Watu watatu wauawa kwa kupigwa risasi Marekani

Polisi wanasema ulinzi umeimarishwa zaidi kwa sasa
Maelezo ya picha, Polisi wanasema ulinzi umeimarishwa zaidi kwa sasa

Polisi katika mji wa San Francisco wamesema watu watatu wameuawa katika shambulio la kufyatua risasi.

Mfyatuaji ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kampuni moja pia alifariki.

Polisi wanasema alijifyatulia risasi mwenyewe wakati wakijaribu kumkamata.

Watu wakiwa wanaondolewa katika eneo hilo
Maelezo ya picha, Watu wakiwa wanaondolewa katika eneo hilo

Watu wengine wawili walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Msemaji wa jeshi la polisi amesema kuwa tukio hilo halina uhusiano na ugaidi.