Morocco yailaza Nigeria kwa penalti na sasa itamenyana na Senegal katika fainali ya Afcon

Chanzo cha picha, Getty Images
Morocco, taifa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika, iliungana na Senegal katika fainali baada ya kuwalaza Nigeria 4-2 kupitia mikwaju ya penalti Jumatano kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat katika nusu-fainali ya pili iliochezwa jana usiku.
Baada ya ushindi huo, itacheza Jumapili ijayo kwenye uwanja huo huo dhidi ya Senegal, ambayo iliifunga Misri 1-0 mapema Jumatano mjini Tangier.
Kipa Yassine Bounou aliiongoza nchi yake kuendeleza ndoto yake ya kutwaa taji la pili katika historia yake na la kwanza katika kipindi cha miaka 50 alipong'ara kwenye mikwaju ya penalti kwa kuokoa penalti mbili ambazo zilitosha kuwashinda Nigeria, mshindi wa pili wa toleo lililopita, 4-2 (muda wa kawaida na wa ziada kutoka 0-0).
Bono aliokoa penalti kutoka kwa Samuel Chukwueze na Bruno Onyeamachi, huku mchezaji wa akiba Youssef En-Nesyri akifunga penalti hiyo muhimu.
Umati ulishusha pumzi wakati wa mikwaju ya penalti baada ya Hamza Ighmane kukosa penalti ya pili, lakini Chukwueze alikosa mkwaju wake huku Ilyas Ben Sghir, Achraf Hakimi, na Youssef En-Nesyri wakifunga penalti zao tatu zilizofuata, naye Farouk Dele Bechir akifunga ya tatu na Onyemechi wa Nigeria akakosa ya nne.
Bono alisema, "Nawashukuru mashabiki kwa usaidizi wao. Hali ilikuwa nzuri, wachezaji walijitahidi sana, mpinzani alikuwa sawa, na kocha (Walid Regragui) alijiandaa vyema kwa mechi hii. Tunamshukuru Mungu tumepata matokeo yaliyotarajiwa."
Inafaa kukumbukwa kuwa hii ni mara ya pili kwa Morocco kutinga fainali, baada ya toleo la 2004 waliposhindwa na wenyeji Tunisia 1-2.
Ushindi huu pia ni wa nne kwa Morocco dhidi ya Nigeria katika mechi sita kati yao, ikilinganishwa na kupoteza mbili na sare moja. Kati ya ushindi huo wa nne, mbili zilikuwa katika toleo la 1976 wakati Atlas Lions ilishinda taji lao la kwanza na la pekee hadi sasa.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Morocco hawajafungwa katika mechi 5 katika toleo la sasa, ambalo ni rekodi bora zaidi.
Kinyume chake, Nigeria, ambayo ilikuwa na matumaini ya kushinda taji lake la nne katika historia ili kufidia kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia majira ya joto yajayo, ilipoteza kwa mara ya kwanza katika Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kurekodi ushindi katika mechi zake tano za kwanza, ya mwisho ikiwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Algeria katika robo fainali.
Nigeria pia ilishindwa kufika fainali yake ya tisa katika historia yake baada ya 1980, 1984, 1988, 1990, 1994, 2000, 2013 na 2023.
Walid Regragui alipanga kikosi kile kile kilichoilazaCameroon 2-0 katika robo-fainali, na "Super Eagles" hawakufanya vyema zaidi ya Indomitable Lions, wakitengeneza nafasi moja pekee katika muda wote wa mechi.
Safu ya ulinzi ya Morocco ilikabili tishio la mashambulizi makali zaidi ya Nigeria kwenye michuano hiyo (mabao 14), hasa Victor Osimhen, Ademola Lookman na Akor Adams, huku safu ya kati ikiteseka kutokana na kukosekana kwa nahodha wake, kiungo Wilfred Ndidi, aliyefungiwa.
Morocco walipata nafasi za hatari zaidi, wakianza kwa shuti kali la Ibrahim Abdelkader Dias ndani ya eneo (9), ambalo lilijibiwa na Lookman kwa shuti kali kutoka nje ya eneo ambalo Bono alilipangua kwa shida (15).
Senegal yafuzu fainali baada ya kuilaza Misri

Chanzo cha picha, Getty Images
Mapema Jumatano, timu ya taifa ya kandanda ya Senegal iliwashinda wenzao wa Misri katika nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa bao 1-0.
Mchezaji nyota wa Senegal, Sadio Mane, aliifungia Senegal bao katika dakika ya 77 ya mchezo huo, baada ya timu yake ya taifa kutawala mchezo na kusababisha tishio katika lango la timu ya taifa ya Misri tangu mwanzo wa mechi.
Hossam Hassan, kocha wa timu ya taifa ya Misri, alikuwa ametumia mbinu alioufuata katika mechi zilizopita dhidi ya Ivory Coast, ambayo ni (5-3-2).
Hata hivyo, mwanzo ulikuwa tofauti kwa timu ya Misri iliyocheza kwa kulinda lango lake hasa mwanzoni mwa kipindi cha pili.
Katika mchezo huo mwamuzi alitoa kadi nyingi za njano, ya kwanza kwa mchezaji wa Misri Hossam Abdel-Maguid na ya pili kwa mchezaji wa Senegal Habib Diarra. Mwamuzi pia alionyesha kadi ya njano kwa mchezaji wa Senegal Coulibaly.
Katika hatua ya mtoano, timu ya taifa ya Misri iliendeleza uchezaji wake mzuri, kwa kuishinda Benin 3-1 baada ya kutumia muda wa ziada katika hatua ya 16 bora, na kisha kuifunga Ivory Coast 3-2 katika mechi ya kusisimua ya robo fainali.
Kwa upande mwingine, timu ya taifa ya Senegal iliingia uwanjani kwa kujiamini sana baada ya kufanya vyema wakati wa michuano hiyo, ikianza kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Botswana, kisha kutoka sare ya 1-1 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kabla ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Benin.
Katika hatua ya 16 bora, Simba ya Teranga iliilaza Sudan mabao 3-1, kisha ikailaza Mali kwa bao 1-0 katika robo fainali.
Timu ya taifa ya Senegal inachukuliwa kuwa moja ya timu zenye ulinzi mkali katika michuano hiyo, ikiwa imeruhusu mabao mawili pekee hadi sasa, kutokana na uchezaji bora wa golikipa wao mkuu, Edouard Mendy, unaoakisi ugumu wa kupenya ngome yao.
Mechi hiyo ilikuwa na kipengele cha kulipiza kisasi kwa timu ya taifa ya Misri, hasa kutokana na kwamba kizazi cha sasa kilipoteza kwa Senegal katika matukio mawili muhimu; ya kwanza katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2021, ambapo Mafarao walipoteza kwa mikwaju ya penalti, na ya pili katika mechi za kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022, ambapo timu ya Senegal pia ilishinda kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya jumla ya mechi mbili za nyumbani na ugenini.
Kabla ya pambano la timu hizo mbili katika nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Morocco, kocha wa timu ya taifa ya Misri Hossam Hassan, akizungumza mjini Tangier, alithibitisha kwamba ushindani kati ya nahodha wa Mafarao Mohamed Salah na mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool, mchezaji wa kimataifa wa Senegal, Sadio Mane, ni "mfano mzuri kwa soka la Afrika."












