Afcon 2025: Cha kujifunza kupitia changamoto na mafanikio

ll

Chanzo cha picha, Getty Images/Reuters

    • Author, Rob Stevens
    • Nafasi, BBC Sport Africa
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) la mwaka 2025 litakumbukwa kwa jinsi lilivyomalizika.

Kulikuwa na matukio ya vurugu katika fainali hasa dakika za mwishoni, pale Morocco ilipopewa penalti dhidi ya Senegal na kusababisha mchezo kusimama kwa zaidi ya dakika 16 kabla ya Brahim Diaz kukosa penalti hiyo.

Kocha wa Atlas Lions, Walid Regragui, amelaani tukio la Senegal kutoka uwanjani na kusema ni la ‘aibu’ na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) bado halijatoa adhabu yoyote.

Mbali na matukio hayo, kuna mambo mengine mazuri. BBC Sport Africa inakueleza mambo ya kujifunza kutokana na mashindano hayo nchini Morocco.

Miundombinu mizuri

A colourful graphic is shown on the exterior of the Prince Moulay Abdellah Stadium in Rabat

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, nchini Morocco.

Hakuna shaka kwamba Morocco imejenga miundombinu mizuri, vifaa na viwanja bora, huku Uwanja wa Prince Moulay Abdellah katika mji mkuu ukiwa mfano bora.

Kuandaa mashindano hayo ni maandalizi ya kuandaa Kombe la Dunia la Fifa la 2030 kwa kushirikiana na Uhispania na Ureno.

Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini imefaidika na uwekezaji mkubwa katika miaka ya hivi karibuni chini ya Mfalme Mohammed VI, ambaye amesema miundombinu ya nchi hiyo ni ya “kiwango cha dunia."

Viwanja vilikuwa bora, hata wakati wa mvua.

"Tunajivunia sana teknolojia yetu," Omar Khyari kutoka Shirikisho la Soka la Morocco alIiambia BBC Sport Africa.

"Tunafuraha sana kwa sababu tumeuonyesha ulimwengu kwamba Afrika inaweza kufanya vizuri zaidi kuliko nchi zingine."

Waandishi wa habari kutoka Afrika Mashariki walifurahishwa na kile walichokiona, lakini kuna swali ikiwa waandaaji wa mashindano yajayo Kenya, Tanzania na Uganda wataweza kuwa na miundombinu mizuri kama hiyo.

Rais wa shirikisho la soka la Kenya Hussein Mohammed alikubali kwamba Morocco “iko mbali” lakini "hatua muhimu" zinachukuliwa ili kuboresha miundombinu iliyopo kabla ya mwaka 2027.

Tarehe za fainali hizo bado hazijatangazwa na Caf.

Mapato yaongezeka

Confederation of African Football president Patrice Motsepe holds the Africa Cup of Nations trophy while he walks alongside Fifa president Gianni Infantino

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Patrice Motsepe akiwa ameshikilia kombe la Kombe la Mataifa ya Afrika huku akitembea na rais wa Fifa Gianni Infantino

Caf inasema mapato yaliyotokana na Afcon yameongezeka kwa 90%, huku mapato kutokana na tiketi yakiongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka dola milioni 11 katika mashindano ya 2023 nchini Ivory Coast hadi milioni 55 nchini Morocco.

Pia idadi ya wadhamini na washirika imeongezeka hadi 23, na umaarufu wa mashindano ukiongezeka kutokana na mitandao ya kijamii.

Licha ya faida kuongezeka, watu watajiuliza kwa nini Caf imeamua mashindano ya Afcon yawe kila baada ya miaka minne badala ya kila miaka miwili kuanzia 2028.

Waamuzi walaumiwa

Referee Jean-Jacques Ndala points his right arm forward as he awards a penalty in the Africa Cup of Nations final. Out of focus in the background Sadio Mane can be seen with a wry grin on his face in t

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uamuzi wa Jean-Jacques Ndala wa kuipa Morocco penalti dhidi ya Senegal ulizua utata
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa upande mwingine, maamuzi ya waamuzi yametiliwa shaka mara kwa mara.

Kabla ya nusu fainali dhidi ya Nigeria, kocha wa Morocco Regragui alikosoa madai kuwa waamuzi wanaipendelea timu mwenyeji.

"Mimi hutazama mechi nyingi na utata hutokea kila mahali, iwe barani Afrika au Ulaya," amesema.

Mfano katika fainali hii, mechi ambayo mwamuzi Jean-Jacques Ndala aliiongoza vyema hadi muda wa mapumziko lakini kipindi cha pili mambo yaliharibika.

Uamuzi wa raia huyo wa Congo wa kuamua ni faulu kabla ya Senegal kutia mpira kwenye wavu. Aliamua kuwa ni mchezo mbaya dhidi ya Achraf Hakimi wa Morocco katika dakika ya pili kati ya dakika nane zilizoongezwa. Uamuzi huo ulileta hisia ya ukosefu wa haki na kuongezeka hisia hiyo baada ya Morocco kupewa penalti dakika sita baadaye.

Matumizi ya VAR yamerudisha nyuma mambo, ukilinganisha na maamuzi yasiyo na dosari katika AFCON ya 2023.

Kulikuwa na matukio yenye utata ya mpira kushikwa kwa mkono na penalti.

Usalama

Security personnel block angry fans over a penalty decision against Senegal during the Africa Cup of Nations final

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki wa Senegal walizozana na maafisa wa usalama baada ya Morocco kupewa penalti katika muda wa ziada wa kipindi cha pili

Shirikisho la soka la Senegal (FSF) liliibua wasiwasi kuhusu ukosefu wa usalama wakati kikosi chao kilipofika kwenye treni jijini Rabat kabla ya fainali, na kusababisha wachezaji kuzongwa na kundi la watu kwenye kituo hicho.

Kisha kulitokea matukio ndani ya uwanja huku mashabiki wa Teranga Lions wakikabiliana na maafisa wa usalama baada ya penalti yenye utata ya Morocco.

BBC Sport Africa ilishuhudia matukio mengine ya mashabiki nje ya viwanja wakipigana au kusukumana kwenye nafasi finyu.

Masuala ya usalama sio tatizo la Afrika pekee, matukio kama hayo yalitokea wakati wa Ligi ya Mabingwa ya Euro 2020 na 2022 za Uefa.

Kabla ya mechi hiyo, FSF ililalamika kuhusu kupokea tiketi chini ya 4,000 kwa ajili ya fainali ambayo ilifanyika katika uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 69,500.

Pia wachezaji wa mpira wa Morocco walijaribu kulipora taulo la kipa wa Senegal, Edouard Mendy kutoka kwa msaidizi wake aliyekuwa amesimama nyuma ya lango.

Video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinawaonyesha mashabiki wa Morocco wakishangilia taulo la kipa wa Nigeria Stanley Nwabali likiibiwa mara mbili wakati wa nusu fainali dhidi ya taifa mwenyeji.