Idriss Deby: Wafahamu viongozi wa Afrika waliofariki madarakani

Mazishi ya aliyekuwa rais wa Ghana John Atta Mills

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mazishi ya aliyekuwa rais wa Ghana John Atta Mills aliyefariki mwaka 2012

Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki akiwa angali madarakani. Katika kipindi cha miaka 20 iliopita mkosi huo umeathiri mataifa mengi barani Afrika .

Lakini ni kwa nini vifo kama hivi vinatokea sana barani Afrika?

Idriss Deby

Tangazo la kifo cha Rais Idriss Deby limetolewa leo na jeshi la Chad ikiwa ni saa chache tu tangu madokeo ya awali ya urais ya uchaguzi wa Aprili 11 kutangazwa.

Dby alikuwa tayari anaongoza kwa asilimi 80 ya kura, na alitazamiwa kuongoz nchi hiyo kwa muhula wake wa sita.

Tofauti na marais wengi, Deby hajafa kwa ugonjwa, amekufa uwanja wa vita akiwa na wanajeshi wake.

Alikwenda mstari wa mbele mwishoni mwa juma lililopita kuwajulia hali wapiganaji wake ambao walikuwa wakikabiliana na waasi ambao walivuka mpaka kutoka kwenye kambi ya nchini Libya. Deby alikuwa na kawaida ya kuongoza mapambano ya kijeshi akiwa mstari wa mbele.

John Pombe Magufuli

John Pombe Magufuli
Maelezo ya picha, John Pombe Magufuli

Kiongozi huyo wa Tanzania aliaga dunia tarehe 17 mwezi Machi 2021, miezi michache tu baada ya kuchaguliwa kwa awamu ya pili.

Kwa mujibu wa tangazo rasmi la serikali kiongozi huyo alifariki kutokana na mshtuko wa moyo baada ya kuugua tatizo hilo kwa zaidi ya miaka 10.

Kabla ya kifo chake, kiongozi huyo alitoweka hadharani kwa zaidi ya wiki mbili na kuzua uvumi kuhusu hali yake ya kiafya.

Aliyekuwa Makamu wake Bi Samia Suluhu Hassan ndiye aliyerithi madaraka ya urais wa nchi hiyo.

Rais Pierre Nkurunziza

Aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Maelezo ya picha, Aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Rais Nkurunziza alifariki akiwa na umri wa miaka 55. Kulingana na Balozi Willy Nyamitwe , Nkurunziza alifariki kutokana na mshtuko wa Moyo , kinyume na uvumi uliokuwa ukienea .

Kulingana na ujumbe uliochapishwa katika Tmtandao wa Twitter Agosti 8 mwaka uliopita "Timu ya madaktari walishindwa kunusuru maisha yake baada ya kupata mshutuko wa moyo."

Rais Bingu wa Mutharika

Bingu wa Mutharika
Maelezo ya picha, Bingu wa Mutharika

Miezi minne kabla ya kifo cha Atta Mills, siku ya kitaifa ilitangazwa nchini Malawi kuwezesha maelfu ya watu kuhudhuria mazishi ya hayati rais Bingu wa Mutharika, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 78 kutokana na mshtuko wa moyo.

Mutharika wa Malawi alifariki dunia mwaka 2021 lakini ukosefu wa habari rasmi ulisababisha hali ya wasiwasi na uvumi nchini.

Maelezo ya video, Kifo cha rais John Pombe Magufuli: Tanzia ya rais wa awamu ya tano Tanzania

Kulingana na katiba , makamu wa rais anachukua uongozi iwapo kiongozi wa taifa amefariki akiwa ofisini.

Lakini makamu wa rais Joyce Banda na Mutharika walizozana kufuatia mzozo wa kumrithi Mutharika 2010 ambapo alipigwa marufuku katika chama tawala cha Democratic party. (DPP).

Na mnamo mwezi Januari, rais wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha, alifariki katika hospitali ya kijeshi mjini paris baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 64.

Meles Zenawi wa Ethiopia

Meles Zenawi

Chanzo cha picha, BMell

Maelezo ya picha, Meles Zenawi

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi alifariki akiwa na umri wa miaka 57 hospitalini ngambo, kulingana na serikali.

Serikali ya Ethiopia hatahivyo haikutoa maelezo lakini msemaji wa Muungano wa Ulaya baadaye aliambia waandishi kwamba Bwana Meles Zenawi alifariki mjini Brussels Ubelgiji.

Bwana Meles alikuwa hajaonekana hadharani kwa wiki kadhaa na kulikuwa na uvumi kuhusu afya yake wakati aliposhindwa kuhudhuria mkutano mjini Addis Ababa mwezi uliopita.

Makamu wake Hailemariam Desalegn alichukua uongozi hadi uchaguzi uliopoitishwa 2015.

Muammar Gaddafi

Muamar Gaddafi
Maelezo ya picha, Muamar Gaddafi

Kiongozi wa zamani nchini Libya kanali Muammar Gaddafi aliuawa baada ya uvamizi katika Kijiji chake cha Sirte , maafisa wanasema.kaimu waziri mkuu Mahmoud Jibril alitangaza kifo chake na baadaye kusema kwamba kanali huyo aliuawa katika ufyatulianaji wa risasi kati ya wanajeshi wake na wapiganaji kutoka kwa mamlaka ya mpito.

Kanali Gaddafi aliondolewa mamlakani mwezi Agosti baada ya miaka 42 mamlakani.Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki akiwa angali madarakani.

Viongozi waliofariki madarakani Afrika