Virusi vya corona: Thailand na mataifa matatu ya Ulaya yasitisha utoaji wa chanjo ya AstraZeneca kwa hofu ya kusababisha kuganda kwa damu

A medical worker fills a syringe from a vial of the British-Swedish AstraZeneca/Oxford vaccine

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chanjo ya AstraZeneca/Oxford

Thailand imesitisha utoaji wa chanjo ya virusi vya corona ya AstraZenica kufuatia ripoti za kuhganda kwa damu, licha ya kuwa hakuna ushahidi juu ya hilo

Waziri Mkuu wa Thailand alikuwa anatarajia kuanzisha kampeni ya utoaji wa chanjo siku ya Ijumaa.

Kampeni hiyo sasa imesitisha.

Hatua hii inakuja baada ya mataifa mengine matatu ya Ulaya- Norway, Denmark na Austria kutangaza kuzuia matumizi ya chanjo za tofauti za Covid-19 ikiwemo ile Oxford na AstraZenica wakitoa madai hayo.

Takribani rais wa milioni 5 wa Ulaya stayari wamekwishapata chanjo ya AstraZeneca.

Wizara ya afya ya umma ya Thailand imesema kuwa imechukua uamuzi huo kwasababu nchi hiyo bado ''haijaaathiriwa vibaya " na virusi na ina chanjo nyingine inazoweza kutegemea kwa sasa.

Kumekuwa na visa takriban 30 barani Ulaya vya watu kukpata kile kinachoitwa kitaalamu "thromboembolic " - au kupata mgando wa damu-baada ya kupata chanjo ya virusi vya corona.

Shirika la madawa la Muungano wa Ulaya(EMA) lilisema Alhamisi kwamba hakuna dalili kwamba chanjo hiyo inasababisha kugada kwa damu mwilini, likiongeza kuwa ni "faida ambayo zinaendelea kuwa kubwa kuliko hatari ".zake

AstraZeneca ilisema kuwa usalama wa dawa umefanyiwa utafiti mkubwa katika majaribio ya tiba, ikiwa ni pamoja na katika maabara za Ureno, Australia, Mexico na Ufilipino ,wamesema kuwa wanaendelea na mpango wa utoaji wa chanjo.

Thailand imesema nini?

"Ingawa thamani ya AstraZeneca ni nzuri, baadhi ya nchi zimeomba kuchelewa kuitumia ," Piyasakol Sakolsatayadorn, mshauri wa kamati ya taifa ya chanjo ya Covid-19 , aliwambia waandishi wa habari

"Tutachelewa pia]."

Hatahivyo, maafisa wa Wizara ya afya wamefafanua kuwa aina ya chanjo ya AstraZeneca waliyoipata ni tofauti na zile zinazosambazwa barani Ulaya, na kuongeza kuwa matatizo ya kuganda kwa damu hayajabainika sana miongoni mwa Waasia.

Shehena ya kwanza ya dozi 117,300 za AstraZeneca iliwasili Thailand tarehe 24 Februari, pamoja na dozi 200,000 za chanjo ya uchina ya Coronavac.

Zaidi ya watu 30,000 nchini Thailand tayuari wamepokea chanjo ya Coronavac tangu nchi hiyo ilipoanza mpango wake wa kutoa chanjo tarehe 28 Februari.

Thailand inasema itaendelea na mpango wake wa kutoa chanjo ya Coronavac iliyotengenezwa na China.

Nurses with the AstraZeneca vaccine

Chanzo cha picha, EPA

Nchi zinafanya nini?

Nchini Uingereza Shirika la udhibiti wa bidhaa za huduma za afya(MHRA) lilisema kuwa hapakuwa na ushahizi kwamba chanjo hiyo ilisababisha matatizo, na watu wananapaswa kuendelea kuchanjwa wakati wanapoobwa kufanya hivyo.

Zaidi ya dozi milioni 11 za chanjo ya AstraZeneca zimekwishatolewa kote Uingereza, kwa mujibu wa MHRA.

Ureno imesema kuwa faida za chanjo zinaendelea kuwa kubwa kuliko hatari zake kwa wagonjwa, na itaendelea kuitumia chanjo hiyo.

Imesema haijapata uhusiano wowite wa chanjo nan a kuganda kwa damu.

Australia, ambayo tayari imekwishatuma dozi 300,000 za chanjo ya AstraZeneca , imekuwa ikielezea uamuzi wake wa kuendelea kutumia chanjo ya AstraZeneca.

"Kwa sasa ushauri ambao ni wa wazi kutoka kwa madaktari ni kwamba hii ni chanjo salama na tunataka chanjo iendelee kutolewa.

Wizara ya afya ya Ufilipino pia imesema kuwa '' hakuna sababu'' ya kuzuia chanjo huko.

Korea Kusini pia inaonekana kuendelea na mpango wake wa utoaji wa chanjo hiyo, ingawa imeelezea hofu yake.

Takriban dozi 785,000 zimewasili nchini humo tayari.

Mamlaka nchini humo hivi karibuni zilisema kuwa vifo vinane vilivyotokea katika kipindi cha kupokea chanjo havikuhusina na chanjo.

Baadaye walibaini kuwa hapakuwa na uhusiano baina ya chanjo na vifo hivyo.

Hatahivyo , Denmark, Norway pamoja na Iceland zimesitisha kwa muda mpango wake wa utoaji wa chanjo.

Italia na Austria, wakati huo huo, zimeacha kutumia aina fulani ya chanjo hiyo kama hatua yake ya kuchukua tahadhari.

Katika taarifa ya awali, EMA ilisema kuwa uamuzi wa Denmark ulikuwa ni "hatua ya kuchukua tahadhari huku uchunguzi kamili ukiendelea kuhusu ripoti za ugandaji wa damu miongoni mwa watu waliopokea chanjo, likiwemo tukio moja nchini Denmark ambako mtu mmoja aliuawa ".

Chanjo inafanya kazi vipi ?

Chanjo ya AstraZeneca , ambayo ilitengenezwa na Chuo Kikuu Oxford,imetengenezwa kutokana na virusi vinavyosababisha na mafua ya kawaida vilivyodhoofishwa (vinavyofahamika kama adenovirus) kutoka kwa sokwe .

Virusi hivi vimebadilishwa umbo ili kuonekana zaidi kama virusi vya corona-inagawa haviwezi kusababisha ugonjwa.

Unapochomwa chanjo hii, inaufundisha mfumo wa kinga ya mwili jinsi ya kupambana na virusi halisi, pale utakapohitaji kufanya hivyo.