Zozibini Tunzi: Changamoto zinazowakumba wanawake weusi katika mashindano ya malkia wa urembo duniani

Zozibini Tunzi alishinda taji la bi Universe siku ya Jumapili , akiwa mwanamke wa kwanza mweusi kufanya hivyo na nywele zake asilia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zozibini Tunzi alishinda taji la bi Universe siku ya Jumapili , akiwa mwanamke wa kwanza mweusi kufanya hivyo na nywele zake asilia

Wakati Zozibini Tunzi wa Afrika kusini alipotawazwa kuwa malkia wa Urembo wa taji la MIss Universe siku ya Jumapili , ilikuwa mara ya kwanza kwa mwanamke mweusi kushinda mataji makuu manne ya malkia wa urembo duniani.

Vyombo vya habari vilichapisha habari hiyo na wengi katika mitandao ya kijamii walisherehekea.

Baadhi yao walisema kwamba pamoja na bi Tunzi , Cheslie Kryst malkia wa urembo wa Marekani, na Nia Franklin malkia wa urembo Amerika , wanawakilisha kizazi kipya cha malkia wa urembo tofauti.

Bi Tunzi hususan amepongezwa kwa ngozi yake nyeusi na nywele zake nyeusi fupi.

Zozibini Tunzi muda mfupi aliposhinda taji la malkia wa Universe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vyombo vya habari vilichapisha habari hiyo na wengi katika mitandao ya kijamii walisherehekea pindi Mwanamke huyo mweusi alipotangzwa kuwa mshindi.

Hata malkia wa urembo wa Marekani 2016 Deshauna Barber alisambaza kanda ya video katika mtandao wa Instagram kuhusu hisia zake muda tu bi Tunzi aliposhinda.

''Malkia wa Universe anafanana nami'' - alipiga kelele katika kamera mara kwa mara. Lakini bi Barber pia aliambia BBC kwamba wanawake weusi wanabaguliwa kirangi wakati wa mashindano hayo na kwamba uwakilishi zaidi unaweza kuwa hatua ya kwanza katika kukabiliana na changamoto hiyo.

''Unapotoka katika kundi ambalo halina uwakilishi mkubwa ni vigumu kuelewa uwakilishi nini'', alisema.

'Niliogopa kushiriki na nywele zangu zilizosokotana'

Gabriela Taveras - ambaye ni mwanamke wa kwanza kushinda shindano la bi Massachussets alisema kwamba swala moja ni kwamba wanawake weusi hawakuafikia masharti ya kushiriki katika mashindano ya urembo .

''Kuna lile wazo la ni nini urembo'', alisema. ''Hapo zamani wazo hilo lilikuwa mwanamke mweupe''.

Gabriela Taveras akiwa na nywele zake nyeusi na taji aliloshinda

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bi Taveras alisema kwamba nywele zake hazikuafikia masharti kiwango cha urembo Ulaya

Bi Taveras alituzwa taji hilo mwaka 2018 na akaendelea kushiriki katika shindano la bi Amerika na kuwa katika nafasi tano bora. Mojawapo ya uamuzi mkubwa alioufanya ni kuonyesha nywele zake.

''Nakumbuka vita vya nywele laini dhidi ya zile zilizojisokota'', alisema ulikuwa mjadala m'baya sana kwa kweli.

''Niliogopa kuonyeshwa nywele zangu nyeusi zilizojisokota kwasababu nilijua hazikuafikia kiwango cha Ulaya cha urembo''.

Aliamua kuendelea kushindana akiwa na nywele zake zilizojisokota . Wakati wasichana wadogo walipomwambia kwamba walifurahia kwa kuwa alifanana nao , alijua amefanya uamuzi wa busara.

''Nilijua nilifanana na kujihisi mwenyewe'', alisema. Nilijua nimejifanya kuwa mimi mwenyewe na sikuwa nikitaka kuwa mtu mwengine''.

Bi Barber pia alisema kwamba aliogopa kuwa na nywele zake asilia akidhania kwamba zingeharibu fursa yake hivyobasi hakuzionyesha wakati wa mashindano hayo.

Lakini wakati wa shindano la malkia wa urembo Marekani alivalia nywele zake kuonyesha heshima kwa mamake aliyefariki.

''Alikuwa akinitaka mara kwa mara katika mashindano yote ya malkia wa urembo kuonyesha nywele zangu asilia, lakini nilikuwa nikiogopa sana''.

Deshauna Barber akiwa jukwaani akiwa amevalia nywele zake asiliao

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bi Barber alivalia nywele asili katika shindano lake la mwisho kama malkia wa urembo wa Marekani 2017.

Bi Barber anasema kwamba pia amekabiliwa na ubaguzi wa rangi - ama ubaguzi dhidi ya rangi yake wakati wa mashindano. Ana ngozi nyeusi na baadhi ya watu hawakuiona rangi yake ya ngozi kuwa na mvuto.

'Hakuna aliyekuwa akiwachanganya wenye nywele nyeupe'

"Mwaka wangu kulikuwa na wanawake wengi weusi waliokuwa wakishiriki katika shindano la malkia wa urembo la bi America'', bi Taveras alisema.

''Unapotazama historia kushiriki shindano hilo lilikuwa jambo zuri sana. laskini hilo lilisababisha changamoto zake ''.

Bi Taveras alisema kwamba watu wangechanganya wanawake weusi walioshiriki.

''Wakati mmoja nilikuwa nyuma ya jukwaa nikisubiri kuitwa , na mtu mmoja alikuja kwangu na kusema: Luosiana, nenda unaitwa;, hadi kufikia kiwango ambacho hawakuniamini kwa mara ya kwanza niliposema sio mimi''.

Watu wengine wangewachanganya washirika wengine weusi wakati walipokuwa na ngozi tofauti . lakini aliongezea, ''hakuna mtu aliyekuwa akiwachanganya wanawake wenye nywele nyeupe.

'Hawajawahi kumchagua mwanamke kama wewe'

Pia alisema kwamba kulikuwa na shinikizo la juu kama mwanamke mweusi , akijaribu kupita kati ya laini ya kujiwakilisha na pia kuhisi kana kwamba anawakilisha kundi kubwa la watu.

''Kiwango cha makosa yako ni kidogo mno'' , alisema. ''Kuna kile kiwango ambacho hatuwezi kuthibitisha upendeleo walio nao dhidi yetu''.

Shindano la malkia wa urembo wa Amerika 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bi Taveras alisema kwamba shindano la malkia wa urembo Amerika 2018 lilishirikisha wanawake wengi weusi

Hata wakati wanawake weusi wanaposhinda taji la malkia mweusi , bi Taveras alisema kwamba hawakupata pongezi waliohitaji kupewa.

''Watu wangesema kwamba alishinda taji lake kwa kuwa ni mtu mweusi. Walitumia rangi yangu kuwa silaha dhidi yangu''.

Bi Barber alihisi ukosoaji kama huo , akisema kwamba ni matusi kwa sababu inamaanisha hatuwezi kufaulu kutokana na uwezo wetu ama kwasababu sisi ndio tulio na uwezo mkubwa wa kufuzu.

Wakati bi Taveras alipokuwa akishindana kuwa malkia wa urembo wa kwa kwanza mweusi kushiriki katika taji la malkia wa Massachussets katika historia ya taji hilo, hadi familia yake ilikuwa na wasiwasi.

''Baadhi ya watu wa familia yangu walisema: Ni lini utasalimu amri? Hawajawahi kuchagua msichana kama wewe''.

Na baadaye kulikuwa na matamshi ya kibaguzi ya moja kwa moja , hususan kutoka kwa watu mitanadoni . wanawake wote walitumia maeneo kama 'tumbili' ili kukosoa kushiriki kwao.

Zozibini Tunzi baada ya kushinda taji la maklia wa urembo la Miss Universe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malkia mpya wa urembo ulimwenguni bi Tunzi anasema kwamba alilelewa kaika ulimwengu ambao wanawake waliofanana naye hawakuonekana kuwa warembo

'Shindano la malkia wa urembo linabadilika'

Licha ya changamoto ambazo zinawakumba wanawake weusi katika mashindano ya malkia wa urembo , wanawake wote wawili wanafurahia kuhusu mataji yanayomilikiwa na wanawake weusi na wana matumaini katika siku za usoni.

''Tupo katika wakati ambapo shindano hilo linabadilika na hicho ni kitu ambacho kinawafanya watu wengi kutohisi vyema, lakini inawafanya watu kama mimi kusherehekea'' , alisema bi Barber.

''Sio kuhusu wanawake weusi pekee na mashindano ya malkia wa urembo'' , alisema, lakini pia kila kundi ambalo halikuwakilishwa vyema.

''Ninasubiri kuona malkia wa urembo wa Miss Universe aliyenona ama malkia wa urembo wa Miss Universe aliyevalia hijab''.

Bi Taveras anakubali na kutumaa kwamba mabadiliko hayo pia yatawasaidia wanawake wasioshiriki shindano hilo.

''Kila siku nasikia vijana na wanawake wakizungumzia kuhusu jinsi walivyonona , ama hawapendi sura zao ama pua'', alisema. ''Natumai hilo litawatia moyo wengi''.