Virusi vya corona: Kwanini chanjo ya AstraZeneca inakataliwa na nchi mbalimbali?

Uholanzi imekuwa nchi ya hivi punde barani ulaya kusitisha matumizi ya chanjo ya corona ya Oxford-AstraZeneca kwa madai kwamba ina madhara .
Hatua hiyo sasa imezidisha idadi ya nchi ambazo zimesitisha matumizi ya chanjo hiyo kutokana na hofu ya usalama wake.
Uholanzi imesema hatua hiyo imechukuliwa hadi Machi 29 ili kuweka tahadhari zinazohitajika kabla ya kurejelea matumizi yake.
Taifa hilo sio pekee ambalo limetilia shaka usalama wa chanjo hiyo ya Oxford-AstraZeneca kwani nchi nyingine zilizofanya uamuzi huo ni pamoja na Denmark, Norway, Bulgaria, Iceland na Thailand.
Awali Jamuhuri ya Ireland ilichukua uamuzi huo huo kwa kuhofia hatari ya watu kuganda damu baada ya kupata chanjo hiyo nchini Norway.
Lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna uhusiano wowote baina ya chanjo hiyo na hatari ya watu kuganda damu.
Shirika la dawa la Muungano wa Ulaya(EMA) lilisema awali kwamba hakuna dalili kwamba chanjo hiyo inasababisha kuganda kwa damu mwilini, likiongeza kuwa ni "faida ambayo zinaendelea kuwa kubwa kuliko hatari zake.
Je, chanzo cha hatua hiyo ni nini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Sababu kuu iliyotolewa na nchi ambazo zimesitisha kuitumia chanjo hiyo ni kwamba ilisababisha watu kuganda damu mwilini.
Ufichuzi huo umezua hofu miongoni mwa nchi nyingi zilizokuwa zimepewa chanjo ya AstraZeneca ambazo sasa zinasitisha kuitoa kwa wananchi hadi usalama wake uthibitishwe .
Licha ya shirika la Afya Duniani WHO kujitokeza na kusema kwamba chanjo hiyo ni salama ,hakikisho hilo limeonekana kutoziridhisha nchi nyingi zinazoamua kungoja kwa muda kabla ya kurejelea matumizi yake .
AstraZeneca inasemaje?

Kupitia taairifa ,AstraZeneca imesema hakuna ushahidi kwamba kuna ongezeko la kuganda damu miongoni mwa watu waliochanjwa.
Imesema kwamba kote barani Ulaya na Uingereza kumekuwa na visa 15 vya watu kuganda damu katika mishipa yao na visa 22 vya watu waliogandiwa damu katika mapafu wote ambao walipewa chanjo hiyo.
Afrika inasemeja kuhusu chanjo ya AstraZeneca?

Afrika Kusini ilikuwa miongoni mwa mataifa ya kwanza barani Afrika kukoamesha matumizi ya chanjo ya Oxford-AstraZeneca baada yamajaribio ya kwanza kutoa 'matokeo ya kufdhaisha' dhdi ya ya virusi vya Corona aina ya B.1.351.
Nchi hiyo ilipokea dozi milioni moja za chanjo hiyo .Ilikuwa imepanga kuanza kuwachanja wahudumu wa afya kuanzia katikati ya mwezi Februari . Majaribio yaliofanyiwa watu 2000 yalipatakwamba chanjo hiyo ilitoa 'kinga adimu' dhidi ya Coviid 19 yenye makali ya wastani.
Serikali ya nchi hiyo badala yake iliamua kutumia chanjo ya Johnson & Johnson na Pfizer.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nayo pia imeahirisha kampeni ya kutoa chanjo hiyo ya corona iliyokua ianze leo Jumatatu kwa hofu ya usalama wake.
Taifa hilo limepokea dozi milioni moja na laki saba ya chanjo hiyo aina ya AstraZeneca na ilikuwa inatarajiwa kuanza zoezi la kuchanja watu leo.
DRC inataka hakikisho la kuaminika kwanza kuhusu usalama wa chanjo hiyo.
Nchini Uganda ,Rais Yoweri Museveni amesema bado anatathmini ni chanjo ipi atakayochomwa, siku chache baada serikali yake kuanza kutoa chanjo ya Oxford-AstraZeneca kwa wananchi.
Tayari marais wengine barani Afrika wameonesha kwa umma wakipewa chanjo ili kuwahakikishia wananchi wao usalama na ufanisi wa chanjo hiyo .
Katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo, Rais Museveni amesema hajapata chanjo bado kwa kuwa yuko makini na ana ulinzi wa kutosha ".
Alisema mke wake, Janet Museveni,pia bado hajapata chanjo hiyo.
Mwezi uliopita Waziri wa afya wa nchini humo Jane Aceng , alikanusha taarifa kuwa rais na watu wake wa karibu walikuwa wanapokea chanjo nyingine kwa siri kabla ya taifa hilo kupokea chanjo rasmi.
Alitoa ufafanuzi baada ya gazeti la nchini humo la Daily Monitor na gazeti la Marekani la jarida la Wall Street.
Uganda ina mpango wa kutoa chanjo kwa 49.6% ya idadi ya watu katika awamu ya kwanza.
Nchi hiyo imepokea dozi 864,000 za chanjo kutoka Covax mapema mwezi huu na inatarajia kupokea nyingine 2,688,000 mwishoni mwa mwezi Juni.














