Idris Deby: Viongozi sita wa nchi za Afrika waliowarithi wazazi wao

Sio kawaida kurithi madaraka au ofisi ya kisiasa kama ilivyo katika tawala za kifalme ulimwenguni.

Sio kawaida kurithi madaraka au ofisi ya kisiasa kama ilivyo katika tawala za kifalme ulimwenguni.

Lakini pia kuna nchi ikiwemo za barani Afrika ambazo zinageuza madaraka ya kisiasa kuwa kitu ambacho hurithiwa kutoka kwa wazazi au babu zao.

Jenerali Mahamat Idriss Déby, mtoto wa aliyekuwa Rais wa Chad Idriss Deby, aliapishwa Jumanne kufuatia kifo cha baba yake kutokana na majeraha aliyoyapata katika mapigano na waasi.

Mbali na Chad, kuna nchi za Kiafrika ambazo zilichukua hatua kama hizo hapo awali kuteua watoto wa marais waliokufa au waliojiuzulu, ingawa hii ni kinyume cha katiba

Hawa hapa baadhi ya viongozi wa Kiafrika ambao walirithi madaraka kutoka kwa wazazi wao:

Joseph Kabila - Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

Joseph Kabila Kabange aliongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Januari 2001 hadi Januari 2019.

Joseph Kabila Kabange aliongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Januari 2001 hadi Januari 2019.

Alianza kazi siku 10 baada ya mauaji ya baba yake, Rais Laurent-Désiré Kabila.

Bwana Joseph Kabila alizaliwa Juni 4, 1971, katika mkoa wa Sud-Kivu, na alikuwa afisa wa jeshi na kuwa mwanasiasa.

Kabila, mwanae kiongozi wa waasi wa Congo Laurent Kabila, alikulia na kusoma nchini Tanzania.

Alikuwa sehemu ya kikundi cha waasi ambacho kilimsaidia baba yake kumtoa Rais Mobutu Sese Seko wa Zaire madarakani mnamo 1997.

Baada ya Laurent kuwa rais alirudisha nchi kwa jina lake la asili, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kutoka hapo Joseph alipelekwa China kwa mafunzo zaidi ya kijeshi.

Aliporudi nyumbani, aliteuliwa Mkuu wa Jeshi na Meja Jenerali.

Faure Gnassingbé - Togo

Rais Faure Essozimna Gnassingbé Eyadéma alizaliwa mnamo Juni 6, 1966, na ni mwanasiasa ambaye amekuwa rais tangu 2005.

Kabla ya kuwa rais wa Togo, baba yake, Rais Gnassingbé Eyadéma, alikuwa amempa wadhifa wa uwaziri kutoka 2003 hadi 2005.

Kabla ya kuwa rais wa Togo, baba yake, Rais Gnassingbé Eyadéma, alikuwa amempa wadhifa wa uwaziri

Kufuatia kifo cha Rais Eyadéma mnamo 2005, Gnassingbé aliteuliwa haraka kuwa rais mpya kutumia usaidizi wa jeshi.

Lakini mashaka juu ya ustahiki wake chini ya katiba ya nchi hiyo yamempa shinikizo kubwa Gnassingbé.

Alishinda pia uchaguzi wa rais uliokuwa na upinzani mkali mnamo Aprili 24, 2005, na aliapishwa kama rais.

Gnassingbé alichaguliwa tena kuwa rais mnamo 2010.

Mahamat Idriss Déby - Chad

Rais mpya wa Chad, Mahamat Idris Deby, ni jenerali wa jeshi aliye chini ya miaka 40, akimrithi babake Rais Idriss Deby Itnu mnamo Aprili 20, 2021.

Jenerali Mahamat Idriss Déby alizaliwa mnamo 1983 ambapo alikua mmoja wa watoto wa marehemu Idriss Deby.

Rais mpya wa Chad, Mahamat Idris Deby, ni jenerali wa jeshi aliye chini ya miaka 40

Anaitwa pia Mahamat Kaka, kwa sababu alilelewa na bibi yake.

Wakati wa kifo cha baba yake, alikuwa mkuu wa walinzi wa rais, kulingana na mwandishi wa BBC huko Chad.

Aliongeza kuwa alikuwa ameshiirki katika mapigano kadhaa ya kijeshi wakati wa kazi yake.

Mnamo 2009, Mahamat Idriss Deby alishiriki katika vita vya Am Dam, ambavyo vilipiganwa pia na binamu yake Timan Erdimialiyemuita mjomba rais Idris Deby mashariki mwa Chad.

Ali Bongo Ondinba - Gabon

El Hadj Omar Bongo Ondimba ni mwanasiasa wa Gabon aliyekuwa rais wa pili wa nchi hiyo kwa miaka 42 kutoka mwaka wa 1967 hadi kifo chake mwaka wa 2009.

Alikuwa rais wa pili wa nchi hiyo kwa miaka 42 kutoka mwaka wa 1967 hadi kifo chake mwaka wa 2009.

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya kifo chake mwanae Ali Bongo Ondimba ambaye wakati mwingine huitwa Ali Bongo alichukua usukani wa nchi hiyo Oktoba mwaka wa 2009. Baba na mwanae wameiongoza Gabon kwa jumla ya miaka 54 sasa .

Presentational white space

Barani Afrika pia bado kuna nchi mbili ambazo zinaongozwa na wafalme ambao ndio wenye mamlaka makuu ya utawala wa Serikali. Nchi hizo ni Morocco na Eswatini. Katika tawala hizo, ni jambo la kawaida na kikatiba kwa watoto wa wafalme kurithi madaraka wanapofariki ama kuondoka madarakani wazazi wao. N a hawa ndio watawala wawili wa nchi hizo ambao waliwarithi baba zao ufalme.

Mfalme Muhammed Bin Sidi Alaouite wa Morocco

Mfalme MuhammEd Bin Sidi Alaouite wa Moroco alizaliwa mnamo Agosti 21, 1963, katika mji mkuu Rabat.

Alichukua usukani mnamo Julai 23, 1999, kufuatia kifo cha baba yake, Mfalme Hassan II.

Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka, Mfalme Mohammed wa Sita aliliambia taifa kwenye runinga kwamba atashughulikia kumaliza umasikini na ufisadi kwa kuunda ajira na kuheshimu haki za binadamu.

Hatahivyo, mabadiliko yake yamewakasirisha wenye msimamo mkali wa Kiisilamu, na ukosoaji mkubwa umetoka kwa Waislamu wahafidhina.

Mnamo Februari 200, alianzisha Sheria mpya ya Familia, ambayo inatoa uhamasishaji wa wanawake.

Mnamo Desemba 2020, Mfalme Mohammed VI alikubali kuimarisha uhusiano na Israeli chini ya makubaliano kwamba Marekani itatambua eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara kama lililo chini ya udhibiti wa Morocco.

Mfalme Mswati III wa Eswatini

Mfalme Mswati III (Makhosetive) alikuwa mtoto wa Mfalme Sobhuza wa Pili ambaye alizaliwa na mmoja wa wake zake Ntfombi Tfwala.

Alizaliwa Aprili 19, 1968 huko Manzini.

Alipewa taji la Prince Mswati III, Ingwenyama, na baadaye akapewa taji la Mfalme wa Swaziland mnamo Aprili 25, 1986 akiwa na umri wa miaka 18, na kumfanya kuwa mfalme mchanga zaidi ulimwenguni wakati huo.

Mfalme Sobhuza II alikufa mnamo Agosti 21, 1982, na Prince Makhosetive alichaguliwa kama mfalme mpya.