Changamoto za wafanyakazi katika shamba la maua Kenya

xc

Chanzo cha picha, Kate Stanworth

    • Author, Ismail Einashe
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Usiku usio na mwezi katika mji wa Naivasha, kando ya ziwa nchini Kenya, Anne ameketi ndani ya nyumba yenye vyumba viwili, akiwa amechoka baada ya kazi ngumu ya kuchuma na kupanga maua ya waridi.

Anne (si jina lake halisi), ni mama asiye na mwenza na mmoja wa maelfu ya wafanyakazi ambao wengi wao ni wanawake katika shamba la maua nchini Kenya, wakivuna maua kwenye ukingo wa Ziwa Naivasha, takribani kilomita 90 (maili 56), kaskazini-magharibi mwa mji mkuu, Nairobi.

Ndani ya vyumba vilivyo na ukubwa wa viwanja vya tenisi, wafanyakazi kama Anne huvuna maua mengi ambayo hukua vizuri katika ardhi yenye rutuba ya Kenya. Mengi ya maua haya yanapelekwa Ulaya.

Anne ametumia zaidi ya miaka 15 kufanya kazi katika shamba hili la maua, mojawapo ya kampuni inayoajiri watu wengi nchini.

Makadirio yanaonyesha kazi hiyo inaajiri zaidi ya watu 150,000 na kuingizia nchi karibu dola za kimarekani bilioni 1 (pauni milioni 760) kila mwaka.

Licha ya kujitolea kwa kazi hii, anasema malipo yake ya kila mwezi ya zaidi ya dola 100 hayajabadilika kwa miaka.

Haitoshi kukabiliana na hali mbaya ya gharama ya maisha nchini Kenya, ambayo imeongeza bei ya bidhaa muhimu za nyumbani kama vile mahindi, ngano, mchele na sukari.

Mwishoni mwa kila mwezi, Anne hana chakula cha kutosha na mara nyingi hulazimika kuruka milo.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Lazima uingie kwenye deni ili kuishi," anasema. Amelazimika kuchukua mkopo kumsaidia mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 23 kusoma chuo kikuu jijini Nairobi.

Kila jua linapochomoza Anne hupanga foleni pamoja na mamia ya wafanyakazi wengine ili kupanda moja ya mabasi ya kampuni kuwapeleka kwenye mashamba, wakati ukungu umetanda juu ya vilima kabla ya kuyeyushwa na jua kali la katikati ya asubuhi.

Anne anaanza kazi saa 01:30 asubuhi, siku sita kwa wiki. Siku ya Jumapili, huenda kanisani.

Masaa nane ndio ya kufanya kazi katika shamba la maua, lakini anasema mara nyingi hulazimika kufanya kazi saa tatu za ziada, ambazo hapokei malipo ya saa za ziada.

Kampuni ya maua imeweka malengo magumu ya kila siku, ambapo wasimamizi huwashinikiza wafanyakazi kuyafikia.

"Tunalazimika kupasisha maua 3,700 kwa siku," anasema.

Anne anahisi malengo haya ni magumu kweli, lakini wafanyakazi kama yeye hawana chaguo ila kutekeleza, au wasimamizi wa mashamba huwaekea vikwazo.

Iwapo tutashindwa kufikia lengo la kila siku, huwabidi waandike taarifa kwa meneja kueleza sababu za kushindwa.

Pia unaweza kusoma
fcv

Chanzo cha picha, Kate Stanworth

Maelezo ya picha, Kenya ni muuzaji mkuu wa maua barani Ulaya

Mwanzoni mwa 2023, Anne alipata tatizo la damu. Alihisi kuishiwa nguvu na kushindwa kupumua, jambo lililofanya kazi yake kuwa ngumu sana.

Alikwenda kumuona nesi wa shamba hilo ambaye alimpa dawa na kumruhusu apumzike kwa saa chache, kisha akamwambia arudi kazini.

"Nilimwambia: 'Unajua, mimi ni mgonjwa na siwezi kufanya kazi.”

Anne anasema ilikuwa vigumu kumshawishi muuguzi huyo kuwa alikuwa mgonjwa, lakini hatimaye alikubali kumpa rufaa kwa daktari aliye nje ya shamba.

Aliruhusiwa siku moja tu ya mapumziko, licha ya kuwa bado alihisi udhaifu na kuwa katika matibabu ya ugonjwa mbaya.

Anne ana wasiwasi kuhusu mambo mengine ambayo kazi yake katika shamba hilo la maua inaweza kudhuru afya yake - kwa mfano, kemikali zisizojulikana ambazo aliombwa atumie kunyunyiza maua ya waridi.

Ni wasiwasi walio nao wafanyikazi wengine wengi.

Margaret, mchuma maua mwingine kwenye shamba, anasema wafanyakazi mara kwa mara wanalazimishwa kunyunyiza kemikali kwenye maua bila kupewa vifaa vya kujikinga.

Margaret (si jina lake halisi) alitutaka tukutane naye baada ya giza kuingia, karibu na ufuo wa Ziwa Naivasha. Anaogopa kusema kwa kuhofia kuadhibiwa.

"Hakuna anayejali," anaongeza.

th

Chanzo cha picha, Kate Stanworth

Maelezo ya picha, Wafanyakazi wengi wana nafasi ndogo ya kupata kazi bora

Ripoti ya Septemba 2023 ya shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu Nairobi, Route To Food Initiative, inaeleza kuwa viuatilifu vyenye hatari hutumiwa mara kwa mara katika kilimo cha Kenya, baadhi vikijulikana kwa kusababisha saratani.

Margaret anasema mara kwa mara amezungumza na wakuu wake kuhusu wasiwasi alio nao. Anasema, “Hawajali, licha ya wao kuwa ni Wakenya.”

Anasema wanawake pia wanaweza kukabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wafanyakazi wa kiume - sekta hiyo imegubikwa na malalamiko ya aina hiyo.

Tumepeleka madai ya unyanyasaji wa kijinsia, saa za ziada zisizolipwa, mazingira magumu ya kufanya kazi, na ukosefu wa zana za kujikinga kwenye mashamba ya maua huko Naivasha kwa Halmashauri ya Maua ya Kenya na Huduma ya Ukaguzi wa Afya ya Mimea (KEPHIS), wakala wa serikali anaehusika na ufuatiliaji viwanda, lakini hakuna aliyejibu.

Kenya hutoa zaidi ya 40% ya maua katika soko la maua barani Ulaya, huku idadi kubwa ya maua yakipelekwa Uholanzi. Maua husafirishwa kila siku kwa ndege na hupelekwa kwenye soko kubwa la maua, ambapo hununuliwa na kusambazwa kwa wasambazaji kote Ulaya.

Katika maduka makubwa na kwa wafanyabiashara wa maua kote Ulaya, watumiaji hununua maua ya bei nafuu kwa ajili ya matukio muhimu kama vile ndoa na siku za kuzaliwa.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Yusuf Jumah