Angelina Vunge: Mwafrika wa kwanza mbunge Uruguay aliyeingia nchini humo miaka 20 iliyopita bila stakabadhi halali

Angelina Vunge arrived in Uruguay 20 years ago without papers and last month she became the first African legislator in the Uruguayan Congress.

Chanzo cha picha, JAVIER NOCETI

Mnamo Aprili 14, 2021, Angelina Vunge alichaguliwa kama mbunge wa chama tawala cha National Party katika bunge la Uruguay .

Spika wa Bunge la wawakilishi alipompa nafasi ya kuzungumza, akasema: "Niamini ninaposema ni muhimu leo mimi kuwa hapa. Ni siku maalum sana kwangu." Huku sauti yake ikisikika kama yenye kukwaruza kwa mbali kabla ya kurejelea mjadala uliokuwa unapigiwa kura siku ile.

Haingekuwa jambo kubwa kwa mwanamke kuwa mbunge wa kiti ambacho kimeachwa na mwanaume kama haingekuwa kwa Angelina Vunge, raia wa Angola ambaye alihangaishwa kupitia ajira ya watoto , alinyanyaswa katika ndoa na kupitia manyanyaso mengine ya kingono, aliyetoroka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwake (1975 - 2002) na kuwasili Uruguay miaka 20 iliyopita bila stakabadhi halali, akiwa hajui lugha ya nchi hiyo, hakuwa na pesa wala kazi.

Na mwezi uliopita alitangazwa kuwa mbunge wa kwanza mwafrika katika bunge la Uruguay.

Vunge, 42, alizaliwa katika familia maskini katika kijiji kimoja kusini mwa Angola.

Aliishi vijiji tofauti na katika kila kijiji pamoja na kwenda shule, yeye pamoja na ndugu zake wanne walikuwa na jukumu la kutekeleza walilopewa na baba yao.

Akifanya kazi ya shamba, pia walikuwa wanakata na kubeba kuni, wanatengeneza unga na kuchukua mmea wa moringa kandokando ya mto na kusafisha nyumba iliyokuwa imejengwa kwa minyaa, mbao na udongo.

Alikwenda shuleni miguu peku

"Kama nisingesoma au nisingefanya kazi ya nyumbani ningelazimika kuelezea kwanini sijafanya, kabla sijachapwa viboko na baba. Kwanza mimi, kisha mama yangu kwasababu aliamini kuwa ikiwa nimeshindwa kufanya majukumu yangu, kosa ni la mamangu kwa kushindwa kunielekeza vyema,"Vunge alielezea BBC Mundo.

Alipitia kichapo kile kile shuleni ikiwa angeandika neno vibaya au angeshindwa kufanya hesabu. Alipiga magoti juu ya mawe mawili na kubeba vitu viwili vizito kwa mikono yake huku ikiwa imenyooshwa, amesema.

Angelina walked ten kilometers a day to go to school, barefoot.

Chanzo cha picha, Getty Images

Angelina, alitembea kilomita 10 kila siku kwenda shuleni akiwa miguu peku.

Akiwa na miaka minane, kwa bahati mbaya alivunja panga wakati analinoa kwa jiwe akiwa anataka kwenda kutafuta kuni. Baba yake akajua alichofanya na kama kawaida akampa kichapo cha nguvu kwanza kabla ya mama yake kuwa wa pili.

Angelia, ipo siku ambayo baada ya kufanya makosa aliamua kumfunga ndugu yake mdogo mgongoni akidhani hiyo itakuwa njia moja ya kukwepa kichapo asijue kuwa baba yake akiamua kumpiga hakuna kitakachomzuia.

Unyanyasaji aliopitia

Angelina anasema kuwa alipitia unyanyasaji kadhaa wa kingono nchini Angola na hakuwahi kusema aliyopitia kwa mtu yeyote

Anakumbuka mara ya kwanza akibakwa akiwa na umri wa miaka 4 na kijana ambaye alikuwa amechaguliwa na familia yake kama mume ambaye angemuoa "akishaanza kuota matiti."

Angelina Vunge suffered multiple sexual abuse during her childhood.

Chanzo cha picha, JAVIER NOCETI

Angelina Vunge alinyanyaswa kingono mara kadhaa akiwa mtoto.

Unyanyasaji huo ulirejelewa akiwa na miaka 7. Familia ya Angelina ikahamia kijiji kingine na huko pia akanyanyaswa tena.

"Núñez, mwanamume aliyembaka alikuwa jamaa yake na alifanya hivyo mara nyingi, tangu nikiwa na miaka 4 na hata kukiuka baadhi ya tamaduni zilizokuwa zinakumbatiwa kijijii: kwamba wanawake wanastahili kulindwa na kuwa wanastahili kuolewa wakiwa bikra", amesema kwenye kitabu chake.

"Mwanamke anayebakwa anasalia kimya siku zote lakini cha ajabu wanaotekeleza ubakaji hakuna hata siku moja wanaadhibiwa (...) Familia yake ilikuwa wapi wakati anamlaza mkekani na kumfanya kitendo kibaya? Nililia lakani alinionya nisijaribu kusema kwa yeyote". Anasema kuna mengine ambayo atasalia nayo moyoni mwake milele.

Alishuhudia unyanyasaji katika ndoa

Akiwa na umri wa miaka, 9, tayari alikuwa ameathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na unyanyasaji kwenye ndoa, Angelina aliapa kusoma kwa bidi na kufanya kazi, nia yake ikiwa ni kuweka akiba aweze kuhamia nchi nyengine.

Mwaka mmoja kabla, alikuwa ameshuhudia kuwa mgogoro mdogo tu, baba yake alikuwa anakaribia kumpiga mama yake kiasi hata cha kutaka kumuua. Mara kadhaa, alimuona mama yake akiwa chini anagaraza, damu zinamtoka.

Angelina began working cleaning family homes, learned Spanish, and got a job as a waitress in a restaurant.

Chanzo cha picha, JAVIER NOCETI

Baba yao alipokuwa amekwenda kutafuta fimbo ya kuendelea kumchapa mama yake, pacha wao wa kiume, walijitahidi kumsihi baba yao aende kwa wake wengine.

Kusaka pasipoti kulimwendea mrama

Akiwa na miaka 14, alitaka kupata pasipoti yake ili ahamie nchi nyingine. Hakuwa na uwezo wa kufikia intaneti na alichofanya ni kuanza kuuliza usaidizi kwa majirani.

Lakini kosa alilofanya ni kuamini kundi fulani la wavulana waliomuahidi kumtafutia, kwasababu walikuwa na ufahamu na mchakato unavyokwenda katika ofisi ya serikali.

Siku moja mchana, walimuita nyuma ya jengo la polisi wakiwa wamemuitisha picha za pasipoti.

Lakini baada ya kuingia kwenye jengo hilo, wavulana wawili walikuwa wanamsubiri. "Funga bakuli lako, mmoja wao akaniambia, kwasababu ukipiga kelele tutaita wavulana wengi zaidi. Wakanirusha kwenye godoro tayari nikiwa ninajua nini kingefuatia

Saa kadhaa baadaye, akaondoka jengo hilo akiwa hana pasipoti na mwenye majeraha makubwa moyoni.

"Uruguay kuna vita?"

Angelina akiwa anafanya kazi katika mgahawa wa Umoja wa Mataifa.

Mwaka 1996, alikutana na Cristina Benítez, mwanajeshi wa Uruguay aliyekuwa nchini mwake kwa ajili ya kulinda amani.

Benítez alisafiri mara tatu kwa wiki katika miji mbalimbali nchini Angola kutoa huduma za chakula na mavazi kwa waasi wa UNITA ambao walikuwa wameamua kuweka silaha chini.

The first thing Angelina asked when they asked her to go to Uruguay was: "Is there a war in Uruguay?"

Chanzo cha picha, JAVIER NOCETI

Wakati wa chakula cha mchana, Angelina na Cristina walikuwa wakipiga gumzo kwa lugha ya Kireno.

Mwanamke huyo wa Angola alimwambia kwamba anataka kuhamia nchi nyingine na anafikiria kujaribu bahati yake katika nchi ya Ureno au Brazil kwasababu ya lugha. Benítez akasema atamsaidia kumpa kazi kwake huko Montevideo.

Cha kwanza Vunge kumuuliza ni: "Uruguay kuna vita?"

"Hapana, hakuna vita. Kilichopo ni baridi kali kwasababu kuna misimu minne. Hali ya hewa ani tofauti kabisa, sio kama hapa."

"Huko pia wanatembea polepole kama ilivyo kwa wanajeshi wa Uruguay hapa?" Nikamuuliza.

"Mara ya kwanza kuwaona, nilidhani wanaishi kwa kutegemea dawa za kulevya siku nzima."

Kutoka Angola hadi Montevideo

Benítez akamshauri: asubiri mkataba wake na Umoja wa mataifa utakapokamilika atakwenda, na kipindi kilichosalia akawa anaweka akiba akitafuta pesa za usafiri.

Novemba 28, 1999, akawasili Montevideo.

Nelson, dereva wa taksi, akachanganywa na uzuri wa Kiafrika akidhania kwamba ni Mbrazil. Alijitambulisha kama mpwa wa mgombea urais wakati huo, kwasababu kilikuwa kipindi cha uchaguzi na akajitolea kumsaidia kupata makaratasi ya kupata kitambulisho cha makazi na hatimaye uraia.

Angelina Vunge sold more than five editions of her autobiographical book.

Chanzo cha picha, JAVIER NOCETI

Wakaanza kuwa wachumba na kufahamiana zaidi na hatimaye wakaoana. Wakajaaliwa watoto wawili ambao sasa hivi ni vijana. Angelina akaanza kufanya kazi ya usafi katika familia za Kihispania na baadaye akapata kazi kwenye mgahawa.

Siku moja akiwa kazini, akapata fursa ya kumhudumia kiongozi mmoja wa kisiasa, Alem García, wa chama tawala. García alimuuliza anatoka wapi na kwanini mwanamke wa Angola ameishia kufika Uruguay.

"Mimi niingie kwenye siasa? Hapana"

Mwasiasa huyo aliendelea kwenda kwenye mgahawa huo ili apate fursa ya kuzungumza naye. Siku moja akamwambia: "Simulizi yako ni ya kuandika kitabu!" na "unachofaa ni kuingia kwenye siasa."

Angelina akaonesha kutokubaliana naye. Na kuongeza: "Siasa, Mimi niingie kwenye siasa? Hapana."

Wiki moja baadaye akakutana na kampuni moja ya uchapishaji vitabu. Na baada ya kusikiliza simulizi yake, wakakubaliana kwamba kuna haja ya kuandika kitabu kinachoangazia maisha yake.

Angelina aliuza zaidi ya matoleo matano ya kitabu chake, akapata kazi katika taasisi ya matibabu, akatalakiana na Nelson, akaanza kuwalea watoto wake peke yake na baadaye akapata fursa ya kuwa afisa wa jeshi wa chama tawala, kama tu alivyokuwa ametabiriwa.

Mwaka 2019 mwishoni, chini ya aliyekuwa rais, Juan Sartori, Angelina aliongoza katika moja ya wagombea wa bunge la wawakilishi na kwa mara nyingine tena, García akampendekeza na kumpigia debe.

Alikuwa amejiwekea lengo hilo miaka kumi iliyopita akiwa anafanyakazi mgahawani.

Akiwa anapita nje ya jengo hilo na vijana wake Ellery (20) na Ian (15) aliwaambia, akijibashiria bila kujua: "Ipo siku nitakuja kufanyakazi katika jengo hili. Sijui nitakuwa kama mfanya usafi, muuza kahawa au mlinzi lakini lazima nitakuja kufanya kazi hapa".

Na Novemba 2019, ndoto yake ikatimia alipochaguliwa kama mbunge wa chama tawala na Aprili 14 akaanza kutekeleza majukumu yake.