Pete Buttigieg: Meya awafungisha ndoa wapenzi kabla ya upasuaji wa kujifungua

Meya wa South Bend Pete Buttigieg (katikati) akiwafungisha ndoa Mary na Gabe

Chanzo cha picha, Facebook/Pete Buttigieg

Maelezo ya picha, Meya Pete Buttigieg (katikati) akiwaf ungisha ndoa Mary na Gabe katika ofisi yake

Meya wa Marekani na mgombea wa kiti cha urais ajaye aliwafungisha ndoa wapenzi waliokuja dakika za mwisho tu kabla ya kuelekea hospitali kupata mtoto kwa njia ya upasuaji

Pete Buttigieg, ambaye ni meya wa jimbo la South Bend, Indiana, alisema kuwa wawili hao Mary and Gabe, walimkuta ndio amewasili ofisini majira ya saa mbili unusu na wakamuomba awafungishe ndoa kabla mtoto wao hajazaliwa.

Wafanyakazi wa ofisi ya Meya walikuwa ndio mashahidi na walitumia vipande vya vitambaa( riboni) kama pete kwa kuwa pete zao zilikuwa bado hazijatengenezwa

Baada ya kufunga ndoa yao Mary aliweza kufika hospitalini saa tatu asubuhi kama alivyoagizwa na daktari na kujifungua salama mtoto mchanga wa kike.

Mtoto Jade Katherine Jones amekuwa ''mkazi mpya kabisa'' wa South Bend ",Aliandiika Meya Buttigieg kwenye ukurasa wake wa Facebook.

"Ni nyakati kama hizi ambazo nitazikosa muda wangu wa umeya utakapokwisha ," aliandika alipotuma picha ya mtoto mchanga wa kike.

Mtoto mchanga aliyezaliwa Jade Katherine Jones

Chanzo cha picha, Facebook/Pete Buttigieg

Maelezo ya picha, "Karibu Jade,katika dunia hii isiyosadikia na nzuri !" Alisema meya Buttigieg

"Hongera kwa wazazi na wanandoa wapya , na karibu Jade, katika dunia hii isiyoyadikika na nzuri!"

Mwezi Januari , Meya Buttigieg, mwenye umri wa miaka 37, alitangaza nia yake ya kugombea urais katika uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2020 , alipojiunga miongozi mwa wagombea wa uteuzi wa chama cha Democratic - ambao tayari idadi yao imekuwa kubwa.

Ikiwa atateuliwa , Bwana Buttigieg atakuwa ni mtu wa kwanza aliyejitangaza wazi kuwa mpenzi wa jinsia moja kuwahi kuchaguliwa katika chama kikuu cha kisiasa