'Ni Unafiki' : Elton John alishutumu kanisa Katoliki kwa kukataa kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja

Chanzo cha picha, Reuters
Mwanamuziki nguli wa Uingereza Elton John ameshutumu makoa makuu ya kanisa katoliki kwa ''unafiki''.
Matamshi yake yanajiri baada ya the Vatican kutoa taarifa ya kukumbusha walimwengu kwamba kanisa katoliki haliwezi kubariki `ndoa za wapenzi wa jinsia moja'.
Mkutano wa mafundisho katika kanisa hilo kwa jina maarufu CDF ulidai kwamba makuhani hawawezi kwa njia yoyote kutoa baraka kama hizo kwasababu ''Mungu hawezi kubariki dhambi''.
Taarifa hiyo iliidhinishwa na papa Francis , ambaye awali ametoa ishara ya kutokubaliana na wale walio na msimamo mkali katika kanisa hilo kuhusu suala la wapenzi wa jinsia moja.
''Wana haki kuwa katika familia'': Papa Francis alisema akiwaunga mkono wapenzi wa jinsia moja.
Wanachama wengi wa Muungano wa wapenzi wa jinsia moja duniani LGBT walikasirishwa na msimamo huo akiwemo Elton John.
Je alisema nini haswa?
Mwanamuziki huyo wa Uingereza alichapisha katika mtandao wake wa twitter:
"Inakuwaje Vatican haiwezi kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja kwasababu ni dhambi na badala yake baadaye wajipatie faida kupitia uwekezaji wa mamilioni ya madola katika Rocketman, filamu inayosherehekea ndoa yangu kwa David???''.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mwisho wa chapisho hilo la Twitter , msanii huyo aliweka alama ya reli: "Unafiki."
Filamu ya The Rocketman ni kuhusu Maisha ya Elton John. Anaelezea jinsi alivyopanda na kuwa nyota katika muziki huku akizungumzia kuhusu jinsia yake na mahusiano yake na waume wengine.
Filamu hiyo ilielezewa kuwa ya kwanza kumuonesha mwanamume mpenzi wa jinsia moja.
Kwanini taasisi ambayo inawachukulia wapeini wa jinsia moja kuwa wenye dhambi kujitolea kuwekeza katika filamu kama hiyo?
Utafiti
Wawakilishi wa nyota huyo wa Uingereza hawakujibu maswali kutoka kwa BBC , lakini msemaji aliambia Newsweek siku ya Jumatatu kwamba uwekezaji wa Vatican umeripotiwa katika vyombo vikuu vya habari ikiwemo gazeti la Financial Times. Mbali na hilo, hatutatoa tamko lolote Zaidi, alisema.
Habari kuhusu uwekezaji huo zinashirikisha uchunguzi wa 2019 uliofanywa na gazeti la Italia la Corriere Della Sera, mojawapo ya magazeti yanayosomwa sana nchni humo.
Gazeti hilo liliripoti kugundua habari kuhusu uwekezaji uliofanywa na hazina moja ya fedha ambazo zilitolewa na katibu wa Vatican.

Chanzo cha picha, PARAMOUN PICTURES
Wizara hiyo ya katibu wa masuala ya kigeni ni mojawapo ya wizara zenye nguvu Vatican. Kwa karne kadhaa, ameweza kusimamia kila kitu
Kutoka usimamizi wa kanisa hilo hadi masuala yake ya kidiploamasia ya kanisa hilo.
Katika uchunguzi wake , gazeti hilo la Italia lilisema kwamba ''Zaidi ya $ 4.7 million zimetengwa kufadhili uzalishaji wa filamu kama vile Men in Black mpya na filamu ya Maisha ya Elton John Rocketman."
Chombo hicho kilisema kwamba Yuro milioni moja ya kitita hicho ziliwekezwa katika failamu hiyo mpya.
Haijulikani Vatican ina ukaribu wa kiasi gani katika kufuatilia uwekezaji huo.
Kiasi cha ufadhili huo uliohojiwa, unatoka kwa Peter Pence , kitengo kinachokusanya michango ambayo hutolewa na wafuasi wa kanisa hilo kulingana na gazeti hilo la Italia.

Chanzo cha picha, Reuters
Matumizi ya fedha hizo za Peter Pence yanachunguzwa kufuatia uchunguzi wa Vatican kuhusu uwekezaji wa kujenga na kununua nyumba za kuuza mjini London 2019.
Mwaka 2020, gazeti la The financial Times lilichapisha kwamba lilifanikiwa kupata stakhabadhi zinazoonesha kwamba Vatican ilichangia katika ufadhili wa filamu ya Rocketman .
Muda mfupi baada ya habari hiyo papa Francis aliagiza mabadiliko katika masuala ya kifedha ya Vatican, na kuondoa usimamizi wa fedha za kanisa hilo kutoka wizara ya masuala ya kigeni.
Je Vatican ilisemaje?
The Vatican haijathibitisha hadharani kuhusu habari za uwekezaji katika filamu ya Rocketman.
BBC iliomba tamko kutoka kwa Vatican lakini haijapata jibu lolote kufikia wakati wa kuchapishwa kwa habari hii.
Kutokana na hilo , haijulikani ni kiwango gani papa Francis anajua kuhusu masuala ya kifedha ya Vatican.
" Rocketman ni filamu kuhusu mpenzi wa jinsia moja ambaye amekuwa na wakati mgumu kukubai hali yake , anaambia BBC.












