WHO:Ongezeko kubwa la ugonjwa wa surua lipo barani ulaya

Chanzo cha picha, SPL
Shirika la afya duniani(WHO) linasema kwamba kuna ongezeko kubwa la kesi za ugonjwa wa surua zipo Barani Ulaya.
Zaidi ya watu elfu arobaini na moja wameambukizwa katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2018.
Mwaka jana kulikuwa na kesi 23,927 na mwaka mmoja kabla kulikuwa na kesi 5,273.
Wataalam wa afya wanalaumu juu ya ongezeko kubwa la watu kuambukizwa ugonjwa huo ni kutokana na wengi kuacha kuzingatia chanjo.
Uingereza kumekuwa na kesi 807 mpaka sasa kwa mwaka huu.Shirika la afya duniani'WHO 'imeyataka mataifa ya ulaya kuchukua hatua thabiti
Wizara ya afya nchini Uingereza imesema mlipuko wa ugonjwa huo umetokana na idadi kubwa ya watu kusafiri katika maineo ya bara la ulaya ambayo yana maambukizi.
Surua inaambukizwa zaidi watu wakikohoa au kupiga chafya.
Maambukizi yanaweza kudumu kwa muda wa siku saba mpaka kumi.Lakini watu wengi waliopona kabisa huwa wanabaki na matatizo mbalimbali kama;
Madhara kwenye ubongo
Homa kali
Kupungua kwa mwili
Nomonia
matatizo la ini
Utafiti uliofanywa miaka 20 iliyopita unaonyesha namna gani watu hawatilii maanani chanjo kama ilivyo kwenye matatizo ya utindio wa ubongo
Wizara ya afya nchini humo inawataka watoto wote kupata chanjo kabla hawajatimiza umri wa mwaka mmoja na kabla hawajaanza kwenda shule.
Ukraine ina idadi kubwa ya ugonjwa wa surua barani ulaya kwa watu zaidi ya watu 23,000 ambao wameathirika.
Lakini kuna nchi nyingine 6 barani ulaya ambazo zina maambukizi zaidi ya elfu moja.
Ufaransa
Georgia
Ugiriki
Italia
Urusi
Serbia
Na vifo vingi vilivyosababishwa na surua vimeripotiwa katika nchi zote hizo ,Serbia ikiwa inaongoza kwa idadi kubwa ya watu 14 kufariki.

Chanzo cha picha, WHO
________________________________________
Dalili za surua
Kuhisi baridi na kupiga chafya
Homa kali,uchovu,kukosa hamu ya kula na misuli kuuma
Macho kuwa na rangi nyekundu na majimaji kama unataka kulia
kuwa na rangi ya kijivu mdomoni
kuwa na vipele vyenye rangi nyekundu ambavyo vinaweza kusambaa kutoka kwenye kichwa,shingoni mpaka kwenye mwili wote.
________________________________________












