Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Pete Buttigieg: Meya awafungisha ndoa wapenzi kabla ya upasuaji wa kujifungua
Meya wa Marekani na mgombea wa kiti cha urais ajaye aliwafungisha ndoa wapenzi waliokuja dakika za mwisho tu kabla ya kuelekea hospitali kupata mtoto kwa njia ya upasuaji
Pete Buttigieg, ambaye ni meya wa jimbo la South Bend, Indiana, alisema kuwa wawili hao Mary and Gabe, walimkuta ndio amewasili ofisini majira ya saa mbili unusu na wakamuomba awafungishe ndoa kabla mtoto wao hajazaliwa.
Wafanyakazi wa ofisi ya Meya walikuwa ndio mashahidi na walitumia vipande vya vitambaa( riboni) kama pete kwa kuwa pete zao zilikuwa bado hazijatengenezwa
Baada ya kufunga ndoa yao Mary aliweza kufika hospitalini saa tatu asubuhi kama alivyoagizwa na daktari na kujifungua salama mtoto mchanga wa kike.
Mtoto Jade Katherine Jones amekuwa ''mkazi mpya kabisa'' wa South Bend ",Aliandiika Meya Buttigieg kwenye ukurasa wake wa Facebook.
"Ni nyakati kama hizi ambazo nitazikosa muda wangu wa umeya utakapokwisha ," aliandika alipotuma picha ya mtoto mchanga wa kike.
"Hongera kwa wazazi na wanandoa wapya , na karibu Jade, katika dunia hii isiyoyadikika na nzuri!"
Mwezi Januari , Meya Buttigieg, mwenye umri wa miaka 37, alitangaza nia yake ya kugombea urais katika uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2020 , alipojiunga miongozi mwa wagombea wa uteuzi wa chama cha Democratic - ambao tayari idadi yao imekuwa kubwa.
Ikiwa atateuliwa , Bwana Buttigieg atakuwa ni mtu wa kwanza aliyejitangaza wazi kuwa mpenzi wa jinsia moja kuwahi kuchaguliwa katika chama kikuu cha kisiasa