COP26: Viongozi wa Ulimwengu waahidi kukomesha ukataji miti kufikia 2030

TH

Chanzo cha picha, Getty

Zaidi ya viongozi 100 wa dunia wataahidi kukomesha na kubadili athari za ukataji miti ifikapo mwaka 2030, katika mkataba wa kwanza mkuu wa mkutano wa kilele wa COP26.

Brazil, ambapo sehemu kubwa za msitu wa Amazon zimekatwa, itakuwa miongoni mwa watia saini siku ya Jumanne.

Ahadi hiyo inajumuisha karibu £14bn ($19.2bn) ya fedha za umma na binafsi.

Wataalamu walikaribisha hatua hiyo, lakini walionya mpango wa awali mwaka 2014 "umeshindwa kupunguza ukataji miti hata kidogo" na kujitolea kunahitajika kutekelezwa.

Kukata miti huchangia mabadiliko ya hali ya hewa kwa sababu hupunguza misitu ambayo inachukua kiasi kikubwa cha gesi ya joto CO2.

Mkutano wa kilele wa wiki mbili huko Glasgow unaonekana kuwa muhimu ikiwa mabadiliko ya hali ya hewa yatadhibitiwa.

Nchi zinazosema zitatia saini mkataba huo , zikiwemo Canada, Brazili, Urusi na Indonesia, zinasheni karibu asilimia 85 ya misitu duniani.

Baadhi ya ufadhili huo utakwenda kwa nchi zinazoendelea kurejesha ardhi iliyoharibiwa, kukabiliana na moto wa nyika na kusaidia jamii za kiasili.

Serikali za nchi 28 pia zitajitolea kuondoa ukataji miti kutoka kwa biashara ya kimataifa ya chakula na bidhaa nyingine za kilimo kama vile mawese, soya na kakao.

Viwanda hivi vinasababisha upotevu wa misitu kwa kukata miti ili kutoa nafasi kwa wanyama kutumia kama malisho au mimea kukua.

Zaidi ya makampuni 30 makubwa duniani yatajitolea kukomesha uwekezaji katika shughuli zinazohusishwa na ukataji miti.

Na mfuko wa £1.1bn utaanzishwa kulinda msitu wa pili kwa ukubwa duniani wa kitropiki - katika Bonde la Congo.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ambaye ni mwenyeji wa Mutano wa wa dunia unaofanyika Glasgow, atayaita "lmakubaliano ya kihistoria ya kulindana kurejesha misitu ya dunia ".

"Hizi timu za mifumo ya ikolojia-hizi - ni mapafu ya sayari yetu ,"anatarajiwa kuwaamba wajumbe waliohudhuria mkutano huo

Profesa Simon Lewis, mtaalamu wa hali ya hewa na misitu katika Chuo kikuu cha London alisea, : "Ni habari njema kuwa na utashi wa kisiasa kutoka nchi mbali mbali wa kujitolea kumaliza uangamizaji wa misiti kutoka, na kuwepo kwa ufadhili muhimu wa kuendelea mbele na safari ."

Lakini aliiambia kuwa dunia "imekuwepo hapa kabla" kukiwa na azimio la New York la mwaka 2014 "ambalo lilishindwa kupunguza ukataji wa misitu kabisa".

Aliongeza kuwa mkataba huu mpya haikusaidia kukabiliana na ongezeko la utashi wa bidhaa kama vile nyama zinazokuzwa kwenye ardhi ya misitu ya mvua -jambo ambalo litahitaji viwangio vya hali ya juu vya ulaji katika nchi kama vile Marekani na Uingereza kulitatua.

Mkurugenzi mkuu katika Chatham House Sustainability Accelerator, Ana Yang, ambaye alikuwa mwandishi mwenza wa ripoti kuhusu uhifadhi wa msitu wa Amazon nchini Brazil iliyoitwa Rethinking the Brazilian Amazon, alisema:. "Mkataba huu unahusisha nchi zaidi, wahusika zaidi. Lakini shetani yuko katika maelezo ambayo bado tunahitaji kuyaona.

"Hii kusema kweli ni hatua muhimu katika COP26. Huu ni mkutano kuhusu kuongeza kiwango cha utashi na kuviweka viwango ongezeko la joto la dunia chini ya nyuzi joto 1.5 - huu ni msingi imara ," aliongeza.

Maelezo ya msingi kuhusu mkutano wa COP26

  • Mabadiliko ya tabia nchi ni moja ya matatizo makubwa ya muhimu zaidi ya dunia. Serikali lazima zitoe ahadi zaidi za kupunguza gesi zinazosababisha ongezeko la joto iwapo tutazuwia ongezeko kubwa zaidi la joto duniani
  • Mkutano wa Glasglow ni mahala ambapo mabadiliko yanaweza kutokea. Unahitaji kutazama ahadi zinazotolewa na wachafuzi wakuu wa dunia, kama vile Marekani na Uchin, na iwapo nchi masikini zinapata usaidizi wanaouhitaji.
  • Maisha yetu yote yatabadilika. Maamuzi yatakayochukuliwa hapa yanaweza kuathiri ajira zetu, jinsi tunavyochemsha nyumaba zetu, kile tunachokula na jinsi tunavyosafiri

Tuntiak Katan, kutoka taasisi ya ya uratibu wa jamii za wazawa wa Amazon Basin, aliafiki mkataba, akiiambia BBC kwamba jamii za wazawa walikuwa mstari wa mbele katika kuzuwia ukataji wa miti.

Bw Katan, ambaye ni kutoka jamii ya wazawa ya Shuar kutoka nchini Ecuador, alisema kuwa jamii za wazawa kote duniani zililinda 80% ya bayoanuwai ya dunia nzima lakini zilikabiliwa na vitisho na ghasia.

"Kwa miaka mingi tumekuwa tukilinda njia zetu za maisha na hilo limelinda mifumo ya ikolojia na misitu. Bila sisi, hakuna pesa wala sera inayoweza kuzuwia mabadiliko ya tabia nchi," alisema.

Deforestation has accelerated in the Amazon in recent years

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ukataji wa miti umekuwa ukiongezeka kwa kasi katika Amazon katika miaka ya hivi karibuni

Watakaosaini mkataba ni pamoja na nchi kadhaa muhimu.

Indonesia ni muuzaji mkuu wa Mafuta ya mitende duniani, zao linalopatikana katika bidhaa mbali mbali kuanzia sabuni za shampoo hadi katika biskuti .

Uzalishaji unaaangamiza mti na kupoteza eneo la watu wa jamii za wazawa.

Wakati huo huo misitu mikubwa asili ya Urusi, yenye zaidi ya moja ya tano ya misitu iliyopo katika sayari ya dunia, huvuta zaidi ya tani bilioni 1.5 za hewa ya kaboni kila mwaka.

Katika msitu mkubwa zaidi katika sayari yetu wa Amazoni ukataji wa misitu uliongezeka kwa kasi hadi mara 12 kwa mwaka katika mwaka 2020 chini ya utawala wa rais wa Brazil President Jair Bolsonaro.

"Kwa Brazil kuweza kusaini mkataba ni jambo muhimu kusema kweli kwasababu ina misitu mikubwa zaidi ya kitropiki. Lakini pesa lazima zifikishwe kwa watu ambao wanaweza kuifanya kazi hii katika maeneo yenyewe ya misitu," Bi Yang alisema.

Watu wengi wanaoishi katika Amazon, ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi katika maeneo yake ya miji, hutegemea msitu kwa ajili ya maisha yao ya kila siku na wanahitaji usaidizi katika kupata vipato vipya vya kujikimu kimaisha, aliongeza.

Miti ni moja wapo ya vitu vinavyozuwia ongezeko la joto duniani. Inavuta hewa ya kaboni dioxidenje ya hewa. Inafyonza karibu theluthi moja ya hewa chafu CO2 inayotolewa duniani kila mwaka.

Kwa sasa eneo la msitu lenye ukubwa wa viwanja 27 vya mpira wa miguu hupotea kila dakika.

Misitu inayotokomea pia inaweza kutoa hewa ya CO2. Iwapomiti mingi sana itakatwa, wnasayansi wana hofu kwamba sayari yetu inaweza kufikia kiwango cha mabadiliko ambayo yanaweza kuwa ya ghafla na ya kutotabilika ya mabadiliko ya tabia nchi.

Footer - Blue