Mabadiliko ya tabia nchi yataleta mzozo wa kimataifa, ripoti ya kiintelijensia ya Marekani inasema

e Chad in 2007

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chad ni moja ya nchi kadhaa zilizotajwa katika tathmini hiyo kuwa katika hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Mabadiliko ya tabia nchi yatasababisha mzozo wa kimataifa unaondelea, kwa mujibu wa taarifa za kijasusi katika tathimini inayoelezwa kuwa mbaya inayohusu hali ya hewa. Taarifa hiyo ya kwanza ya kiintelijensia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi inaangalia athari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye usalama kuelekea mwaka 2040.

Mataifa yatazozana kuhusu namna gani ya kushughulikia athari ambazo zitazigusa zaidi nchi masikini, nchi ambazo zina uwezo mdogo wa kukabiliana nazo. Ripoti hiyo pia inaonya juu ya hatari ikiwa teknolojia za uhandisi za jiografia za baadaye zitatumiwa na nchi zingine zikiendelea kusimama peke yake.

Tathimini hiyo ya kurasa 27 zinajumuisha maoni ya taasisi zote 18 za kijasusi Marekani. Ikiwa ni ya kwanza ikiangalia mabadiiko ya tabia nchi na usalama wa taifa hilo. Ripoti hiii inatoa picha kwamba kushindwa kwa dunia kushirikiana, kutapelekea kuwa na ushindani wa hatari na kuyumba. Ripoti hiyo imetolewa muda mfupi kabla mwezi ujao Rais nchi hiyo, Joe Biden kuhudhuria mkutano mkubwa wa mabadiliko ya tabia nchi wa COP26 utakaofanyika huko Glasgow, Scotland kutafuta muafaka wa kimataifa.

Ripoti inaionya kwamba nchi zitajaribu kulinda chumi zao na kufaidika kupitia teknolojia mpya. Baadhi ya nchi zitagomea kuchukua hatua, huku zaidi ya nchi 20 zinategemea nishati ya mafuta kwa zaidi ya asilimia 50% ya mauzo yake ya nje.

Ripoti inasema punde tu dunia itashuhudia athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Nchi masikini

Taarifa hiyo ya kijasusi inaanisha nchi 11 na maeneo mawili ambapo, nishati, chakula, maji na afya viko kwenye hatarei zaidi. Joto na ukame kutazidi kutoa msukumo kwenye huduma kama ya usambazaji wa umeme.

Nchi tano kati ya hizo 11 ziko Kusini na Mashariki mwa Asia - Afghanistan, Burma, India, Pakistan na Korea Kaskazini - zingine 4 ziko Amerika ya kati na Caribbean - Guatemala, Haiti, Honduras na Nicaragua. Colombia na Iraq ni nchi zingine kwenye kundi hili. Afrika kati na maeneo mengine madogo huko Pacific yako pia katika hatari.

Kunaweza kuwa na ukosefu mkubwa wa utulivu, haswa kwenye masuala ya wakimbizi, na kwa onyo , hii inaweza kuweka shinikizo zaidi kwenye mpaka wa kusini wa Marekani na kusababisha kuwepo kwa mahitaji mapya ya kibinadamu.

A Russian nuclear-powered icebreaker, the Yamal, in Murmansk

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Chombo cha Urusi kinachoondoa barafu majini ili kutengeneza njia kwa vyombo kupita hasa sehemu zenye baridi sana na kusababisha barani kwneye maji

Upatikanaji wa maji pia utakuwa chanzo cha mzozo ama shida. Katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, karibu asilimia 60% ya rasilimali za maji huvuka mipaka. Pakistan na India zina mizozo ya maji ya muda mrefu. Wakati huo huo, bonde la Mto Mekong linaweza kusababisha mzozo kati ya China na Cambodia na Vietnam, ripoti inaonya.

Teknolojia ya baadaye

Chanzo kingine kinachoweza sababisha hatari ni kwamba nchi inaweza kuamua kutumia teknolojia za uhandisi za jiografia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hii inajumuisha kutumia teknolojia ya wakati ujao, kwa mfano kutumia 'erosoli' kupoza bahari katika eneo fulani.

Lakini kama nchi moja itachukua hatua hiyo peke yake ni rahisi kuhamisha matatizo na athari kwenye eneo lingine na kusababisha hasira kutoka katika mataifa mengine yaliyoathiriwa vibaya au yaliyoshindwa kuchukua hatua kama hiyo.

Watafiti katika nchi kadhaa zikiwemo Australia, China, India, Russia, Uingereza na Marekani, na baadhi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, wanazitazama teknolojia hizi lakini kuna sheria na kanuni chache za kuziongoza.

Kuhimiza ushirikiano

Ripoti hii inasema kuna njia kadhaa zijazo ambazo ni mbaya zinaweza kuepukwa, kwa mfano matumizi ya uhandisi wa kijiografia. Nyingine ni janga la hali ya hewa ambalo hufanya kama chachu ya ushirikiano mkubwa.

Ripoti hii ni ishara kwamba mabadiliko ya hali ya hewa ni jambo muhimu kwenye fikra za masuala ya usalama na kwamba itaongeza shida zilizopo na vile vile zitasababisha shida ama mizozo mipya