Qasem Soleimani: Jenerali wa kikosi maalum cha Iran aliyeuawa na Marekani

Qassem Soleimani

Chanzo cha picha, Getty Images

Qasem Soleimani anasadikiwa kuwa mtu wa pili maarufu katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran baada ya kiongozi wa kidini Ayatollah Ali Khamanei.

Kama kiongozi wa kikosi maalum cha jeshi la ulinzi wa Iran nje ya nchi kinachofahamika kama Quds, Soleimani alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zote za kijeshi za Iran kwenye mataifa ya kigeni, na kuwa waziri wake wa Mambo ya nje linapokuja suala la vita na amani.

Inasadikiwa kwamba alikuwa mshirika wa rais Bashar al-Assad katika vita dhidi ya waasi nchini Syria, kubuniwa kwa vikosi vya angani vinavyoungwa mkono na Iraq, mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State, na mengine mengi.

Akiwa mkuu wa kikosi cha Quds Soleimani alisimamia operesheni za kijeshi nje ya Iran katika hatua ambayo ilimfanya kuingia uhasama na Marekani wakati wa vita vya Iraq akionekana kuwa mfadhili wa makundi ya wanamgambo wa kishia.

Kwanini Marekani ilimlenga?

Marekani iliilaumu kikosi cha Quds kwa shambulio la Karbala lililosababisha vifo vya wanajeshi wake watano pamoja na kutoa mafunzo kwa watengenezaji mabomu yaliotumika kuvilenga vikosi vyake.

Tangu mwaka 2013, Afisa wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), John Maguire, aliliambia gazeti la New York kwamba Soleimani "alikuwa mtu mmoja mwenye uwezo mkubwa mashariki ya kati".

Mwisho wake ulikuwa ghafla na ulikumbwa na ghasia.

Januari 3 Pentagon ilitangaza kuwa ilimuua Jenerali huyo kufuatia agizo la rais Donald Trump.

Pentagon ilitangaza kuwa ilimuua Jenerali huyo kufuatia agizo la rais Donald Trump.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pentagon ilitangaza kuwa ilimuua Jenerali huyo kufuatia agizo la rais Donald Trump.

Mauaji yake yamefuatia kuongezeka kwa uhasama mkali kati ya Marekani na Iran pamojana makundi yanayoungwa mkono na Iran- nchini Iraq baada ya kifo cha afisa wa kijeshi wa Marekani kuuawa katika shambulio la makombora katika kambi ya kijeshi ya Mraekani nchini Iraq - ambayo Marekani iliilaumu Iran.

Marekani ilijibu hatua hiyo kwa mashambulizi ya angani dhidi ya waaasi wa Kataib Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.

Wafuasi wa waasi hao baadae wakashambulia ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.

Hali ya taharuki kati ya Marekani na Iran imekuwa ikiongezeka baada ya Marekani kujiondoa katika mkataba wa kimataifa wa nyukilia hatua iliyoifanya Iran kurejelea mpango wake wa uundaji silaha za nyuklia.

Marekani iliiwekea upya vikwazo Iran, hali ambayo iliathiri uchumi wake.

Wasiifu wake

Soleimani anaamini kulelewa katika familia masikini na hakupokea masomo rasmi.

Amepanda katika ngazi ya kikosi cha ulinzi wa Iran Revolutionary Guards - kupitia kikosi chake cha Quds ambacho kinaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, na ilipewa hadhi ya shujaa wa kitaifa.

Tangu mwaka 1998, Meja Jenerali Qasem Soleimani ameongoza vikosi vya Quds nchini Iran- kitengo maalum cha jeshi la Iran (Revolutionary Guards) ambacho huendesha opareshani zake nje ya nchi.

Alikuwa kiungo muhimu katika mapambano ya kimkakati mashariki ya kati kupitia vikosi vya Quds, ambavyo vinaendesha oparesheni yake kwa ushirikiano na jeshi la ulinzi la Iran.

Usuhuba wake na Ayatollah Ali Khamanei

Jina lake lilianza kuwa maarufu alipopewa nafasi ya kuongoza kikosi cha Quds na kujenga ushirikiano wa karibu na kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Khamenei kiasi wakati mmoja kiongozi huyo alishiriki na kufungua dhifa ya harusi ya binti ya Jenerali Soleimani.

Meja jenerali Qasem Soleimani, na vikosi vyake vinafanya kazi chini ya kiongozi mkuu wa kidini, Ayatollah Ali Khamanei, badala ya kufuata muundo wa kawaida wa kijeshi wa Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitaja jeshi la ulinzi la Iran Revolutionary Guards na washirika wake vikosi vua Kikurdi kama shirika la kigeni la ugaidi mwezi April mwaka jana.

Jenerali Qasem Soleimani hakuwa anajulikana na wengi nchini Iran hadi mwaka 2003 wakati Marekani ilipoivamia kijeshi Iraq.

Umashuhuri wake uliimarika hatua ambayo ilifanya maafisa kadhaa wa Marekani kutoa wito wa kuuliwa kwake.

Muongo mmoja na nusu baadae Soleimani alifikia kuwa kamanda maarufu wa vita nchini Iran kiasi akipuuza miito ya umma kumtaka aingie kwenye siasa.

Baada ya Marekani kuivamia Iraq kijeshi mwaka 2003 alianza kutoa amri kwa makundi ya waasi kushambulia kambi ya kijeshi ya Marekani, na kuwaua mamia.