Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Miss Universe 2019: Anasema dhana ya kuwa ngozi nyeusi sio kigezo cha urembo yapaswa kukoma
''Nilikua katika ulimwengu ambao mwanamke anayefanana na mimi, kwa rangi ya ngozi yangu na aina ya nywele zangu, anaonekana si mrembo''.
''Ninafikiri ni wakati sasa hali hiyo ikomeshwe.''
Huo ni ujumbe wa mshindi mpya wa michuano ya Miss Universe Zozibini Tunzi, kutoka Afrika Kusini.
Zaidi ya wanawake 90 kutoka duniani kote walishiriki kwenye mshindano hayo yaliyofanyika Atlanta nchini Marekani siku ya Jumapili.
Zozibini alimshinda Madison Anderson wa Puerto Rico na Aofia Aragon wa Mexico.
Waliofaulu kuingia fainali ya mashindano hayo waliulizwa maswali kuhusu maada mbalimbali kama vile mazingira, maandamano na mitandao ya kijamii.
Katika swali lake la mwisho, mshiriki Zozibini mwenye miaka 26 aliulizwa kuhusu jambo gani tunapaswa kuwafundisha wasichana wa leo.
Jibu lake lilikuwa uongozi.
''Ni kitu ambacho kinakosekana kwa wasichana na wanawake kwa muda mrefu- si kwa sababu hatutaki, lakini kwa sababu jamii inavyotaka tuwe,'' alisema.
''Ninafikiri ni viumbe wenye nguvu sana duniani, na kuwa tunapaswa kupatiwa kila fursa.
''Na hicho ndicho tunachopaswa kuwafundisha mabinti wadogo.''
Washiriki wengine wakimpongeza kwa makofi Zozibini Tunzi
Zozibini ni mwanamke wa kwanza mweusi kushinda kwenye mashindano hayo tangu Lila Lopes aliponyakua taji hilo mwaka 2011.
Hashtag #MissUniverse ilisambaa kwenye mtandao wa Twitter na hata akapata salamu za pongezi kutoka kwa Oprah Winfrey.
Watu kadhaa walieleza umuhimu mkubwa wa wanawake weusi wakiwa na nywele za asili kushinda taji hilo la urembo.
Washindi wa taji la Miss Universe kutoka Afrika
Miss Universe 1999: Alishinda Mpule Keneilwe Kwelagobe kutoka nchini Botswana
Miss Universe 2011:Alishinda Leila Lopes wa Angola
Unaweza pia kutazama