Qasem Soleimani: Marekani imemuua mkuu wa Iran wa vikosi vya Qudsi, Pentagon yathibitisha

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Qasem Soleimani, Jenerali wa vikosi vya Qudsi vinavyoungwa mkono na Iran, ameuawa na vikosi vya Marekani nchini Iraq.
Pentagon imethibitisha kuwa aliuawa kufuatia "amri ya rais".
Hayo yamejiri kufuatia ripoti ya mashambulio katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Baghdad, ambayo ilisema watu kadhaa wameuawa.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, ametaja hatua hiyo kuwa "hatari na uchokozi".
Gen. Soleimani alikuwa mtu mashuhuri kwa utawala wa Iran. Kikosi chake cha Quds kilikuwa kinaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na alisifiwa kama shujaa wa kitaifa.

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter picha ya bendera ya Marekani baada ya kutangazwa kuuawa kwa jenerali hiyo.
Bei ya mafuta duniani imepanda kwa asilimia nne baada ya shambulio hilo.
Nini kilichofanyika?
"Kufuatia agizo la rais, jeshi la Marekani ilichukua hatua ya kuwalinda wafanyikazi wake nje ya nchi kwa kumuua Qasem Soleimani," taarifa ya Pentagon ilisema.
"Hatua hii ililenga kudhibiti mipango ya Iran ya mashabulio ya siku zijazo. Marekani itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuwalinda watu wetu na maslahi yetu kote duniani."
Shambuio hili linakuja baada ya siku kadhaa za maandamano ambapo waandamaanaji waliokuwa wakishambulia ubalozi wa Marekani mjini Baghdad kukabiliana na vikosi vya Marekani katika eneo hilo.
Pentagon inasema jenerali Soleimani aliidhinisha mashambulio dhidi ya ubalizi.
Kikosi maalum cha jeshi la Iran kimesema kiongozi wa waasi wa Iraq Abu Mahdi al-Muhandis pia ameuawa katika shambulio hilo lililotekelezwa na Marekani, na kulaumu mashambulio ya helikopta kutoka kwa nchi hiyo.
Ripoti zinaashiria kuwa viongizi kadhaa wa waasi wa Iraq wanazuiliwa na vikosi vya Marekani mjini Baghdad, japo tarifa hizo hazijathibitishwa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Qasem Soleimani ni nani?
Tangu mwaka 1998, Meja Jenerali Qasem Soleimani ameongoza vikosi vya kikurdi nchini Iran- kengo maalum cha jeshi la Iran (Revolutionary Guards) ambacho huendesha opareshani zake nje ya nchi.
Alikuwa kiungo muhimu katika mapambano ya kimkakati mashariki ya kati kupitia vikosi vya Kikurdi, ambavyo vinaendesha oparesheni yake kwa ushirikiano na jeshi la ulinzi la Iran.
Jina lake lilianza kuwa maarufu alipopewa nafasi ya kuongoza kikosi cha Quds na kujenga ushirikiano wa karibu na kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Khamenei kiasi wakati mmoja ulamaa huyo alishiriki na kufungua dhifa ya harusi ya binti ya Jenerali Soleimani.
Meja jenerali Qasem Soleimani, na vikosi vyake vinafanya kazi chini ya kiongozi mkuu wa kidini, Ayatollah Ali Khamanei, badala ya kufuata muundo wa kawaida wa kijeshi wa Iran.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitaja jeshi la ulinzi la Iran Revolutionary Guards na washirika wake vikosi vua Kikurdi kama shirika la kigeni la ugaidi mwezi April mwaka jana.
Jenerali Qasem Soleimani hakuwa anajulikana na wengi nchini Iran hadi mwaka 2003 wakati Marekani ilipoivamia kijeshi Iraq.
Umashuhuri wake uliimarika hatua ambayo ilifanya maafisa kadhaa wa Marekani kutoa wito wa kuuliwa kwake.
Muongo mmoja na nusu baadae Soleimani alifikia kuwa kamanda maarufu wa vita nchini Iran kiasi akipuuza miito ya umma kumtaka aingie kwenye siasa.















