Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Villa inamfukuzia Mateta Crystal Palace
Aston Villa imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 28, huku The Eagles wakimsaka mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Evann Guessand, 24. (Athletic - usajili unahitajika)
Villa pia inaongeza juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Roma Tammy Abraham, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Besiktas, huku maafisa wa klabu hiyo wakimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 akicheza mjini Istanbul Jumatatu. (Sky Sports), nje
Ajax inataka kumsajili Manuel Ugarte, 24, kwa mkopo huku ikimtafuta kiungo mkabaji lakini Manchester United haina mpango wa kumtoa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay. (Athletic- Usajili unahitajika)
Mkufunzi wa Borussia Dortmund Niko Kovac ameibuka kama jina jipya kwenye orodha ya Manchester United ya meneja anayefuata lakini kocha mkuu wa England Thomas Tuchel na Roberto de Zerbi wa Marseille wanasalia kuwa walengwa wawili wakuu. (Mirror)
Inter Milan inataka kumsajili mlinda lango wa Aston Villa Emiliano Martinez, 33, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina atalazimika kukubali kupunguziwa mshahara ili kusaini msimu ujao. (Sky Sports)
Muda wa mkopo wa Leon Bailey katika klabu ya Roma umekatizwa huku winga huyo wa Jamaica mwenye umri wa miaka 28 akirejea Aston Villa. (Sky Sports - kwa Kiitaliano)
Fulham itamenyana na Wolfsburg na Real Betis katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambulizi wa Jamhuri ya Ireland Troy Parrott, 23, kutoka AZ Alkmaar msimu wa joto. (Independent)
Kocha wa Coventry City, Frank Lampard anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Oliver Glasner kama meneja wa Crystal Palace huku klabu hiyo ikimtaka Jose Bordalas wa Getafe na Inigo Perez wa Rayo Vallecano. (Talksport)
Sunderland haina nia ya kumuuza kiungo wa kati wa DR Congo Noah Sadiki, 21, kwa Manchester United lakini ipo tayari kupokea ofa za wachezaji wasio na uwezo kama mkubwa vile kipa Mwingereza Anthony Patterson, 25, na kiungo wa kati wa zamani wa England aliye na umri wa chini ya miaka-20 Dan Neil, 24. (Sun)
Everton imemuulizia mshambuliaji wa Sunderland Mfaransa Wilson Isidor, 25, huku ikilenga kuimarisha safu yake ya ushambuliaji. (Mirro)
Beki wa Sheffield Wednesday, 17, Muingereza Yisa Alao anakaribia kujiunga na Januari klabu ya Chelsea. (Sheffield Star)