Kifo cha kasa Uchina: Mmoja wa kasa wanne wanaofahamika kuwa wakubwa wa Yangtze afariki akiwa na miaka 90

kasa wa kike wa Yangtze mwenye gamba laini akiwa katika mazingira yake ya kawaida ya maji ya matope katika hifadhi ya wanyama mwaka 2015

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kasa wa Yangtze mwenye gamba laini akigaagaa kwenye maji ya matope, anaweza kuwa na uzito wa kilo 90

Mmoja wa kasa wanaopatikana kwa nadra zaidi duniani wa Yangtze mwenye gamba laini amekufa nchini Uchina na kuwaacha wenzake watatu pekee wa kizazi hicho wanaofahamika.

Kasa huyo jike alikufa katika hifadhi ya wanyama iliyopo kusini mwa Uchina.

Wataalamu walikuwa wanajaribu kupandikizia mbegu za uzazi kwa kiumbe huyo kwa njia bandia , aliyekuwa na miaka zaidi ya 90, kwa mara ya tano , siku moja kabla ya kufa.

Kizazi cha kasa hawa kilitokomezwa kwa shughuli za uwindaji, uvuvi wa kupindukia na uharibifu wa makazi yao.

Kasa jike akifanyiwa mchakato wa kupandikizwa mbegu za uzazi kwa njia bandia mwaka 2015

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kasa huyo alifanyiwa majaribio kadhaa ya kupandikiziwa mbegu za uzazi kwa matumaini ya kuendeleza kizazi chake, lakini yote hayakufanikiwa

Kasa dume mmoja anakadiriwa kuwa na umri wa miaka zaidi ya 100 , amebakia katika hifadhi ya wanyama ya Uchina huku wengine wawili waliobaki wakiishi katika porini nchini Vietnam. Ugumu wa kuwakamata Kasa wa aina hii umefanya kazi ya kubaini jinsia yao

Wafanyakazi katika hifadhi hiyo ya kasa na wataalamu wa kimataifa walikuwa wamejaribu kupandikiza mbegu za uzazi kwa njia bandia kwa kasa huyo wa kike saa 24 kabla ya kufa Jumapili mchana.

Walisema hakupata matatizo yoyote kutokana na upasuaji na alikuwa ana afya nzuribaada ya upasuaji huo, lakini hali yake ikawa mbaya zaidi siku iliyofuatia.

Sababu ya kifo chake inachunguzwa na sehemu ya nyama ya mfuko wa mayai yake ya uzazu ilichukuliwa kwa ajili ya utafiti wa siku zijazo.

Kasa mkubwa dume wa Yangtze alipigwa picha akiwa amelala kwenye kipande cha plastiki

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kasa mkubwa dume wa Yangtze mwenye gamba laini kwa sasa ndiye aliyebakia pekee wa kizazi chake