Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mtindo wa kupanda maua kwenye viatu Kenya
Mjasiriamali raia wa Kenya Wanjiru Waweru-Waithaka ameamua kupanda mimea ya maua katika viatu vya plastiki vikuu kuu.
Mwandishi wa BBC Taurai Munda alipiga picha hizi alipozuru Kenya.
Anasema mimea ya maua inayopandwa kwenye viatu vya plastiki vikuu huwafanya wateja wanaotembelea biashara yake ya kuuza vitanda vya watoto, katika mji wa Kikuyu nje ya jiji la Nairobi watabasamu.