Kanisa katoliki haliwezi kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja

Chanzo cha picha, Getty Images
Kanisa katoliki halina uwezo wa kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja, Ofisi ya mafundisho mjini Vatican amesema.
Haiwezekani kwa Mungu kubariki dhambi, ofisi inayotoa mafundisho imesema siku ya Jumatatu.
Hatahivyo ofisi ya mkutano huo inatambua kwamba kuna mambo mazuri katika mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja.
Mwezi Oktoba, Papa Francis alisema katika makala moja kwamba alifikiria kwamba ndoa za wapenzi wa jinsia moja zinapaswa kuhalalishwa.
Papa Francis anaonesha kuunga mkono vyama vya wapenzi wa jinsia moja, Katika Kanisa Katoliki, baraka hutolewa na kuhani au mhudumu mwingine kwa jina la Kanisa.
Mwaka 2013 papa Francis alivunja mafundisho akisema kwamba '' Mimi ni nani kuwahukumu wapenzi wa jinsia''?

Chanzo cha picha, Getty Images
Siku ya Jumatatu papa Francis aliidhinisha jibu la mkutano wa mafundisho, akisema kwamba sio njia ya kuwabagua, badala yake ni ukweli.
"Baadhi ya parokia katika miezi ya hivi karibuni, ikiwemo Ujerumani na Marekani zimeanza kuwabariki wapenzi wa jinsia moja kama njia ya kuwakaribisha wakatoliki wapenzi wa jinsia moja katika kanisa hilo, Kitengi cha habri cha reuters .
Jibu hilo la CDF lilitokana na jibu kutoka kwa swali lililoulizwa.
Je kanisa hilo lina uwezo kutoa baraka kwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja? Lilijibu hapana.
Mkutano wa mafundisho hayo ulisema kwamba ndoa kati ya wanaume na wanawake ni sakramenti na hivyo basi baraka haziwezi kupewa kwa wapenzi wa jinsia.
Kwasababu hiyo, sio makosa kutoa baraka kuhusu mahusiano, au ushirikiano hata yalio thabiti ambayo uhusisha vitendo vinavyohusisha tendo la ndoa nje ya ndoa.












