Surua DR Congo: Kwanini kuna 'janga la ghafla la surua duniani'?

The authorities are planning to vaccinate a further 1.4 million people against measles

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wanapanga kuwachanja watu milioni 1.4 zaidi dhidi ya surua

Janga la Surua limetangazwa katika Jamhuri ya kidmeokrasi ya Congo.

Waziri wa afya anasema takriban visa 87,000 vinavyoshukiwa vya ugonjwa huo vimenakiliwa tangu kuanza kwa mwaka huu.

Kumeripotiwa visa vya surua katika majimbo 23 kati ya 26 nchini Congo, katika maeneo ya mashambani na mijini pia.

Licha ya kwamba surua huambukizwa, unaweza kuzuiwa kwa chanjo sahihi.

Hatahivyo, ugonjwa huo umeongezeka kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni kutokana na miundo mbinu duni, ukosefu wa usalama na mfumo duni katika sekta ya afya.

Inaaminika kufikia sasa Surua imesababisha vifo vya takriban watu 1, 500 nchini tangu mwanzoni mwa mwaka 2019 , wengi wao wakiwa ni watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano

Duru kutoka ndani ya nchi katika kitengo cha utoaji chanjo zimeiambia BBC kwamba wanachangisha fedha hivi sasa kupanga kampeni ya kusambaza chanjo kuzuia kusambaa kwa virusi katika maeneo ambayo hayaja athirika.

Zaidi ya watoto milioni mbili walipewa chanjo dhidi ya surua au ukambi mnamo Aprili na wengine milioni 1.4 wanalengwa katika kampeni inayotarajiwa kuanza katika siku chache zijazo katika vituo vya afya vilivyopokea wagonjwa wa surua.

Katika taarifa, madaktari wa misaada wasiokuwa na mipaka, wameonya kwamba huenda janga hili likawa baya zaidi kushuhudiwa tangu jingine lililozuka mnamo 2011-2012.

Presentational grey line

Kwanini kunashuhudiwa 'janga la ghafla la surua duniani'?

Visa vya ugonjwa wa surua vilivyoripotiwa kote duniani katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2019 vimeongezeka mara tatu ikilinganishwa na hali ilivyokuwa wakati kama huu mwaka jana kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO).

Ni mojawapo ya virusi vinavyoambukiza pakubwa, hatahivyo hakuna kilichobadilika kuhusu ugonjwa wa surua. Sio kwamba umegeuka kuwa hatari zaidi, badala yake majibu yote yanatokana na hatua ya binaadamu.

Kuna hadithi mbili hapa - moja kuhusu umaskini na nyingine kuhusu kusambaa kwa taarifa za uongo. Katika mataifa ya kimaskini watu wachache wanapewa chanjo na sehemu kubwa ya watu wanaachwa katika hatari ya kuugua ugonjwa huo.

Hii hutoa nafasi ya kushuhudiwa mlipuko mkubwa kama ilivyoshuhudiwa katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo, Kyrgyzstan na Madagascar.

Lakini mataifa yalio na viwango vikubwa vya utoaji chanjo vinashuhudia kuongezeka kwa ugonjwa huu. Na hii ni kutokana na kwamba baadhi ya watu wanaamua kutowapeleka watoto wapewe chanjo kutokana na kusambaa kwa taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii dhidi ya chanjo hizo.

Ni muhimu kutambua kwamba takwimu hizi ni za awali, shirika la afya duniani linasema takwimu halisi zitakuwa juu zaidi. Na kwamba surua au ukambi ni tishio. Husababisha vifo vya takriban watu laki moja, wengi wao watoto kila mwaka.

Presentational grey line
measles

Chanzo cha picha, MAMYRAEL

Wakuu hao wa WHO wameandika kwamba "inaeleweka, katika mazingira hayo wazazi wanaweza kupotea" lakini kwamba "mwisho wa kwisha faida za chanjo hiyo hazina mjadala".

Wameongeza: "Maisha ya zaidi ya watu milioni 20 yameokolewa kwa chanjo ya surua tangu mwaka 2000 pekee yake."

Dalili za surua

  • Kuhisi baridi na kupiga chafya
  • Homa kali,uchovu,kukosa hamu ya kula na misuli kuuma
  • Macho kuwa na rangi nyekundu na majimaji kama unataka kulia
  • Kuwa na rangi ya kijivu mdomoni
  • Kuwa na vipele vyenye rangi nyekundu ambavyo vinaweza kusambaa kutoka kwenye kichwa,shingoni mpaka kwenye mwili wote.

Kutokana na mlipuko wa hivi karibuni wa surua, kumetolewa wito katika mataifa tofuati duniani kuhakikisha kwamba watoto wanapewa chanjo kwa lazima.