Maelfu wakumbwa na changomoto za usafiri huku sheria za barabarani zikitekelezwa Kenya

Abiria wakisubiri mabasi kituo cha Kencom Nairobi
Maelezo ya picha, Abiria wakisubiri mabasi kituo cha Kencom Nairobi

Wakenya wengi kote nchini waemkia changamoto kubwa katika usafiri wa umma baada ya wamiliki wa magari ya usafiri kuandoa magari yao barabarani kupinga hatua ya serikali kurejesha sheria za barabarani maarufu kama "sheria za Michuki."

Kuanzia mapema Jumatatu kulikuwa na magari machache kwenye barabara za mji wa Nairobi ambayo yaliongeza nauli, hali iliyolazimu mamia ya wasafiri kutembea kwenda maeneo tofauti.

Wengi walitumia bodaboda kusafiri
Maelezo ya picha, Wengi walitumia bodaboda kusafri

Magari machache yaliyokuwa barabarani yaliongeza nauli hadi zaidi ya mara dufu.

Kati ya sheria ambazo magari ya uchukuzi wa abiria yanastahili kutekeleza ni pamoja na:

  • Kuweka mikanda kwenye viti.
  • Kuweka vidhibiti mwendo na kupaka rangi ya mstari wa manjano kwa magari.
  • Dereva na kondakta kuvaa sare rasmi na kuwa na vitambulisho.
  • Picha ya dereva kuwekwa kwenye kioo cha mbele cha gari.
  • Mabasi ya masafa marefu kuwa na mipangilio ya safari na madereva wawili.
  • Dereva na Kondakta kulipwa mshahara wa kile mwezi na sio wa kila siku jinsi ilivyo sasa.

Wakati huo huo waziri wa uchukuzi James Macharia ameliagiza shirika la Reli chini Kenya kuongeza safari zake kwenda mitaa yote ambayo linatao huduma, kama njia ya kuwapunguzia matatizo ya usafiri wakaazi wa Nairobi.

Abiria wakisubiri mabasi kituo cha Kencom Nairobi
Maelezo ya picha, Abiria wakisubiri mabasi kituo cha Kencom Nairobi

Kwenye taarifa iliyotolewa mapema leo Jumatatu waziri aliamrisha Shirika la Reli kupunguza nauli kwa asilimia 10 hadi pale huduma za kawaida za usafiri zitakaporejea.

"Wakati serikali inaendelea kutekeleza sheria za barabarani kuimarisha usalama wa barabarani na kuboresha sekta hiyo, umma unaombwa kuunga mkono jitihada za serikali ili kuhakikisha kuwa kuna manufaa ya muda mrefu kwa wakenya wote," Bw Macharia alisema.