Ziwa Maracaibo: Kwa namna gani uchafuzi wa hali ya hewa na umwagikaji wa mafuta umeyabadili rangi ya maji na kuwa kijani?

Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, Nasa Earth Observatory

Maelezo ya picha, Ziwa Maracaibo magharibi mwa Venezuela kwa muda mrefu limekuwa injini ya uchumi wa taifa hilo
    • Author, Daniel González Cappa
    • Nafasi, BBC News Mundo

Janga la athari ya mazingira , uchumi na afya ya umma- hivi ndivyo wataalamu wa mazingira na wanasayansi wanalielezea ziwa la Maracaibo ,muhimili wa sekta ya mafuta nchini Venezuela na uchumi wa nchi hiyo.

Picha za Satelaiti zimebainisha namna ambavyo maji ya ziwa kubwa la Kusini mwa Marekani yalivyoobadilika na kuwa ya kijani na mafuta yakionekana kuelea juu ya uso wa maji.

Imechukua Kilomita 13,000 za mraba kupakana na mkondo wa maji wa bahari ya Caribbean, Inaaminika kuwa ziwa Maracaibo ni moja kati ya maziwa ya zamani zaidi duniani na limekuwa muhimili wa sekta ya mafuta Venezuela kwa miongo, ikifanya mji huo kuwa wa pili kwa ukubwa,

Satellite images of Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, Nasa Earth Observatory

Maelezo ya picha, Picha za setilaiti zilizotolewa na NASA zimeichua kuhusu uvujaji wa mafuta

Vilevile jamii nyingi zimefaidika katika ajira ya uvuvi wa samaki , watu wamepata chakula na uuzaji wa vitoweo vya majini. Picha zilizooneshwa na Nasa hivi karibuni zimebaini uchafu wa rangi ya kijani, kahawia na kijivu ambao unasababisha uasili wa eneo hilo la ziwa kupotea.

Mtaalamu wa bailojia bwana Yurasi Briceño, ambaye alikuwa anafanya kazi katika eneo hilo tangu mwaka 2017, anasema rangi ya kijani inasababishwa na mwani ambao hupata virutubisho katika maji ya ziwa. Ingawa hili linaweza lisionekane kuwa tatizo lakini kwa wavuvi hili ni janga kubwa," bwana Briceño ameiambia BBC.

Satellite images of Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, NASA Earth Observatory

Maelezo ya picha, Rangi ya kijani ni kwa sababu ya uwepo wa mwani

Ingawa hili linaweza lisionekane kuwa tatizo lakini kwa wavuvi hili ni janga kubwa," bwana Briceño ameiambia BBC.Mwani huo umetengenezwa na aina ya bakteria ambao unakuwa kwa kutumia virutubisho.

Athari hizi zimetokana na shughuli za majumbani na uchafu wa viwandani ambao unatupwa karibu na eneo la ziwa au kuelekezwa katika mkondo wa ziwa. Chanzo cha uchafu na mwani kuongezeka katika juu ya maji ya ziwa.

Mwani unazuia kwa jua kupiga katika maji na hata kuzuia majani kuzunguka ziwa yasiweze kuota kwa asili , alieleza. Inazuia mimea mingine kuota kwa kupunguza kiwango cha oksijeni na hivyo kusababisha idadi ya samaki na spishi wengine kupungua.

Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, Getty Images

"Wakati kuna uvamizi mkubwa wa algae,Oksijeni inapotea katika maji, hivyo kunakuwa hakuna oksijeni ya kutosha kwa ajili ya viumbe vyote vinavyohitaji," Briceño anasema.

"Na wanaanza kuona idadi ya samaki ikipungua pia."Mwani unaweza kuwa na aina ya sumu kwa binadamu.

"Wakati samaki anapokula huu mwani na samaki hao wanaliwa na binadamu, hiyo sumu inaweza kwenda kwa mwili wa binadamu na utaweza kuona athari za kiafya zikijitokeza."

Kuvuja kwa mafuta

Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ziwa Maracaibo lina maelfu ya majukwaa ya mafuta na mitambo

BLakini kuvuja kwa mafuta kulionekana na picha za satelaiti , jambo ambalo linawapa wanasayansi hofu zaidi. Ziwa Maracaibo ni eneo kubwa la uzalishaji wa mafuta huko Venezuela na linawakilisha sekta hiyo kwa muda mrefu sana.

Lakini sasa magugu maji yanahatarisha mazingira yake kwa ubora wa maji na afya za watu. Eduardo Klein, mwanasayansi kutoka kituo cha Marine Biodiversity katika chuo kikuu cha Simón Bolívar, anasema kuna zaidi ya maeneo 10,000 ya mafuta katika eneo ambalo linazunguka ziwa, na kukiwa na maelfu ya mabomba chini ya maji .

Baadhi ya mabomba hayo yana zaidi ya miaka 50 na hayajafanyiwa ukarabati mzuri. "Yaliwekwa zamani sana na imekuwa kawaida kuvujisha mafuta kila mara," Klein ameiambia BBC.

The propeller of a boat covered in oil

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meli na boti huathiriwa pia na uchafuzi wa mazingira

Anasema huwa anaangalia picha za satelaiti kila siku kuona sehemu mpya ziliyotoboka.

"Si picha zilizooneshwa na Nasa tu ndio zinabainisha hali hiyo," alisema. "Kila wakati ukiangalia picha za ziwa Maracaibo utaona mafuta yakielea katika maeneo mbalimbali, inaweza kuwa kwenye ziwa au katika ufukwe wa ziwa haswa eneo la mashariki mwa pwani."

Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kumwagika kwa mafuta ni tishio kwa ziwa muhimu zaidi Venezuela

BBC ilijaribu kufanya mawasiliano mara kadhaa na wizara ya nishati na mafuta ya Venezuela bila mafaniko, maofisa wake wakisema hawana mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari.

José Lara, mkuu wa usalama wa majini nchini Venezuela ameiambia BBC kuwa inawezekana kuwa uvujaji wa mabomba ulionekana na alipoulizwa juu ya picha za NASA hata hivyo alisema hawezi kuthibitisha katika hilo.

Ukarabati mbovu

A beach with waves which appear dark with oil

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwambao wa ziwa Maracaibo

Wanasayansi wamepata wakati mgumu kukadiria kiwango cha mafuta kilichomwagika na matukio ya namna hiyo yametokea mara ngapi kwa kuwa kuna takwimu kidogo tu ambazo ni rasmi na picha za satelaiti zinaweza zisieleze kila kitu kwasababu ya mawingu.

Picha za rada ndio chanzo mbadala , lakini haziwezi kuonesha ukweli halisi pia alisema Klein.

Kwa miaka mingi,Venezuela ni taifa linalofahamika katika uzalishaji mkubwa wa mafuta , PDVSA, inaweka mfumo ambao utaweza kufuatilia na kudhibiti utiririkaji wa mafuta.

"Kumwagika kunatokea lakini huwa ni kwa haraka sana," Klein alisema. Lakini hilo sio tatizo kwa sasa.

Fish caught in Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uchafuzi wa mazingira unaathiri wanyama wanaotumiwa na binadamu kama chakula

Bomba la mafuta kutoka ziwa Maracaibo mpaka Cardón na Amuay katika eneo la viwanda katika eneo la jirani la Falcón mabomba yalipasuka kama mara tano katika maeneo matano tofauti ndani ya mwaka mmoja , alisema.

"Na kwa kile tunachokiona , inachukua hata mwezi mmoja bila kufanyiwa ukarabati wa eneo ambalo limepata itilafu. Yani pata picha tu, mwezi mzima hewa chafu inatoka tu ," anasema Klein.

Si ziwa Maracaibo pekee ambalo linaonekana kuvujisha mafuta miaka ya hivi karibuni.

Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakazi wa eneo hilo wa karibu na ziwa Maracaibo wamepata athari za mazingira na afya

Ivan Freites,msemaji wa umoja wa wafanyakazi wa PDVSA anasema matukio kama hayo yanasababishwa na kukosa kwa ufadhili katika utunzaji wa mazingira wa ziwa na fukwe.

Kampuni inasema haina rasilimali au fedha za kuweza kufanyia ukarabati mabomba na viwanda hivyo vya mafuta.

'Athari ya muda mrefu'

A fisherman on the shores of Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jamii zinazoishi katika mwambao wa ziwa zimeathiriwa vibaya

ABaada ya mafuta kutiririka au kuelea katika maji ya ziwa. Maeneo yanayozunguka yanaathirika kwa kiwango kikubwa na hata viumbe wanaathirika kwa kuwa matope yanajitengeneza.

"Tumezoea kuona athari ya mafuta kumwagika kwa ndege na watu wakisafisha fukwe," alisema Klein. Lakini si kwasababu uoni mafuta haimaanishi kuwa tatizo limeisha, bado lipo."

Lake Maracaibo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna ushahidi wa kumwagika kwa mafuta, lakini madhara mengi hutokea kwenye uwanda wa chini wa kitako cha ziwa

Miji kadhaa katika ukingo wa ziwa wanaathirika na sumu ambayo inatoka katika mwani na mafuta. Na athari za kiafya na uchumi zimeanza kuonekana sasa.

Mafuta yanaathiri nyavu zao na kuharibu boti zao. Wavuvi wengi wanakabiliwa na athari kubwa katika maisha yao.

"Matatizo ya mazingira yanasababisha athari za muda mrefu na urithi wa asilia ," Klein alisema.