Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Zozibini Tunzi: Changamoto zinazowakumba wanawake weusi katika mashindano ya malkia wa urembo duniani
Wakati Zozibini Tunzi wa Afrika kusini alipotawazwa kuwa malkia wa Urembo wa taji la MIss Universe siku ya Jumapili , ilikuwa mara ya kwanza kwa mwanamke mweusi kushinda mataji makuu manne ya malkia wa urembo duniani.
Vyombo vya habari vilichapisha habari hiyo na wengi katika mitandao ya kijamii walisherehekea.
Baadhi yao walisema kwamba pamoja na bi Tunzi , Cheslie Kryst malkia wa urembo wa Marekani, na Nia Franklin malkia wa urembo Amerika , wanawakilisha kizazi kipya cha malkia wa urembo tofauti.
Bi Tunzi hususan amepongezwa kwa ngozi yake nyeusi na nywele zake nyeusi fupi.
Hata malkia wa urembo wa Marekani 2016 Deshauna Barber alisambaza kanda ya video katika mtandao wa Instagram kuhusu hisia zake muda tu bi Tunzi aliposhinda.
''Malkia wa Universe anafanana nami'' - alipiga kelele katika kamera mara kwa mara. Lakini bi Barber pia aliambia BBC kwamba wanawake weusi wanabaguliwa kirangi wakati wa mashindano hayo na kwamba uwakilishi zaidi unaweza kuwa hatua ya kwanza katika kukabiliana na changamoto hiyo.
''Unapotoka katika kundi ambalo halina uwakilishi mkubwa ni vigumu kuelewa uwakilishi nini'', alisema.
'Niliogopa kushiriki na nywele zangu zilizosokotana'
Gabriela Taveras - ambaye ni mwanamke wa kwanza kushinda shindano la bi Massachussets alisema kwamba swala moja ni kwamba wanawake weusi hawakuafikia masharti ya kushiriki katika mashindano ya urembo .
''Kuna lile wazo la ni nini urembo'', alisema. ''Hapo zamani wazo hilo lilikuwa mwanamke mweupe''.
Bi Taveras alituzwa taji hilo mwaka 2018 na akaendelea kushiriki katika shindano la bi Amerika na kuwa katika nafasi tano bora. Mojawapo ya uamuzi mkubwa alioufanya ni kuonyesha nywele zake.
''Nakumbuka vita vya nywele laini dhidi ya zile zilizojisokota'', alisema ulikuwa mjadala m'baya sana kwa kweli.
''Niliogopa kuonyeshwa nywele zangu nyeusi zilizojisokota kwasababu nilijua hazikuafikia kiwango cha Ulaya cha urembo''.
Aliamua kuendelea kushindana akiwa na nywele zake zilizojisokota . Wakati wasichana wadogo walipomwambia kwamba walifurahia kwa kuwa alifanana nao , alijua amefanya uamuzi wa busara.
''Nilijua nilifanana na kujihisi mwenyewe'', alisema. Nilijua nimejifanya kuwa mimi mwenyewe na sikuwa nikitaka kuwa mtu mwengine''.
Bi Barber pia alisema kwamba aliogopa kuwa na nywele zake asilia akidhania kwamba zingeharibu fursa yake hivyobasi hakuzionyesha wakati wa mashindano hayo.
Lakini wakati wa shindano la malkia wa urembo Marekani alivalia nywele zake kuonyesha heshima kwa mamake aliyefariki.
''Alikuwa akinitaka mara kwa mara katika mashindano yote ya malkia wa urembo kuonyesha nywele zangu asilia, lakini nilikuwa nikiogopa sana''.
Bi Barber anasema kwamba pia amekabiliwa na ubaguzi wa rangi - ama ubaguzi dhidi ya rangi yake wakati wa mashindano. Ana ngozi nyeusi na baadhi ya watu hawakuiona rangi yake ya ngozi kuwa na mvuto.
'Hakuna aliyekuwa akiwachanganya wenye nywele nyeupe'
"Mwaka wangu kulikuwa na wanawake wengi weusi waliokuwa wakishiriki katika shindano la malkia wa urembo la bi America'', bi Taveras alisema.
''Unapotazama historia kushiriki shindano hilo lilikuwa jambo zuri sana. laskini hilo lilisababisha changamoto zake ''.
Bi Taveras alisema kwamba watu wangechanganya wanawake weusi walioshiriki.
''Wakati mmoja nilikuwa nyuma ya jukwaa nikisubiri kuitwa , na mtu mmoja alikuja kwangu na kusema: Luosiana, nenda unaitwa;, hadi kufikia kiwango ambacho hawakuniamini kwa mara ya kwanza niliposema sio mimi''.
Watu wengine wangewachanganya washirika wengine weusi wakati walipokuwa na ngozi tofauti . lakini aliongezea, ''hakuna mtu aliyekuwa akiwachanganya wanawake wenye nywele nyeupe.
'Hawajawahi kumchagua mwanamke kama wewe'
Pia alisema kwamba kulikuwa na shinikizo la juu kama mwanamke mweusi , akijaribu kupita kati ya laini ya kujiwakilisha na pia kuhisi kana kwamba anawakilisha kundi kubwa la watu.
''Kiwango cha makosa yako ni kidogo mno'' , alisema. ''Kuna kile kiwango ambacho hatuwezi kuthibitisha upendeleo walio nao dhidi yetu''.
Hata wakati wanawake weusi wanaposhinda taji la malkia mweusi , bi Taveras alisema kwamba hawakupata pongezi waliohitaji kupewa.
''Watu wangesema kwamba alishinda taji lake kwa kuwa ni mtu mweusi. Walitumia rangi yangu kuwa silaha dhidi yangu''.
Bi Barber alihisi ukosoaji kama huo , akisema kwamba ni matusi kwa sababu inamaanisha hatuwezi kufaulu kutokana na uwezo wetu ama kwasababu sisi ndio tulio na uwezo mkubwa wa kufuzu.
Wakati bi Taveras alipokuwa akishindana kuwa malkia wa urembo wa kwa kwanza mweusi kushiriki katika taji la malkia wa Massachussets katika historia ya taji hilo, hadi familia yake ilikuwa na wasiwasi.
''Baadhi ya watu wa familia yangu walisema: Ni lini utasalimu amri? Hawajawahi kuchagua msichana kama wewe''.
Na baadaye kulikuwa na matamshi ya kibaguzi ya moja kwa moja , hususan kutoka kwa watu mitanadoni . wanawake wote walitumia maeneo kama 'tumbili' ili kukosoa kushiriki kwao.
'Shindano la malkia wa urembo linabadilika'
Licha ya changamoto ambazo zinawakumba wanawake weusi katika mashindano ya malkia wa urembo , wanawake wote wawili wanafurahia kuhusu mataji yanayomilikiwa na wanawake weusi na wana matumaini katika siku za usoni.
''Tupo katika wakati ambapo shindano hilo linabadilika na hicho ni kitu ambacho kinawafanya watu wengi kutohisi vyema, lakini inawafanya watu kama mimi kusherehekea'' , alisema bi Barber.
''Sio kuhusu wanawake weusi pekee na mashindano ya malkia wa urembo'' , alisema, lakini pia kila kundi ambalo halikuwakilishwa vyema.
''Ninasubiri kuona malkia wa urembo wa Miss Universe aliyenona ama malkia wa urembo wa Miss Universe aliyevalia hijab''.
Bi Taveras anakubali na kutumaa kwamba mabadiliko hayo pia yatawasaidia wanawake wasioshiriki shindano hilo.
''Kila siku nasikia vijana na wanawake wakizungumzia kuhusu jinsi walivyonona , ama hawapendi sura zao ama pua'', alisema. ''Natumai hilo litawatia moyo wengi''.