Maisha yangu ya jinsia mbili: Sasa nina uume mpya nina matumaini ya kupata mpenzi

Anick 25 October 2018
Maelezo ya picha, Anick 25 Oktoba 2018

Mapema mwaka huu Anick mwenye miaka 23 ambaye alizaliwa akiwa na viungo viwili, alikuwa akijiandaa kwa upasuaji wa mwisho ambao utampa uume ulio kamili.

"Siwezi kukumbuka ni mara ngapi madaktari na wauguzi wameona uchi wangu kwa miaka kadhaa," anasema Anick. "Katika miaka michache iliyopita pekeer imekuwa zaidi ya mara 100."

Anick alizaliwa akiwa na viungo ambavyo havikufanana na vya mvulana wala msichana. Madaktarai waliwaambia wazazi wangu: Mtoto huyu ni kama mvulana, lakini bado hatuna uhakika," anasema.

Alikuwa na korodani lakini zilikuwa eneo tofauti, kwa hivyo upasuaji wake wa kwanza kuzihamisha ulifanyika akiwa na umri wa miezi minne.

Miaka yake ya utotoni, watu walikuwa wakimuambia Anick kuwa hakuwa kama watoto wengine.

Anick as a small child
Maelezo ya picha, Anick akiwa mtoto

"Nilijua kukulikuwa na kitu fulani tofauti kwangu, lakini sikuelewa ni kipi," anasema.

"Nilijua kuwa wazazi wangu walinipenda, lakini wakati huo pia walikuwa wakinipeleka hospitalini baada ya kila miezi sita, ambapo madaktari walitumia majina kuwa "kisicho cha kawaida" wakati wakizungumza kunihusu."

Alikuwa na wakati mgumu kuwa na marafiki shuleni, alijaribua kujizuia kupumua ili afe.

Baada ya kujaribu kujiua akiwa na umri miaka 14 alipewa ushauri lakini hakuweza kufikia kifichua kwa mtoa ushauri kiini hasa cha matatizo yake.

"Sikutaka yeyote ajue ambaye hakuhitaji kujua, anasema.

Anick as a teenager
Maelezo ya picha, Anick akiwa kijana

"Nilifikiri hakuna mtu alijua kile kilichokuwa tofauti kwangu, kuwa nilikuwa mtu pekee duniani, kisa kama miujiza hivi, anasema.

Ni miaka mitano iliyopita, akiwa na miaka 18 ndipo alifahamu kuwa kulikuwa na jina kwa tatizo hilo na sababu ya upasuaji huo wote na matibabu ya homoni: alikuwa na viungo wa "kike na kiume".

Ufahamu huu na kujua kuwa kuna watu wengine huko nje walio kama mimi, ilichangia mabadiliko makubwa kwangu, anasema: "mara nikafahamu kuwa nisihisi haya kuhusu jinsi nilivyo ni vile nilvyozaliwa."

Madaktari pia walikuwa wamemuambia Anick kuwa ataanza kufanyiwa upasuaji kubuni uume mpya wakati alifika umri wa miaka 18 kwa ruhusa yake mwenyewe. Walimuambia asiharakishe maamuzi na kuamua tu wakati atahisi kufanya hivyo.

Kugundua zaidi

Miaka mitatu baadaye mwaka 2016, Anick aliamua kuwa alikuwa tayari.

"Huo ni wakati nilipata kuelewa zaidi," anasema. Nilihitaji kuanza kuwaambia watu, nilihitaji kusema ukweli. Ningepitia upasuaji mkubwa.

Alianza kuwaambia binamu zake, shangazi na kushangazwa kuona kuwa hawakushtushwa na hilo.

"Sikujua watu wanaweza kuwa wanakubali kitu ambacho nimekuwa nikikificha kwa muda mrefu," alisema.

Upasujia wa mwisho ulipangwa Juni 2018, na kumpa Anick kujiamini kuwa baada ya muda usiokuwa mrefu atakuwa na uhakika kuwa ataanza kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Anick on Pride day 2018
Maelezo ya picha, Anick siku ya mkutano wa watu wenye jinsia mbili mwaka 2018

Ni Februari 2018 na Anick yuko njiani kwenda mkutano wa shirika linalojulikana kama Organisation Intersex International (OII) huko Copenhagen. Ana furaha sana lakini pia ana uoga kidogo.

Wajumbe kama Anick wanawasili kutoka sehemu tofauti za dunia kuzungumzia masuala yanayohusu kubadilishana maisha yao.

"Ni kitu ambacho kukizungumzia ni vigumu, lakini baada ya saa kadhaa tulianza kuzungumza kuhusu viungo vyetu," Anick anasema.

Jinsia mbili

Ni neno linalotumiwa kuwaelezea watu wanaozaliwa na matatizo ya kibaolojia katika jinsia zao ambazo haziwezi kutajwa kuwa upande wa kike au kiume.

Kuna aina tofauti inayohusu viungo nyeti, ovari, korodani na homoni.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa karibu asilimia 1.7 ya watu wako hali hiyo duniani.

Anafurahia hisia za kuwa karibu na watu ambao haitaji kujieleza. Anajiuliza ikiwa hivi ndivyo ilivyo mtu anavyohisi akiwa hali ya kawaida.

Lakini pia anashangazwa kugundua kuwa anahisi kutengwa kidogo, kwa sababu watu wengine wana mawazo tofauti na yake.

"Niko na watu ambao sasa wanaweza kuelewa vile ninahisi, lakini wakati huo huo hawajapitia maisha kama yangu," anasema.

Anick
Maelezo ya picha, Anick

Baadaye Anick anawasiliana kwa njia wa Skype na mwananarakakati wa watu walio na viungo vya jinsia mbili. Kama Anick, Pidgeon alizaliwa bila uume wale kiungo cha kike - lakini kwa Pidgeon madaktari waliamua kumwekea sehemu ya kike badala ua uume.

Pidgeon alilewa kama msichana. Wakiwa chuo kikuu ndipo walikuja kugundua kuhusu upasuaji waliofanyiwa kama mtoto na kufahamu kuwa walikuwa na viungo vya jinsia mbili.

Pidgeon sasa anataja upasuajia huu kama usio wa manaa, akidai kuwa kutumia upasuaji kubadilsiha hali ya kiafya ya mtu aliye na viungo viwili ni ukiukaji wa haki za bindamnu.

"Ninaweza kusema kuwa unastahili kumruhusu mtoto wako akue kama mtu mwenye viungo wa kike na kiume na uwaache siku moja wafanye uamuzi wa miili yao." Pidgeon anasema.

"Lazima tuwashinikize madakatari waache kuwafanyia upasuaji watoto na badala yake wawafanyike upasuaji watu wazima walio na viungo vya jinsia mbili wanaohitaji."

Baada wa kuhudhuria mkutano wa OII na kuongea na Pidgeon, Anick pia anafikiri kuwa upasuaji mwingi aliofanyiwa akiwa mtoto ulikuwa ni wa "mapambo."

Amekuwa akifikiria sana kuhusu ikiwa anahitaji upasuaji ambao anapangiwa kufanyiwa au ni kile watu wamesababisha ahisi ni kuwa anakihitaji ili apate kuishi maisha ya raha.

Lakini amemua kuendelea na upasuaji huo.

Anick's arms, including the left arm from which skin was taken to form his penis
Maelezo ya picha, Mikoni ya Anick akionyesha eneo la mkono ambalo alitolewa ngozi

Sasa ni Juni 2018 na Anick anataka kwenda hospitalini.

Mwaka mmoja uliopita madaktari walitoa ngozi kutoka sehemu ya mkono wake wa kushoto. Imechukua mwaka mmoja kuweza kuitumia kwenda haja ndogo kwa njia nzuri.

Anabadilishwa mavazi na kuvalishwa yale ya kwenda chumba cha upasuaji hali ambayo ameizoea kwa muda mrefu.

Leo hii kifaa kitawekwa kwenye uume wake Anick ambacho atakihitaji kusukuma kama angehitaji kufanya mapenzi.

Anick in hospital in 2018
Maelezo ya picha, Anick akiwa hospitalini mwaka 2018

"Kila kitu katika maisha yanga kitakuwa tofauti, Anick anasema. Hatimaye nitakuwa na kitu kinakaribiana na kile watu wengine wako nacho, na labda nitahisi vile watu wengine uhisi wakiwa umri wangu. Nimejitenga sana kutoka kwa mahusiano kutokana na kukosa kuuamini mwili wangu na kujichukia.

"Upasuaji umeenda vizuri." Anick anasema kuwa mambo huko chini yako tofauti sasa. Hajui itamchukua muda gani kuweza kuzoea.

Wakati dawa ya kupunguza machungu inapokaribia kuisha anajiandaa tayari kwenda nyumbani ambapo wazazi wake watamuuguza.

"Kila mara watu hunitembelea na mimi hujaribu kuwa na furaha, hata wakati ule sina furaha," anasema.

Mwezi mmoja umepita. Tangu aondoke hospitalini Anick amekuwa na machungu mengi. Haukuwai kuhisi uchungu kama huo awali licha ya kufanyiwa upasuaji mara kadhaa,

Kumekuwa na matatizo kadhaa na kwa mwezi uliopita amekuwa akirudi hospitalini.

Lakini Anick anajaribu kuvumilia.

"Leo ni siku ya kihistoria, anasema, "Ndiyo mara ya kwanza watu wenye viungo vyote viwili wanakusanyika na kutembea mjini London."

Anick at Pride
Maelezo ya picha, Anick akiwa kwenye mkutano

"Wakati kama huu mwaka uliopita, sikuwa nimekutana na mtu mwingine mwenye jinsia mbili," Anick anasema. Nilinda kwenye mikusanyiko peke yangu kumtafuta mtu mwenye jinsia mbili lakini sikumpata yeyote. Kwa sasa mwaka huu ninaenda na kundi zima la watu wenye jinsia mbili.

Hataacha kutabasamu.

"Siwezi kufikiri kuhusu ni kiwango gani maisha yangu yamebadilika tangu mwaka uliopita," anasema

Anick in hospital
Maelezo ya picha, Anick akiwa hospitalini

Sasa ni Agosti mwaka 2018. Anick anastahili kufanyiwa upasuaji mwingine kurekebisha mambao ambayo hayakwenda sawa. Kifaa kilichowekwa ndani ya uume wake kimejifunga kwenye moja ya korodani zake na kumsababishia machungu mengi.

Anahisi uchungu na anahitaji awe muangalifu zaidi kuzuia maambukizi lakini ana matumaini kuwa huenda sasa asifanyiwe upasuaji kwa muda wa miaka mitano au saba.

Mara nilipofanyiwa upasuaji, niliuona mwili wangu kuwa ulio tofauti kabisa, anasema.

Anick in hospital
Maelezo ya picha, Anick akiwa hospitalini

Ameanza kuwa na uhusiano wa karibu na wazazi wake pia.

"Nilikua nikihisi kuwa hawakufanya ya kutosha na hawakujua kile kilikuwa kinaendelea," anasema. Lakini sikufahamu lile giza na usumbufu waliokuwa nao.

Kwa jumla anasema, kufanyiwa upasuaji huo imempa furaha zaidi. Amejisajili kwenye mitandao ya kutafuta wapenzi na tayari amekutana na wapenzi wachache.

"Ninajaribu kuelewa hali ilivyo huko nje. Moja wa mikutano yangu na msichana haukwenda vyema kwa sababu aliniambia kuwa sikuwa mwanamume kamilia.

Kisha nikakutana na mwanamume na sikuhisi chochote, kwa hivyo nimekumbwa na matatizo ya kawaida ambayo watu hupitia kwenye mapenzi - ni hisia nzuri."

Na ana matumaini kuwa kuzungumzia kila ambacho kilikuwa siri yake kuu katika maisha yake kitasaidia watu wengine walio katika hali kama hizo.