Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Upigaji kura wakamilika Angola
Zoezi la upigaji kura limekamilika nchini Angola ambapo inatarajiwa kuwa na Rais mpya baada ya José Eduardo Dos Santos kukaa madarakani kwa karibia miongo minne.
Baadhi ya sehemu za vijijini ambapo upigaji kura ulichelewa, ziliruhusiwa pia kuongeza muda wa kumaliza.
Waziri wa zamani wa ulinzi João Lourenço anatarajiwa kushinda,lakini Dos Santos atasalia kama kiongozi mkuu wa chama cha MPLA.
Chama kikuu cha upinzani nchini Angola ni UNITA.