Mzozo wa siasa DRC: Wabunge kumuondoa madarakani Spika wa bunge

Spika Jeanine Mabunda anatoka chama cha rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila

Chanzo cha picha, Mbelechi Msochi

Maelezo ya picha, Spika Jeanine Mabunda anatoka chama cha rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila

Spika wa bunge la DRC Jeanine Mabunda ameondolewa katika nafasi yake baada ya wabunge kupiga kura ya maoni dhidi yake iliyowasilishwa bungeni na Upinzani.

Miongini mwa wabunge 484 katika Bunge hilo kura 281 zilisema kwamba kiongozi huyo wa muhimili huyo aondoke katika nafasi yake.

Zaidi ya wanabunge mia mbili kati ya wabunge mia tano waalifanya kikoa cha kupiga kura ya kumuondoa madarakani Spika wa bunge Jeanine Mabunda kutoka chama cha Joseph kabila.

Mwandishi wa BBC, nchini DRC anasema ; Upande wa chama cha Kabila tayari kulikuwa na mzozo katika vyama vilivyokuwa vinamuunga mkono, hivyo hiyo inaweza kuwa sababu ya kuanguka kwao.

Na hatua inayofuata ni waziri mkuu kujiuzulu sasa kwasababu rais atamchagua mtu atakayeunganisha vyama bungeni hivyo nia ya rais kuvunja muungano huo.

Lakini kinachoshangaza inakuwaje spika huyo ashindwe kupata kura za kutosha kumtetea kupata kura za kutosha wakati wabunge wa chama chake ni wengi zaidi.

Kwanini hasa kimesababisha chama cha Rais wa zamani chenye idadi kubwa ya wabunge Bungeni kushindwa kumuunga Mkono Spika huyo wa Bunge?

Tuhuma zimemwendea rais wa zamani Joseph Kabila kwa kumchagua mtu dhaifu ambaye hajawahi kuwa kiongozi au kusimamia watu wowote.

Hata kutoka kwa wafuasi wake Kabila wanaona kuwa nafasi ile ilihitaji mtu ambaye ana uzoefu wa kisiasa, tofauti na spika aliyeondolewa.

Huku wabunge wa upande wa rais aliyeko madarakani Felix Tschisekedi wanamtuhumu kwa uongozi mbaya.

Kwa mujibu wa mbunge Moindo Nzangu , ambaye aliwasilisha mapendekezo ya kura hiyo mwanzilishi Spika Bi Jeanine Mabunda atatakiwa kujitetea mbele ya wabunge kabla ya kumpigia kura ya kutokuwa na Imani naye.

Bunge

Chanzo cha picha, Mbelechi Msochi

Vurugu na ghasia zilitokea ndani ya bunge hilo wiki hii wakati ulipowasilishwa muswada wa kura ya maoni na watu kadhaa walijeruhiwa wakati wanaharakati na wabunge walipoanza kurushiana viti na kuharibu samani ndani ya bunge.

Mzozo wa hivi karibuni wa kisisia nchini Congo umeibuka tena baada ya rais Félix tshikedi kutangaza nia yake ya kuvunja bunge ili apate wingi wa wabunge ambalo kwa sasa lina idadi kubwa zaidi ya wabunge kutoka chama cha mtangulizi wake rais mstaafu Joseph Kabila.

Félix Tshisekedi
Maelezo ya picha, Mzozo wa kisiasa uliibuka baada ya Félix Tshisekedi kutangaza mpango wa kuvunja serikali ya muungano na wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila.

Jumapili Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, alitangaza kuweka mpango wa kuvunja serikali ya muungano na wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila.

Alisema alipata ushauri wa wiki tatu kabla ya kutoa tangazo hilo la kusitisha serikali ya muungano.

Bwana Tshisekedi anasema ameshindwa kutekeleza matakwa ya Wakongo kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na changamoto hiyo.

Rais mstaafu Joseph Kabila bado ana ushawishi mkubwa ndani ya siasa za DRC

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais mstaafu Joseph Kabila bado ana ushawishi mkubwa ndani ya siasa za DRC

Jambo muhimu ambalo ameliamua Rais Tschisekedi ni kuchagua maofisa wapya kuunda baraza jipya kwani bunge la sasa lina wafuasi wengi wa Kabila ambao hawamsikilizi.

Alisema alikuwa amejiandaa kuvunja bunge lote kama kuna ulazima.

"Ni wakati muafaka wa kuzingatia maadili, kanuni na mfumo wa mipango iliyopo.

Hivyo ni muhimu kufanya mageuzi yakinifu na sahihi katika bunge lililopo sasa ni muhimu'', alisema Bw Tschisekedi..

Alimteua 'mtoa taarifa' ,kwa mujibu wa katiba kifungu namba 78, aya ya pili.

Mtoa taarifa huyo atawajibika kuainisha watu watakaokuepo kwenye serikali mpya ya muungano, ambayo itakuwa na wajumbe wengi ambao ni wafuasi wa chama kilichopo madarakani tofauti na awali.

Kabila na Tschisekedi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Huenda isiwe rahisi kwa Tschisekedi kufanya mageuzi ya kisiasa kutokana na ushawishi wa kisiasa wa mtangulizi wake Joseph Kabila

Utakuwa muungano mpya ambao serikali utauweka na kufanya kazi kwa miaka iliyosalia ya uongozi wangu, alisema alisema na kuongeza kuwa :''Kwa mujibu wa maono yangu, ili kufanikisha kukidhi matakwa ya watu mabadiliko hayo yanapaswa kufanyika.Kwa maana nyingine , sababu ya kusitisha muungano huu ni kukabiliana na mvutano uliopo ambao unaweka kizuizi katika jitihada za serikali.''

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Congo wanasema, huenda isiwe rahisi kwa Bwana Tschisekedi kufanya mageuzi ya kiuongozi ikizingatiwa kuwa kuwepo kwake madarakani kuna mkono wa mtangulizi wake Joseph Kabila ambaye bado ana ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo.

Unaweza pia kusoma :