Mtindo wa kupanda maua kwenye viatu Kenya

Viatu vya plastiki vimetumiwa kupanda maua
Maelezo ya picha, Upandani wa mimea ya maua kwenye viatu vikuu

Mjasiriamali raia wa Kenya Wanjiru Waweru-Waithaka ameamua kupanda mimea ya maua katika viatu vya plastiki vikuu kuu.

Maua yamepandwa kwenye viatu vya plastiki
Maelezo ya picha, Mimea hii ya maua iliyopandwa kwenye viatu vya plastiki huwavutia wateja wa Bi Wanjiru Waweru-Waithaka

Mwandishi wa BBC Taurai Munda alipiga picha hizi alipozuru Kenya.

Anasema mimea ya maua inayopandwa kwenye viatu vya plastiki vikuu huwafanya wateja wanaotembelea biashara yake ya kuuza vitanda vya watoto, katika mji wa Kikuyu nje ya jiji la Nairobi watabasamu.

Wanjiru Waweru-Waithaka
Maelezo ya picha, Mjasiliamali wa Kenya Wanjiru Waweru-Waithaka huuza vitanda vya watoto