Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii (18.08.2022)

Casemiro

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United hawana uwezekano wa kuwasajili Casemiro na Frenkie de Jong katika dirisha moja la usajili, kulingana na ripoti. Wachezaji hawa wa Real Madrid na Barcelona wanalengwa na Erik ten Hag.

Ni wazi kwamba Mashetani Wekundu wanahitaji kuongezewa nguvu baada ya kuvumilia mwanzo mbaya wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England.

Manchester United, hadi hivi majuzi, walikuwa tayari kuweka nguvu zao zote ili kumpata De Jong. Lakini huku dili la nyota huyo wa Barcelona likionekana kuwa gumu. United wameweka nia yao ya kumsajili Casemiro kutoka Real Madrid. 

Sky Sports Deutschland inaripoti kwamba kiungo Naby Keita 'hana furaha' na anaweza kuondoka Liverpool msimu huu wa joto ingawa haijafahamika ataelekea timu gani.

Keita alikuwa kwenye benchi katika mchezo dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumatatu, huku akioneka kutokua chaguo la kwanza la Klopp.

Hata hivyo Liverpool imesema kwamba haipo tiyari kumuachilia kiungo huyo wa kimataifa wa Mali.

Naby Keita

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wanatarajiwa kutuma ofa rasmi kwa nyota wa Leicester City, Youri Tielemans kabla ya mwisho wa dirisha baadaye mwezi huu.

Mbelgiji huyo amekuwa akitajwa kuhamia Arsenal majira ya joto lakini The Gunners wamekuwa wakionekana kusita sita kutoa ofa rasmi.

Hata hivyo Leicester imesema itaikubali ofa ya Arsenal iwapo itakua ya kuridhisha.

Youri Tielemans

Chanzo cha picha, Getty Images

Pierre-Emerick Aubameyang

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea wameweka wazi kwamba watakua na uwezo wa kumchukua mshambuliaji wa Barcelona Pierre-Emerick Aubameyang baada ya bosi wa The Blues Thomas Tuchel kufanya mazungumzo yenye tija na mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal. Klabu hiyo ya Magharibi mwa London inatarajiwa kukutana na Aubameyang baadaye leo kujadili masuala kibinafsi.

Arsenal wanakaribia kumuuza Nicolas Pepe anayewaniwa na OGC Nice, kulingana na ripoti.

Inatajwa kamba winga huyo anakaribia kusaini mkataba ambao utamwezesha kujiunga na klabu hiyo ya Ufaransa kwa mkopo.

Amefunga mabao 27 katika mechi 112 na sasa ni chaguo la pili nyuma ya Bukayo Saka.