Mashambulizi ya Urusi yawatimua IS kutoka Palmyra

Wanajeshi wa Syria wakipita Palmyra mwezi Aprili

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Syria wakipita Palmyra mwezi Aprili

Wapiganaji kutoka kundi la Islamic State wamelazimishwa kuondoka kati kati mwa mji wa Palmyra saa chache baada ya jaribio lao la kuuteka mji huo

Mashambulizi ya ndege za Urusi yaliwalazimu wanamgambo hao kurudi nyuma.

Islamic State walikuwa wamedhibiti mji wa kitamadudi wa Palmyra kutoka mwezi Mei mwaka 2015 hadi wapolitimuliwa mwezi Machi.

Sasa shirika la kuangalia haki za binadamu linasema kuwa mashambuli makubwa ya ndege za Urusi yaliwalazimu Islamic State kuondoka mjini humo

Maelezo ya video, Parts of the ancient city of Palmyra were reduced to rubble by the jihadists

Mji wa Palmyra unaonekana kuwa muhimu kwa kundi la Islamic State kufuatia kukaribiana kwa na maneo yaliyo na mafuta.

Islamic State iliharibu sehemu za kitamaduni za mji huo na kumkata kichwa mkurugenzi wa maeneo hayo ya kale muda wa miezi 10 waliodhibiti Palmyra.

Maelfu ya raia wanakimbia kutoka maeneo yanayodhibitwa na waasi mashariki mwa Aleppo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Maelfu ya raia wanakimbia kutoka maeneo yanayodhibitwa na waasi mashariki mwa Aleppo.

Vikosi vya waasi jana Jumamosi vilisema kuwa vilikuwa vimezuia vikosi vya serikali katika maeneo wanayoyadhibiti mjini Aleppo.

Kamanda mmoja wa waasi alieleza sababu ya vikosi vya serikali kupunguza kasi akisema kuwa wanajeshi wengine wamepelekwa mjini Palmyra.