Mabadiko ya hali ya hewa: Hali ya maisha maeneo yenye nyuzi joto 50

Graphic image showing someone looking into the sun and alongside a photo of the Earth

Suala la athari za mabadiliko ya hali ya hewa sio tena la siku za usoni. Sehemu nyingi duniani tayari zimeanza kuonekana.

Mamilioni ya watu wanaishi katika mazingira yenye viwango vya juu vya joto, wakikabiliwa na tisho linaoongezeka la mafuriko na moto wa nyika. Hapa watu watano wanaeleza jinsi viwango vya juu vya joto vimebadilisha maisha yao.

'Mara nyingi hatupati usingizi'

Woman wiping sweat from her brow

Shakeela Bano wakati mwingine hutandika mito yao kwenye paa la nyumba yao ya ghorofa moja nchin India. Siku zingine joto haliwaruhusu kulala ndani ya nyumba. Paa linaweza kuwa moto hata kwa kutembea. "Ni vigumu sana," anasema. "Siku nyingi hatupati usingizi."

Shakeela anaishi na mumewe, binti yao na wajukuu watatu, kwenye chumba kisicho na dirisha huko Ahmedaab, Wako na kipepeo kimoja kwenye dari kinachawasaidia kupata upepo.

Mabadiliko ya hali ya hewa yanamaanisha miji mingi nchini India sasa inkumbwa na joto la hadi nyuzi 50C. Maeneo yenye misongamano na yaliyojengwa sana yanakumbwa na kile kinachojulikana kama visiwa vya joto.

Maelezo ya video, Maisha katika nyuzi joto 50: Suluhisho rahisi kupoza nyumba yako

Vifaa vya kujenga kama saruji hunasa joto na kuchania kuongezeka viwango vya joto.

Kwenye nyumba kama za Shakeela, joto hufika hadi nyuzi 46C.

'Joto kama moto'

Sidi Fadoua

"Ninatoka eneo lenye joto," anasema Sidi Fadou. Lakini joto lililo kaskazini mwa Mauritania, magharibi mwa Afrika, sasa ni la juu zaidi kwa watu kuishi na kufanya kazi. Joto lililo hapa sio la kawaida, anasema. "Ni kama moto."

Sidi mwenye umri wa miak 44 anaishi katika kijiji kidogo karibu na jangwa la Sahara. Anafanya kazi kama mchimba chumvi maneo yaliyo karibu. Kazi ni ngumu, na imekuwa vigumu zaidi kwa sababu eneo hilo huwa joto kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. "Hatuwezi kusahimili joto kama kama hilo," amasema. "Sisi sio mashine."

Ili kuepuka joto la zaidi ya nyuzi 45C msomi wa masuala ya joto, Sidi amenza kufanya kazi usiku. Wale waliokuwa wanapata riziki kutoka kwa mifugo hawana tena kwa sababu hakuna lishe tena kwa mbuzi na kondoo wao.

Kwa hivyo kama majirani zake, Sidi anapanga kuhamia mji wa pwani wa Nouadhibou ambapo mawimbi ya bahari huchangia mji kupata upepo mzuri

"Watu wanahama eneo hili," anasema Sidi. Hawawezi kustahimili joto tena.

Huko Nouadhibou , ana matumaini ya kupata kazi katika sekta ya uvuvi. Upepo wa bahari unaweza kuwa suluhu, lakini kutokana na idadi kubwa ya watu wanaolikimbia jangwa, nafasi za ajira zimekuwa adimu, lakinia Sidi bado ana matumaini.

'Unazima moto kwa njia gani?'

Patrick Michell

Patrick Michel, Chifu wa eneo la Kanaka Bar First Nation, kwanza alianza kutambua mabadiliko ya kutia hofu kwenye msitu karibu na hifadhi yake huko British Columbia, Canada zaidi ya miongo mitatu iliyopita.

Kulikuwa na upungufu wa maji mitoni na uyoga ukaanza kuota

Msimu huu wa joto hofu zake zikageuka kuwa ukweli. Wimbi la joto likazuka Amerika kasakzini. Juni 29 mji wa nyumbani kwake wa Lytton ulivunja rekodi na kufikia nyuzi 49.6C. Siku iliyofuatia mkewe akamtumia picha ya kipima joto chenye vipimo vya nyuzi 53C. Saa moja baadaye mji wake ulikuwa umeshika moto.

Binti yake, Serena, aliyekua na ujauzito wa miezi 8, akang'ang'ana kuwachukua watoto na vitu vichache kwenye gari lao, "tuliondoka na nguo zetu migongoni, moto ulikuwa mkubwa."

Patrick akakimbia kuona iwapo anaweza kuokoa nyumba, amekua akikabiliana na moto tangu awe mdogo. Lakini kama hali ya hewa ilivyobadilika moto nao umebadilika. "Unazima kwa njia gani moto mkubwa kama huu?"

Licha ya yale yaliyoikumba familia, Patrick alikiona kile kilichotokea kama fursa: "Tunaweza kuujenga tena mji wa Lytton kuambatana na mabadiliko ya hali ya hewa miaka 100 inayokuja."

'Nilipokuwa mtoto haikuwa hivi

Joy

Nilipokuwa mtoto hali ya hewa haikuwa hivi, anasema Joy, anayeishi huko Niger Delta nchini Nigeria. Eneo hilo ni kati ya yaliyochafuliwa zaidi dunaini, na siku zenye viwango vya juu vya joto zinazidi kuongezeka.

Joy anailisha familia yake kwa kutumia moto kutoka kwa gesi zinazovuja kuchoma mihogo anayouza sokoni, "Nina nywele fupi, kwa sababu ikiwa nitaacha nywele ziwe ndefu inaweza kuchoma kichwa changu ikiwa moto utakuja upande wangu au utalipuka."

Maelezo ya video, Jinsi wakazi wa Australia wanavyoathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa

Lakini moto ni sehemu ya tatizo lililopo. Kampuni za mafuta hutumia moto kuchoma gesi inayotoka ardhini wakati wanachimba mafuta. Moto unaopaa juu hadi mita 6 ndio chanzo cha gesi ya kaboni inayochangia mabadiliko ya hali ya hewa.

Mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa yenye athari kubwa hapa, yamegeuza ardhi yenye rutuba kuwa jangwa maeneo ya kaskazini, huku mafuriko yakilikumba eneo la kusini. Watu hawakumbuki uwepo wa hali kama hizo walipokuwa wadogo.

"Watu wengi hapa hawafahamu vizuri kuweza kuelekeza ni kwa nini hali ya hewa inabadilika kwa haraka," anasema Joy. Lakini tunashukuru mioto hii ambayo imewaka kwa muda mrefu, anaitaka serikali kupiga marufuku uchomaji wa gesi hata kama anaitegemea kulisha familia yake.

Hakuna utajiri wa mafuta umewekezwa nchini Nigeria ambapo watu milioni 98 wanaishi katika hali ya umaskini . Hawa ni pamoja na Joy na familia yake. Kwa siku tano za kufanya kazi hupata pauni 4 kama faida.

'Joto si la kawaida'

Om Naief

Miaka sita iliyopita, Om Naief alianza kupanda miti sehemu ndogo ya jangwa kando na barabara. Baada ya kustaafu kutoka ajira ya serikali nchini Kuwait alikuwa na wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa joto na vumbi jangwani.

'Nikazungumza na maafisa. Wote wakasema ni vigumu kupanda chochote kwenye mchanga.

"Nilitaka kufanya kitu ambacho kitashangaza kila mtu."

Om anaishi Mashariki ya Kati, eneo linalokumbwa na joto linaloongeza kwa kasi kuliko maeneo mengine duniani. Kuwait inaelekea kukumbwa na joto ambalo halitastahimilika - mara nyingi kuna joto la zaidi ya nyuzi 50C. Utabiri unaonesha kuwa viwango vya joto vitaongrzeka kwa nyusi 4 ifikapo mwaka 2050.

Watu nchini Kuwait sasa wanaitaka serikali ipande miti mingi. Matumaini yao ni kwamba Kuwait iko tayari kusimama kidete dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Om anasema ni lazima walinde ardhi wasiiache ikauke.

"Joto si la kwaida hapa," Om anasema. "Hii ni ardhi ya mababu zetu na hivyo lazima turudishie, kwa sababu imetupa mengi.

Unaweza pia kusoma: