Kwa Picha: Tembo aliyekwama matopeni alivyookolewa Kenya
Tembo huyu alikwama kwenye matope katika eneo la vilima vya Chyulu katika kaunti ya Makueni mashariki mwa jiji la Nairobi, alijaribu kujikwamua akashindwa.
Alikwama kwa siku tatu topeni.

Chanzo cha picha, KWS
Lakini wahenga walisema Ndovu hashindwi na mkonga wake. Ndovu aliyekomaa huwa na uzani wa kati ya tani 2 na tani 7.
Ndovu mwenyewe aliposhindwa kujinasua, jukumu liliwaangukia maafisa wa Shirika la Huduma kwa Wanyama pori Kenya (KWS) ambao walishirikiana na maafisa wa wakfu wa David Sheldrick Wildlife Trust wa wakfu wa Big Life kwa ushirikiano na wakazi wa eneo hilo.

Chanzo cha picha, KWS

Chanzo cha picha, KWS
Kazi ya kumnasua ilifanywa ngumu kutokana na eneo hilo la Kiboko karibu na Vilima vya Chyulu kuwa na matope.
Magari mara nyingi yalikuwa yanakwama kwenye matope njiani yakisafirisha maafisa wa uokoaji na mengine kwenye tope yakijaribu kumvuta tembo huyo.

Chanzo cha picha, KWS
Kutokana na kujaribu kwa muda mrefu kujinasua bila kufua dafu, tembo huyo alikuwa ameishiwa na nguvu hata za kusimama.

Chanzo cha picha, KWS

Chanzo cha picha, KWS
Baada ya kuokolewa, iliwalazimu maafisa kumdunga sindano zenye dawa na virutubisho na mwishowe akaweza kusimama bila kusaidiwa.
Alikuwa amenasuliwa saa moja jioni usiku wa Jumatatu na kufikia Jumanne asubuhi nguvu zake zikawa zimerejea na akaondoka na kwenda zake msituni.

Chanzo cha picha, KWS
Unaweza kusoma pia:
Picha zote kwa hisani ya Shirika la Huduma kwa Wanyamapori Kenya (KWS)













