Fahamu vitu vitano vya kushangaza vinavyoathiri mabadiliko ya tabia nchi

A woman looking surprised

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mambo mbali mbali ya kushangaza yanayoleta hewa ya kaboni, yawe makubwa au madogo

Sote tunafahamu aina za vitu ambavyo vinaweza kupunguza athari yetu kwa ongezeko la joto duniani.

Kupunguza usafiri wa anga, kuanza kutumia magari ya kielektroniki na kula vyakula vitokanavyo na mimea zaidi.

Lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo huenda haujavigundua .

Vitu vitano vya kushangaza vinavyoathiri mabadiliko ya tabia nchi:

1. Wali

A bowl of rice

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wali ni chakula kikuu cha watu bilioni 3.5 kote dunaini

Zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani wanakula wali kama chakula chao kikuu, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Lakini ni zao lenye matatizo kulilima.

Kiasi kikubwa cha maji uhitajika kuyanyunyizia mashamba na kusababisha viumbe wadogo wanaoishi katika udongo wenye unyevu nyevu kutengeneza gesi ya methane, gesi ambayo ni chafu zaidi ya kaboni dioksidi.

Ukulima wa mpunga huchangia 1% hadi 2% ya gesi zote chafu zinazosababishwa na binadamu, na kukata na kuchoma misitu kunakofanywa ili kutengeneza mashamba mapya, pia kunachangia kuachiliwa kwa gesi ya kaboni angani.

Watafiti wanafanya juhudi kote duniani kutengeneza aina mbali mbali za mpunga ambao unaleta mavuno zaidi na ambao utapunguza athari za ukulima katika ongezeko la joto duniani.

2.Utafutaji wa taarifa (searching) mtandaoni

A woman in a dark room on her laptop

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Takriban 60% ya watu dunaini hutumia intanewa taarifa unahitaji kiasi kidogo cha nishati inayotoakaboni diokside

Kila utafutaji wa taarifa katika intaneti huzalisha hewa ya kaboni , kutokana na nishati inayohitajika kuwezesha utendaji wa kifaa chako na nishati ya mtandao usiotumia waya (Wifi)

Inaweza kuonekana ni kiwango kidogo, lakini takwimu za hivi karibuni zinakadiria kuwa kuna watumiaji wa intaneti bilioni 4.66 hivi karibuni athari zake zinaweza kuongezeka kote duniani, kwa hiyo

3. Hifadhi ya maji

A reservoir surrounded by mountains on three sides and a dam at the bottom

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mafuriko ya hifadhi ya maji yanaweza kusababisha kuoza kwa miea asilia na kuzalisha methan

Wakati ardhi imefurika maji kwa ajili ya kutengeneza hifadhi ya maji , mimea na viumbe wengine asilia ambao wamefunikwa huanza kuoza na kutoa hewa ya sumu ya methane-sawa na vile inavyotokea katika mashamba ya mpunga

Watafiti katika chuo kiku cha jimbo la Washington -Vancouver walibaini kwamba hifadhi za maji duniani zina uwezekano wa kuchangia karibu 1.3% ya gesi chafu zinazozalishwa na binadamu kila mwaka-karibu sawa na kiwango kinachotolewa kwa ujumla na Canada.

Hatahivyo, hifadhi nyingi pia husaidia kama vyanzo vya nishati itokanayo na maji.

4. Jibini

Several different kinds of cheese on a table

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jibini huzalisha kiwango kikubwa zaidi cha gesi chafu katika sekta ya maziwa na nyama

Inaweza kukushangaza kufahamu kuwa jibini ni ya tatu kwa kuzalisha hewa ya kaboni katika sekta ya nyama na maziwa baada ya nyama ya ng'ombe na kondoo.

Jibini hutengeneza kila 13.5 za kaboni , kwa kila kilo moja inayoliwa, na kuifanya kuwa juu katika orodha ya vitu vinavyochangia zaidi mabadiliko ya tabia nchi kuliko kuku, nguruwe, na bata.

Karibu lita 10 hutumiwa kutengeneza kilo moja ya jibini kutokana na mchakato wa ukuaji wake, ingawa jibini laini hutumia maziwa kidogo, kwahiyo inakuwa na athari ndogo ya kimazingira.

Sekta ya maziwa duniani huzalisha karibu 4% ya gesi chafu inayozalishwa na binadamu na bidhaa nyingine za maziwa zitokanazo na wanyama huhusika kwa sehemu moja, kwani hutoa kiwango kikubwa sana cha methane, ambayo tunafahamu kuwa husababisha uharibifu mkubwa angani kuliko Kaboni diokside.

5. Kuwaelimisha wasichana

Two girls in uniform smiling with exercise books

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Elimu huwajengea uwezo wanawake na wasichana jambo linalosaidia katika kuimarika kwa njia ya kudumu kwamazingira ya kijamii

Utafiti umeonyesha kwamba wakati wanawake na wasichana wanapokwenda shule na wakiwa na fursa sawa, hii ina huimarisha mikakati ya mazingira kwa njia kadhaa tofauti.

Mwanamke ambaye amemaliza masomo yake ya shule ya sekondari ana uwezekano mkubwa wa kuwa na watoto wachache zaidi katikamaisha yake kuliko mwanamke ambaye alimaliza shule ya msingi pekee.

Unaweza pia kusoma:

Kupungua kwa kiwango cha uzazi kuna athari chanya kwa dunia kwa kupunguza ongezeko la idadi ya watu na hivyo kupunguza watu wanaotengeneza hewa ya kaboni.

Elimu pia huwajengea uwezo wanawake na wasichana wa kuwa viongozi wanaodhibiti mabadiliko ya tabia nchi. Tafiti zimeonyesha kuwa nchi zenye idadi kubwa ya wanawake bungeni zina uwezekano mkubwa wa kuishinisha mikataba ya kimataifa ya mazingira, kulinda maeneo ya ardhi, na zina sera madhubuti za mabadiliko ya tabia nchi.