Mgahawa wa chai wa China waomba msamaha kwa kuwaita wanawake bidhaa ya 'kujadiliana' bei

File photo of a woman drinking bubble tea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mgahawa maarufu wa kamouni ya China uliwaelezea wanawake kama bidhaa ya 'kujadiliwa' bei

Mgahawa maarufu wa Kichina umeomba msamaha kwa kutumia nembo iliyoonekana kuwadhalilisha wanawake katika badhaa yake, baada ya maandishi hayo kuibua hisia kali kwenye mtandao.

Mgahawa huo unaoitwa Sexy Tea shop uliwaelezea wanawake kama bidhaa ya "kujadiliana" bei katika moja ya vikombe vyake, na kuongeza kuwa wateja wanaweza kumchukua mwanamke huku wakisubiri kupewa vivywaji.

Awali mgahawa huo pia uliuza pakiti za chai yenye nembo "Lazima nikuchague wewe, ninakutaka wewe'' ambayo pia ilikuwa na picha ya vijusi cha chura.

Baadae mgahawa huo ulisema kuwahaukuwa na nia ya "kuwadharau wanawake".

Uliongeza kuwa itaacha kutumia vikombe vyake na kuongeza kuwa "umeaibika sana" na kutengeneza vikombe hivyo.

Mgahawa huo hivi karibuni uliweka maneno yaliyoandikwa kwa lafudhi ya "Changsha kwenye vikombe vyake " - , inayozungumzewa zaidi katika mji mkuu wa jimbo la Hunan. Kampuni inayomiliki mgahawa huo ina migahawa ya aina hiyo 270 huko.

Ilichapisha maandishi kadhaa ya lugha hiyo isiyo rasmi kwenye vikombe, ikiwa ni pamoja na maneno "jian lou zi", yanayomaanisha chukua mali kwa bei rahisi.

Pia ulitoa mfano wa jinsi sentensi inavyoweza kutumiwa , katika sentensi "Ninapotaka kununua chai yenye povu, kuna wasichana wengi warembo pale. Kama ukikutana na mmoja kama huyu, unaweza kumwambia rafiki yako - Nilimchukua kwa majadiliano".

Picha ya kikombe cha mgahawa huo ilisambazwa sana kwenye mtandao wa kijamii ya Uchina Weibo na mara ujumbe huo ukaibua ukosoaji mkubwa kuhusu maandishi yaliyoandikwa kwenye kikombe cha mgahawa huo.

"Hii ni aina ya uuzaji wa bidhaa inayotumiwa matusi ," mtu mmoja alisema kwenye mtandao huo.

"Maandishi yenyewe hayana matusi-ni mfano uliotolewa na kampuni ndio wenye matusi ," mwingine aliongeza. "Kwani hakuna yeyote katika timu ya masoko aliyeona kuwa kuna kosa katika hili ?"

Sexy Tea

Chanzo cha picha, Sexy Tea/Website

Maelezo ya picha, Kampuni hii ni maarufu sana nchini Uchina

Baadae kampuni inayomiliki mgahawa ilitoa taarifa ndefu ikiomba radhi kwa jinsi ilivyotoa ufafanuzi wa maandishi yake.

" Tulitengeneza sentensi ambayo ilikuwa haifai kabisaambayo hata wajtu katika Changsha hawakuipenda.... tumeaibika sana. Hatukuwa kabisa na nia ya kuwavunjia heshima wanawake ," ilisema.

"Tumeondoa mara moja wenye migahawa yetu vikombe vilivyokuiwa na maandishi ya lugha ya Changsha na tunatathmini sana tukio hili."

Watumiaji wa mtandao pia wanasema kuwa sio mara ya kwanza kwa mgahawa huu unaojiita Sexy Tea kutumia maneno kingono katika kunadi bidhaa zake.

Wengi wamezungumzia kuhusu picha za vijusi vya chura ambavyo imevichapisha kwenye vikombe vyake, ambavyo wamesema vilimaanisha mbegu za kiume.

Unaweza pia kusoma?