Upigaji kura wakamilika Angola

Viongozi mbalimbali wakipiga kura
Maelezo ya picha, Viongozi mbalimbali wakipiga kura

Zoezi la upigaji kura limekamilika nchini Angola ambapo inatarajiwa kuwa na Rais mpya baada ya José Eduardo Dos Santos kukaa madarakani kwa karibia miongo minne.

Baadhi ya sehemu za vijijini ambapo upigaji kura ulichelewa, ziliruhusiwa pia kuongeza muda wa kumaliza.

Kulikuwa na msisimko mkubwa wakati wa kampeni
Maelezo ya picha, Kulikuwa na msisimko mkubwa wakati wa kampeni

Waziri wa zamani wa ulinzi João Lourenço anatarajiwa kushinda,lakini Dos Santos atasalia kama kiongozi mkuu wa chama cha MPLA.

Chama kikuu cha upinzani nchini Angola ni UNITA.