya dunia.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuelewa zaidi, kupotea kwa kiwango kikubwa ni wakati ambapo asilimia 60 hadi 90 ya familia ya viumbe ilitokewa kabisa. Kwa mfano kwa familia za wanyama na mimea zilizo duniani, milioni moja ziko kwenye hatari ya kuangamia.

3. Mabadiliko katika matumzi ya ardhi

Matumizi ya ardhi ni kati ya mipaka ambayo tumevuka na inahusu kugeuza misitu, ardhi zenye maji na malisho kuwa ardhi za kilimo na mifugo. Ukataji miti kwa mfano, huwa na athari kubwa kwa uwezo wa mazingiri kuweza kujidhibiti, kitu ambacho watalamu wanarudia kila wakati kunatokea moto katika msitu wa Amazon.

Lakini mabadiliko katika kutumika kwa ardhi ni moja ya sababu za kupungua kwa viumbe kutokana na na kuongezeka kwa hitaji la ardhi ya kuzalisha chakula. Moja ya changamoto iliyopo sasa ni jinsi ya kulisha takriban watu bilioni 8 wanaoishi duniani, na wengine bilioni 2 zaiid ifikapo mwaka 2050 bila kuharibu ardhi zaidi.

4. Mtiririko wa biokemikali

Hii inahusia mtitiriko wa vitu kama phosphorus na nitrogen. Licha ya kuwa hivo vyote ni muhimu kwa ukuaji wa mimea, matumizi yao makubwa kwenye mbolea huziweka kwenye eneo hatari.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Moja ya tatizo linalotokana na hili ni kuwa sehemu ya zile hutumiwa katika kilimo husombwa kwenda baharini ambapo huathiri maisha ya majini.

5. Kuharibiwa kwa ozoni

Kati ya masuala haya tisa ni moja tu ambalo wanadamu walichukua hatua kwa kuona dalili ambalo ni kuharibiwa kwa ozoni.

Kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita dunia nzima ilikubaliana kupiga marufuku kemikali ambazo zlichangia kuweoa shimo kwenye ozoni.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Athari zitokanazo na kupotea kwa ozoni ni pamoja na kuongezeka kwa saratani ya ngozi na kuharibika kwa mazingira.

6. Matumizi ya maji safi

Licha kuwa matumizi ya maji safi yako katika viwango vilivyo salama kwa sasa tunasonga kwa haraka kwenda eneo hatari. Dunia inaiokena kama nukta ya rangi ya bluu kutoka anga za mbali lakini in asilimia 2.5 ya maji safi.

Viwango vya maji safi vinapungua kutokana na kuongezeka shinikizo za kilimo kuzalisha chakula zaidi.

7. Asidi ya bahari

Suala kama hilo hutokea kwa maji ya baharai na yale safi. Mipaka haijavukwa lakini tuko eneo hatari.

Tatizo ni kwamba athari zinafichwa chini ya maji kwa mfano kutokana na kufa kwa matumbawe.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa takriban miaka 200 iliyopita asidi ya bahari imeongekeza kwa asilimia 30, kasi ambayo ni haraka mara 100 kuliko viwango vilivyorekodiwa miaka milioni 55 iliyopita.

Hali hii inahusishwa kwa karibu na mabadiliko ya hali ya hewa na mara nyingi hufahamika kama evil twin

8. Kuachilia erosoli angania

Hii inahusu kuachia angani chembechembe zitokanazo na shughuli za wanadamu ambayo mara nyingi hutokana na kuchomwa kwa mafuta ya kisukuku lakini pia na shughuli zingine kama vile moto wa nyika.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Erosoli huathiri hali ya hewa kwa mfano mabadiliko kwenye monsuni na kwa viumbe kwa mafano watu 800,000 hufa mapema kila mwaka kwa kupumua hewa chafu.

9. Mambo mapya

Jambo la tisa na la mwisho ni kile kinachofahamika kuwa masuala mapya. Hivi ni vitu vinavyotengenezwa na mwanadamu. Vikiwemo vifaa vya mionzi.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini mfano bora zaidi ni vile vinavyofahamika kama CFC ambazo ni zile kemikali zilizopigwa marufuku ili kuokoa gwana la ozoni

Hatua za matumaini

Taasisi ya Stockholm Resilience Center haionyi tu kuhusu masuala yanayohatarisha dunia lakini pia inaleta matumaini. Hatua za haraka zinahitajika kwa kila serikali duniani kwa kuanzia matumizi ya nishati safi.

"Uraibu wetu kwa matumizi ya mafuta ya kisukuku yatupeleka kubaya," alisema katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kwenye mkutano wa COP26. Ulaji wa mboga nyingi, kuokoa nishati, kupanda miti na kuamua kutembea, kutumia baiskeli au usafiri wa umma na hatua madhubuti zinazoweza kuleta mabadiliko.