'Mtoto mchanga wa kiume mwenye mwili mdogo zaidi kuwahi kushuhudiwa aondoka hospitalini mjini Tokyo

Chanzo cha picha, Keio University Hospital
Mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa na uzito wa gramu 268 alipozaliwa ameruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali nchini Japan, na anaaminiwa kuwa ndiye mtoto wa kiume mwenye mwili mdogo duniani kuwahi kuruhusiwa kwenda nyumba akiwa mwenye afya.
Mtoto huyo alizaliwa kwa dharura kwa njia ya upasuaji mwezi Agosti , na wakati huo mwili wake haukuweza kujaa kwenye viganja.
Mtoto huyo alikuzwa chini ya uangalizi makini hadi aliporuhusiwa kwenda nyumbani wiki iliyopita , miezi miwili baada ya tarehe aliyotarajiwa kuzaliwa.
Alikuwa amekua na kuwa na uzito wa kilo 3.2 na kwa sasa ananyonya kama kawaida.
Alizaliwa katika wiki ya 24 ya ujauzito , na hivyo kulazimika kuendelea kuwa hospitalini kwa miezi mitano.
"Ninachoweza kusema tu kwamba nimefurahi kuwa amekuwa mkubwa hivi kwasababu kusema ukweli sikuwa na uhakika angeliweza kuishi ," alisema mama yake mtoto huyo wa kiumekwamu mujibu wa hospitali ya Chuo kikuu cha Keio.
Daktari Takeshi Arimitsu, aliyemtubu mtoto huyo wa kipekee , ameiambia BBC kuwa alikuwa mtoto mchanga mwenye mwili mdogo zaidi kuwahi kuruhusiwa kutoka hospitalini, kulingana na rekodi ya data za watoto wanaozaliw awakiwa na wenye mwili mdogo zaidi zinazohifadhiwa na Chuo kikuu cha Iowa.
Alisema alitaka kuonyesha kuwa " kuna uwezekano kwamba watoto wachanga wanaweza kuondoka hospitalini wakiwa na afya nzuri hata kama watazaliwa wakiwa na mwili mdogo".

Chanzo cha picha, Keio University Hospital
Rekodi ya mwisho ya mtoto mwenye uzito wa chini zaidi wa mwili ilikuwa ni ya mtoto wa kiume aliyezaliwa nchini Ujerumani akiwa na uzito wa mwili wa gramu 274. Mtoto mwingine aliyeweza kuishi ni wa kike aliyerekodiwa kwenye data hizo ni wa kike ambaye pia alizaliwa nchini Ujerumani mwaka 2015 akiripotiwa kuwa na uzito wa kilogramu 252.
Chuo kikuu cha Keio kilisema kiwango cha kuishi cha watoto wachanga wenye uzito mdogo wa mwili wa chini ya kilo moja ni cha asilimia 90% nchini Japan. lakini kwa wale wanaozaliwa wakiwa na uzito wa chini ya kilo, ni karibu asilimia 50%.
Miongoni mwa watoto wenye uzito wa chini zaidi wanaoweza kuishi ni wa kike kuliko wa kiume. Wataalamu wa tiba hawana uhakika ni kwa nini , lakini baadhi wanasema huenda inatokana na kwamba mapafu ya watoto wachanga wa kiume hukua pole pole.












