Wanamgambo wa serikali, wasaka IS Sirte, Libya

Wanamgambo wanaounga mkono serikali, Libya

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wanamgambo wanaounga mkono serikali, Libya

Wanamgambo waliowatiifu kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya wanasema wanawasaka wapiganaji wa kundi la Islamic State katika mji wa Sirte.

Baada ya miezi saba ya mapigano. Majeshi ya Libya wamekuwa wakipambana kuelekea wilaya ya al-Giza al Bahriya, eneo pekee la mjini ambalo mpaka sasa linadhibitiwa na wapiganaji wa IS.

Ingawa, serikali imeyarudisha majengo yaliyochukuliwa, maeneo hayo bado hayako na usalama karibu.

Maafisa wa jeshi wamesema baadhi ya wapiganaji hao wenye msimamo mkali wametoroka baada ya kuzingirwa.

Mwaka uliopita kundi hilo la IS waliigeuza Sirte kuwa ngome yao.