COP26: Ni kitu gani, kwanini muhimu, na nini tutarajie?

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC
COP26 unafanyika nchini Scotland mwaka huu na matarajio ya tukio hili yanazidi kuwa makubwa. Lakini mkutano huu wa mabadiliko ya tabia nchi una nini hasa?. Kwa makala haya itakusaidia kufahamu masuala muhimu kuhusu mijadala mingi ya mabadiliko ya tabia nchi.
COP26 ni nini?
COP - ni kifupi cha maneno ya kiingereza (Conference of the Parties) - ukiwa ni mkutano wa mwaka ukiyaleta pamoja mataifa 197 duniani kuzungumzia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na namna gani nchi hizo na watu wote wamejipanga kukabiliana na mabadiliko hayo.
Ni sehemu ya maazimio ya umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi - ni mkataba wa kimataifa uliotiwa saini na karibu kila nchi ulimwenguni unaokusudia kupunguza athari za shughuli za kibinadamu kwenye masuala ya hali ya hewa.
COP26 utakuwa mkutano wa 26 tangu makubaliano ama mkataba huo uanze kutekelezwa Machi 21 mwaka 1994. Mwaka huu utafanyika nchini Scotland katika jiji kubwa la Scotland, Glasgow, kati ya Novemba 1-12.
Kwa namna gani COP26 ni muhimu?

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC
Ni muhimu sana. COP26 Utakuwa mkutano wa kwanza utakaoangalia hatua zilizofikiwa mpaka sasa au zilizoshindwa kuchukuliwa tangu makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.(Paris Climate Agreement).
Makubaliano ama mkataba huo, ambao unajulikana pia kama Paris Accord, unajielekeza kuweka mipango ya kuzuia majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi. Mkataba huo unatambua kwamba ikiwa ongezeko la joto ulimwenguni litaendelea kuongezeka zaidi ya 1.5C juu ya hali ya joto tuliyokuwa nayo katika nyakati za kabla ya viwanda, hakutakuwa na mabadiliko mengi makubwa.
Kwa mpango mwingine wowote, unapaswa kujiegemeza kwenye mpango huu, na hapo ndipo mkutano wa COPs unapochukua nafasi yake. Kufikiri kwa pamoja kujadili mbinu mbalimbali na kuhakikisha kila mmoja anawajibika.

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC
Katika mkutabo wa Partis - COP21 - malengo ya msingi yaliwekwa kwa lengo la kuepuka athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi. Nchi zote zilikubaliana:
- Kupunguzu hewa inayosababisha kuongezeka la joto
- Kuongeza uzalishaji wa nishati mbadala
- Joto kuongezeka chini ya nyuzi joto "2C (3.6F) na lengo ni kutovuka nyuzi joto 1.5C (2.7F), na
- Kuwekeza mabilioni ya dola kuzisaidia nchi masikini kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Pia walikubaliana kwamba kila baada ya miaka mitano, watakuwa wanapitia maendeleo na hatua zilizofikiwa. Mkutano wa kwanza ulikuwa ufanyike mwaka 2020 , lakini kutokana na kuwepo kwa janga la corona, mkutano huo wa COP26 ulisogezwa mbelehadi mwaka huu wa 2021.
Janga la Corona limeleta tofauti gani?

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC
Janga limeleta athari kubwa kwa shughuli za kutano huo, sio tu kusababisha kuhairishwa kwa kipindi cha mwaka mzima, lakini kwa upande mwingine, Covid 19 imesababisha watu kufikiria upya kuhusu maisha yatakuwaje baada ya janga. Na kuibua maswali mengi, je tunahitaji kutumia ndege zaidi? au watu kutoka mjini kwenda kuishi vijijini ndio uwe mpango mbeleni?
Tayari, Rais wa Marekani Joe Biden (ambaye alibadili uamuzi wa mtangulizi wake wa kujitoa kwenye makubaliano ya Paris), amezipa kipaumbele sera rafiki za masuala ya hali ya hewa wakati wa mipango yake ya kurejesha hali ya mambo Marekani ukiwemo uchumi. Na watakapokutana kwenye mkutano huo wa COP26, viongozi wenye maamuzi wanatarajiwa kuja na mipango ya muda mrefu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi - na mipango hiyo inatarajiwa kuwa kabambe na yenye kutekelezeka.
Nini matarajio ya COP26?

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC
Mambo mengi yanatarajiwa. La kwanza kuna masuala mengi ambayo hayajapatiwa ufumbuzi kutoka kwenye mkutano uliopita wa COP25 uliofanyika mjini Madrid, Hispania.
Utakumbuka, mwanaharakati kutoka Sweden Greta Thunberg aliyetoa hotuba iliyogusa wakati huo, akiiwaonya viongozi wa dunia juu ya hatari ya hatari za kutokuchukua kwa uzito masuala ya hali ya hewa na kupuuza ushahidi wa kisayansi.
Lakini hata hivyo, haikuweza kusaidia nchi kufikia makubaliano juu ya maswala yenye ubishi. Kwa mfano, mataifa masikini ni kati ya mataifa ya kwanza kuguswa na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Kuongezeka kwa viwango vya bahari taratibu kunameza polepole visiwa, ukame na joto husababisha kuharibika kwa mazao.

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC
Kwa hivyo, kuelekea mkutano wa COP26, zaidi ya mataifa 100 yanayoendelea yataweka mahitaji yao ambayo ni pamoja na:
- Fedha (kutoka kwa nchi tajiri )kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
- Fidia (kutoka nchi tajiri) kutokana na athari zitakazopata, na
- Fedha (kutoka nchi tajiri) kuwasaidia kufufua uchumi wa nchi hizo.
Sasa fikiria kama ni moja ya nchi tajiri. Kwa pamoja zimetenga dola $100bn kufikia mwaka 2020 kwa ajili ya kushughulikia mahitaji hayo. Lakini sasa ni mwaka 2021 na zimeweza kukusanya kiasi cha dola $79bn mpaka sasa, na kiasi kikubwa cha fedha hizo ni mikopo (ambayo inapaswa kurejeshwa), na sio ruzuku (ambayo hakuna kurejesha).

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC
Suala hili - linalojulikama kama fedha za kusadia mabadilko ya tabia nchi - litakua maoja ya jambo litakaloibua mjadala mzito kwenye mkutano huo.
Jambo lingine litakaibua mjadala ni kuhusu namna gani bora ya kushughilia mifumo ya 'carbon markets' na 'carbon credits'. Hii ni mifumo ama njia mbazo zitawaruhusu wachafuzi wa hewa kulipa kama fidia ama fedha kutokana na kuzalisha hewa inayoharibu hali ya hewa na nchi zenye uchumi kuuza 'carbon credits' au kutoa vibali vya kuzalisha kiwango fulani cha hewa isiyofaa. Kama jambo jema, lakini fikiria, nchi tajiri zinalipia 'leseni ya kuchafua hali ya hewa' badala ya kutekeleza mabadiliko ya kweli? Na ni nani anayeamua ni kiasi gani nchi inapaswa kulipa, kwa kwa mfano kwa kukata misitu?
Hata kama mkutano huu wa Glasgow utaweza kukubaliana masuala yote hayo juu, ili kila mtu awe katika njia moja , inahitajika kuweka muda maalumu kwa mipango yote iliyowekwa. Unaweza kusema ni rahisi kutekelezeka lakini ukweli sivyo.

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC
Kwa hivyo, COP26 utakuwa na mlima mkubwa wa kupanda hata kabla ya kuanza kuangalia masuala mapya katika ajenda zake.
Kipaumbele kikubwa itakuwa ni kuzifanya nchi kujitolewa kupunguza uzalishaji wa hewa ya kaboni mpaka kufikia mwaka 2030.
Mipango mingi inatarajiwa kuanzishwa kukabiliana na changamoto mahususi kama kuondoa matumizi ya makaa ya mawe na kulinda mazingira.
Safari hii mwanaharakati Greta hatakuwepo lakini kuna tetesi kwamba huenda Papa akahudhuria kwenye mkutano huo. Kwa vyovyote vile kuna mengi ya kuyafuatilia.















