Kifo cha Stan Lee: Nyota wa filamu na mashabiki wake duniani wasifia ustadi wake

Stan Lee

Chanzo cha picha, PA

Muda wa kusoma: Dakika 4

Stan Lee, mwandishi mashuhuri wa Marekani na rais wa zamani wa kampuni ya vichekesho ya Marvel Comics amefariki dunia akiwa na miaka 95.

Mwaka 1961, Lee alibuni filamu nne bora za Marvel Comics, na kuzipatia majina maarufu ikiwemo Spider-Man NA The Incredible Hulk.

Mwandishi huyo mkongwe wa vitabu vya vichekesho alifariki katika kituo cha matibabu cha Cedars Sinai mjini Los Angeles, kwa mujibu wa wakili wa familia.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya burudani ya Pow inayomilikiwa na Lee! alimtaja kama "Baba wa mitindo ya pop" kwa kubuni "wahusika wanaofahamika kote duniani".

Mkurugenzi mkuu Shane Duffy alimkumbuka kama "mwanzilishi wa kweli ambaye hana mpinzani".

Mke wa Lee, Joan, alifariki mwaka 2017.

Akizungumza na mtandao wa TMZ unaoangazia habari za nyota mashuhuri, binti yake JC Lee alisema mbaba yake alikuwa ''mtu mashuhuri na mwenye heshima".

Aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba : "katika utendakazi wake alihisi kuwa na wajibu mkubwa kwa mashabiki wake."

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, miaka ya hivi karibuni Lee, amekuwa akiiugua mara kwa mara.

Stan Lee

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Stan Lee au Stan Lieberman alizaliwa mwaka 1922

Lee alifahamika kwa kutengeneza filamu ya maarufu alipokuwa na kampuni ya filamu ya Marvel, japo aliachana na kampuni hiyo mwaka 1972.

Siku ya Jumapili, ambayo siku ya kuwatambua mashujaa , ukurasa wake rasmi wa Facebook uliweka picha za Lee akiwa jeshini, na kuandika kwa utani kwamba alikuwa mtunzi wa michezo tangu wakati wa vya pili vya Dunia.

Presentational white space

Stan Lee ni nani?

Lee alizaliwa mwaka 1922. Wazazi wake walikuwa wahamiaji wa kiyahudi kutoka Romania.

Alianza kufanya kazi katika sehemu ya kampuni ya machapisho ambayo hatimaye itabadilika na kufahamika kuwa Marvel Comics - na baadaye kuwa mhariri wa wasanii akiwa na miaka 18.

Alianza kufanya kazi kwenye sehemu ya Jumuia ya Machapisho ya wakati - kampuni ambayo hatimaye ilibadilika kuwa Marvel Comics - na kuwa mhariri wa wasanii akiwa na umri wa miaka 18.

Kwa miaka kadhaa Lee alijikita zaidi katika uandishi wahadithi za uhalifu, hadithi za kuogofya na masuala mengine ya kijamii ili kuwavutia wasomaji wadogo.

Alipotimiza miaka 40 aliachana na vichekesho lakini mke wake alimshauri kuuni wahusika ambao angelipenda wahusishwe nae

Mwaka 1961, Lee na mchoraji Jack Kirby waliungana kubuni wahusika wanne maarufu sana- wahusika hao walikua tabia binafsi na matatizo yaliyohusiana

Timely Publications ilibadilishwa jina kuwa Marvel na ni hapo safari ya vitabu vya kichekesho ilianza.

Stan Lee shakes Chadwick Boseman's hand

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Stan Lee akimsalimia muigizaji Chadwick Boseman

Wakati huo wahusika wengi wa kampuni ya filamu ya Marvel walikuwa wameanza kutambulika.

Kwa mfano, Black Panther ndiye alikuwa shujaa wa kwanza mashuhuri mweusi kushirikishwa katika vichekesho nchini Marekani.

Wahusika wengine waliyobuniwa ni pamoja na Silver Surfer, the X-Men, Iron Man na Doctor Strange.

Lee pia alitambuliwa kwa kuwapatia wachoraji haki miliki. Kirby, Frank Miller, John Romita na wengine walipata nafasi ya kutambulisha vipaji vyao na kupata umaarufu mkubwa

Katika miaka ya umaarufu wake, Marvel iliuza nakala milioni 50 kwa mwaka.

Hadi alipostaafu kuhariri uandishi wake mwaka1971, Lee alikuwa ameandika nakala zote za utambulisho wa vitabu vya Marvel.

Kifo chake kimepokelewaje?

Bob Iger, mwenyekiti wa kampuni ya Walt Disney,ambayo ilinunua vitabu vya vichekesho vya kampuni ya Marvel kwa kima cha dola bilioni 4 mwaka 2009 alimtaja Lee kama "Shujaa mtajika"

Nyota wa filamu na mashabiki wake wamekuwa wakielezea katika mitandao ya kijamii jinsi kazi ya Lee ilivyowagusa

Hugh Jackman, alifahamika kama Wolverine katika filamu ya X-Men, alimtaja Lee kama "Mwanzilishi wa ulimwengu wa superhero".

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Presentational white space

Evangeline Lilly, ambaye aliyeangaziwa kama mpenzi wa superhero wa Ant Man, Wasp, pia alitoa pole zak kwenye Twitter.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Presentational white space

Chris Evans, nyota wa filamu ya Captain America, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akisema : ''Kwa miaka mingi Lee aliwaburudisha vijana na wazee kwa kuwahimiza wajiamini, wawe na motisha, kujenga urafiki na kuwa na furaha. Alikuwa na upendo na fadhila zake zitaacha alama katika mioyo na maisha ya watu wengi sana.''

Astrophysicist Neil deGrasse Tyson praised Lee for creating a universe full of "scientifically literate superheroes".

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Presentational white space

Tom Hardy, ambaye ni mmoja wa wahusika katika filamu ya hivi karibuni inayoangazia mhusika Venom, wa kampuni ya vichekesho ya Marvel aliweka picha za Lee akiwa katika ubora wake, kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe

Presentational white space
line