Jinsi gani wadukuzi waliweza 'kuteka' bomba la mafuta?

oil worker and cyber imagery

Chanzo cha picha, Getty Images

Wachunguzi katika bomba kubwa la mafuta huko Marekani wanafanya kazi ya kuangalia namna ya kujinasua katika shambulio kubwa la kimtandao ambalo limevuruga mfumo wa usambazaji wa mafuta.

Udukuzi wa bomba kubwa la mafuta la Colonial umeonekana kuwa na athari kubwa katika historia ya miundombinu ya kitaifa nchini humo.

Bomba hilo usafirisha karibu nusu ya mafuta yote yabayotumiwa katika majimbo ya Pwani ya Mashariki ya Marekani na bei zinatarajia kuongezeka kama tatizo hili litaendelea kwa muda mrefu.

Bomba la mafuta linawezaje kudukuliwa?

Kwa watu wengi, picha ya kiwanda cha mafuta inayowajia kichwani ni ya mabomba, pampu na vifaa vingine vikuukuu viliyopiga weusi kwa uchafu wa mafuta.

Ukweli ni kuwa bomba la Colonial linafanya kazi kwa njia ya kidigitali.

Mabomba na vifaa vyote vinavyotumika kuangalia na kudhibiti usambazaji wa mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya ndege katika mamia ya maili vinafanya kazi kidijitali.

Colonial inatumia teknolojia ya kiwango cha juu kuendesha operesheni za bomba hilo.

The Colonial Pipeline

Chanzo cha picha, Colonial Pipeline

Maelezo ya picha, Bomba hilo la Colonial linasafirisha mapipa milioni 2.5 kila siku

Operesheni zote za teknolojia hii zimeunganishwa na mfumo mmoja.

Na wataalamu wa masuala ya mtandao kama kama Jon Niccolls kutoka taasisi ya CheckPoint, anaeleza kuwa popote pale kwenye kuunganisha mfumo kuna hatari ya uvamizi wa kimtandao:

"Vifaa vyote ambavyo vinatumika kuliendelesha bomba hili la kisasa vinatumia kompyuta badala ya kudhibitiwa na watu," amesema.

"Kama vifaa hivyo vimeunganishwa kupitia mtandao wa ndani wa kampuni na ukadukuliwa, basi bomba lenyewe linakuwa limeathirika katika shambulio baya la kimtandao."

Wadukuzi waliwezaje kuchukua hatamu ya bomba hilo?

COLONIAL PIPELINE

Chanzo cha picha, COLONIAL PIPELINE

Shambulio la moja kwa moja katika operesheni ya kiteknolojia huwa ni nadra kwa sababu mifumo hii huwa inalindwa vizuri, wataalamu wanasema.

Hivyo inawezekana mdukuzi alifanikiwa kupata fursa ya kuingia kwenye komputa yenye mfumo wa Colonial kutoka upande wa utawala wa bomba hilo.

"Baadhi ya mashambulio makubwa tumeona yakianzia kwenye barua pepe," bwana Niccolls amesema.

"Mfanyakazi anaweza kurubuniwa kupakuwa mfumo wa wizi wa mtandaoni , kwa mfano.

"Hivi karibuni tumeona wadukuzi wakitumia udhaifu wa kutumia programu ya kompyuta.

"Wadukuzi wanaweza kutumia njia yeyote ya kuingia kwenye mtandao."

Wadukuzi wanaweza kuwa ndani ya mtandao wa taarifa za kiteknolojia wa Colonial kwa wiki kadhaa au hata miezi kabla ya kutangaza kuwa wamefanya uvamizi.

Hapo nyuma, wahalifu waliweza kusababisha ghasia baada ya kupata njia ya kuingia kwenye programu za operesheni za kiteknolojia.

Mwezi Februari, wadukuzi wamepata mfumo wa maji wa mji wa Florida na walijaribu kuvuta kemikali hatari katika mabomba hayo.

Mfanyakazi aliona jinsi ilivyotokea katika kompyuta na kusitisha shambulio katika gari lake.

Sawa kabisa na wakati wa msimu wa baridi wa mwaka 2015-16, wadukuzi nchini Ukraine walifanikiwa kuzima mtambo wa kidigitali na kusababisha athari kwa mamia na maelfu ya watu.

Hili linaweza kuzuiliwa vipi

Namna nzuri ya kulinda operesheni za kiteknolojia ni kuzizima na kutounganisha na intaneti kabisa.

Lakini katika hili biashara inakuwa ngumu, wanategemea kuunganisha vifaa kwenye mtandao ili viweze kufanya kazi kwa ufasaha.

"Kwa kawaida , kampuni inaacha mwanya'," Mtaalamu wa usalama wa mtandao Kevin Beaumont amesema.

man at pipeline terminal

Chanzo cha picha, Colonial Pipeline Company

Maelezo ya picha, Bomba la Colonial lilidukuliwa Ijumaa, 07 Mei

"Wanaweza kuhakikisha kuwa mfumo unafanya kazi katika mtando tofauti na sio kuunganisha teknolojia ya taarifa.

"Hata hivyo, uhalisia wa kubadilika kwa dunia una maanisha kuwa mambo mengi yanaweza kwenda vizuri kama yameunganishwa na mtandao."

Wadukuzi ni kina nani?

Shirika la kijasusi la Marekani- FBI limethibitisha kuwa genge la DarkSide limehusika, ni genge jipya la udukuzi mtandaoni na linadhaniwa kuwa lipo Urusi.

Si kawaida kwa kundi la genge la wahalifu kushambulia miundombinu ya taifa - lakini wataalamu kama Andy Norton kutoka yber-defender Armis, anasema suala la kukua.

"Kile tunachokiona sasa ni kukua kwa genge la wizi wa mtandaoni ," amesema.

"Eneo ambalo lina changamoto katika huduma za jamii, ni rahisi kwa wadukuzi kupata mwanya wa kushambulia."

A DarkSide ransomware notice
Maelezo ya picha, Wadukuzi hao waliacha maandishi kama hayo kwenye komputa walizofanya udukuzi

Kinachoshangaza, kundi hilo limetuma ujumbe wa kuomba radhi kwa kudukua tovuti ya darknet.

Ingawa ujumbe huo hauulengi moja kwa moja Colonial, inawekwa kwenye taarifa za leo, amesema: "Lengo letu ni kutengeneza fedha na sio kuleta matatizo kwa jamii.

"Kuanzia leo, tumeanzisha mfumo wa kuangalia kila kampuni ambazo washirika wetu wanataka taarifa ili kuzuia athari za mtandaoni kwa siku zoijazo."

Kama ilivyo kwa makundi mengine ya udukuzi, DarkSide inafanya kazi na programu ambazo zinaruhusu washirika wake kutumia programu za udukuzi ambazo wamezilenga kwa kubadilishana na kiasi cha fedha za kile watakachonufaika nacho.

Awali DarkSide ilisema itaanza kuchangia fedha kwa wahitaji.

Huduma kama hizi zinapaswa kulindwa?

Wataalamu wamekuwa na wasiwasi kwa muda kuhusu athari ya miundombinu ya taifa kudukuliwa.

Mwezi uliopita wataalamu wanasema wanahatarisha usalama wa kitaifa.

Makundi ya serikali yanahitaji kuchukua hatua ya haraka kuzuia wadukuzi kulipwa kwa siri.

Vilevile inataka msukumo kuwekwa kwa nchi kama Urusi , Iran,na Korea Kaskazini ambazo zimekuwa zikishutumiwa mara zote kuhusika na udukuzi.

Lakini bwana Norton amesema shirika hilo linapaswa kuwajibika pia.

"Ni jukumu la kampuni kuhakikisha kuwa kuna usalama wa mtandoani ambao unawezesha kampuni kufanya kazi vizuri na mamlaka zinapaswa kufanya kazi yake kwa ufasaha," amesema.