Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Mo Salah na Vinicius Jr kujiunga na Ligi ya Saudia?

Mo Salah na Vinicius Jr

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Mshambuliaji wa Liverpool na na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, 33, na Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Vinicius Jr, 25, wanatarajiwa kuwa walengwa wakuu Ligi Kuu ya Saudia msimu huu. (Telegraph - usajili unahitajika)

Wadadisi wa Saudi Pro League wanaamini Salah ataondoka Liverpool msimu huu wa joto. (i Paper - usajili unahitajika)

Klabu ya Inter Milan inavutiwa na kipa wa Tottenham Muitaliano Guglielmo Vicario, 29, inapojiandaa kuziba pengo lililoachwa na mchezaji wa kimataifa wa Uswizi Yann Sommer, 37. (Gazzetta - kwa Kiitaliano).

Klabu ya Crystal Palace imefanya mazungumzo na Wolves kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Norway Jorgen Strand Larsen, 25. (Talksport)

Manchester United iko tayari kujadiliana na kiungo wa kati wa England Kobbie Mainoo, 20. kuhusu kandarasi mpya (Sky Sports)

Chelsea inafikiria kumsajili kwa mkopo kiungo wa Brazil Douglas Luiz, 27, ambaye yuko Nottingham Forest kwa mkopo kutoka Juventus, kwa msimu uliosalia. (Athletic - usajili unahitajika)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Leeds na Sunderland huenda zikamkosa mshambuliaji wa Norwich City Josh Sargent. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani mwenye umri wa miaka 25 ana nia ya kurejea Ligi Kuu ya Soka huku Toronto FC. (Teamtalk)

Arsenal inamuwania beki Iago Machado mwenye umri wa miaka 16 kutoka Corinthians ya Brazil. (Globo - kwa Kireno)

Roma na vilabu vingine kadhaa bado viko mbioni kusaka saini ya mshambuliaji wa wa Manchester United na Uholanzi Joshua Zirkzee, 24. (Florian Plettenberg).