Je, kumwaga manii usingizini ni ishara ya ugumba?

Muda wa kusoma: Dakika 5

Na Nandrakumar, BBC Tamil

Wakati ambapo mwanamume anamwagaa manii akiwa usingizini, wataalamu wanaeleza hali hiyo kama ndoto pevu. Wanaume wengi huwajawa na wasiwasi, kwasababu wanahisi kwamba hatua hiyo ni ishara ya mapema ya kupungukiwa kwa manii au hata kuwa na ugumba.

Madaktari wanasema kwamba, kumwaga manii wakati upo usingizini ni tukio la kawaida.

Shirika la afya duniani WHO linasema kwamba, wakati ambapo mvulana anapobalehe, viwango vyao vya homoni ya kichocheo cha testosterone vinapanda, hali ambayo inachangia kumwaga manii wakati anapolala.

Unaweza pia kusoma:

Sayansi na utafiti zinasema nini kuhusu suala hili?

Ndoto za kujamiiana

Utafiti uliotekelezwa na chuo kikuu cha Shu Yen huko Hong Kong inayofahamika kama 'Ndoto za ngono, ndoto nyevu na kumwagaa manii usiku,' unanchunguza chanzo cha kuwamaga manii mja akiwa usingizini.

Asilimia 80 ya walioshirikishwa kwenye utafiti huo, walisema kwamba ndoto za ngono zilikuwa chanzo cha wao kumwaga manii wakiwa usingizini.

Na japo kwa jumla inaaminiw akwamba vijana waliopo shule ya upili na chuo kikuu ndio wenye kuwa na ndoto za ngono kwa wingi. Utafiti huo pia uligunduwa kwamba wao huwa na ndoto za ngono takriban mara 9 kwa mwaka.

Utafiti huo aidha, unaonyesha kwamba japo ngono ni jambo muhimu katika maisha ya binadamu, ni nadra kujitokeza kwenye ndoto.

'Mwili wa mwanamume kwa kawaida hutengeneza manii. Hata kama kumwagika kwa manii hakutofanyika kupitia shughuli za kingono au kwa kupiga punyeto, manii yanayotengenezwa huondolewa mwilini wakati ambapo mwanamume yupo usingizini. Hili ni jambo la kawaida,' alisema Dkt. Kamaraj ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ngono na afya ya uzazi.

"Kama wanavyopata hedhi wanawake, wanaume pia humwaga manii. Lakini kuna taarifa nyingi za kupotosha ambazo zimehusishwa na nguvu za kiume , na kusababisha wengi kuwa na fikira za kupotosha,' alisema daktari John Bhupathi.

Je, wanaume wanaweza kuwa na ugumba?

Katika ripoti iliyochapishwa kwenye tovuti ya maktaba ya kitaifa ya sayansi ya matibabu ya Marekani, watafiti kutoka chuo cha matibabu cha Tongji kutoka China waliangazia manii ya wananume iliyomwagwa katiak hali isiyoeleweka na manii ya wanaume wenye afya njema.

Katika hali hii, ambayo inafahamika kama kumwaga manii pasi na kukusudia huwa mwanamume anakabiliw ana changamoto ya ugumu wa kumwaga manii, hata ikiwa shughuli hiyo inafanyika kwa haraka.

Utafiti unasema kwamba hali hii ndi chanzo cha asilimia 72 ya ugumba wa wanaume na kwamba wanaume wanakumbwa na hali ya kumwaga manii pasi na kukusudia wanachangamoto ya kumwaga manii wakati waanaposhiriki ngono na hata kuwa na mchangamsho, ila wao humwaga manii wakiwa usingizini.

Manii ilichukuliwa kutoka kwa wanaume 91 ambao wanakabiliw ana tatizo la kumwaga manii pasi na kukusudia wakiwa usingizini, kwa kutumia vifaa vinavyotumia mbinu maalum vya special vibration (PVS na EEJ)

Kwa kukamilisha, utafiti huo una shauri kwamba manii yaliyopatikana kwa njia ya kawaida wakati mwanamume yupo usingizini yana uwezo mkubwa wa kuwa na nguvu za kusonga kwa haraka kwa asilimia 30.6 na muundo wake uko wa asilimia 61.4 kuliko yale ambayo yameopatikana kw anjia zingine.

Tafiti zinaonyesha kwamba wanaume wanaomwaga manii bila kuhafau au kujijua wana manii yenye afya njema ambayo humwagwa wanapokuwa usingizini.

Na kwa kuwa hali ya kumwaga manii wakati upo usingizini ni hali ambayo haijulikani itakotea lini au wakati gani, wale ambao wameshuhudia hali hiyo usingizini mwao katika miezi mitatu iliyopita wameshauriwa kuvaa mipira ya kondomu na kuhifadhi sampuli ya manii kila usiku, kwa ajili ya utafiti huo.

Utafiti mwingine uliochapishwa katika tovuti ya chuo kikuu cha afya ya uzazi wa wanawake na wanaume ya Marekani ilitathmini uwezo wa wanaume wanaokumbwa na changamoto za kusimama wima kuzalisha wenza wao na manii yaliyopatikana walipokuwa usingizini.

Utafiti huo pia unasema kwamba japo viwango vya ubora vya manii inayopatikana kwa njia ya kumwaga manii usingizini huwa tofauti kw akila mwanamume, huenda ikatumika katika uzalishaji wa kisayansi wa kuunganisha na mayayi ya kike, na kuzuia njia ngumu kama vile kumwaga manii kwa kutumia njia za kiektroniki au upasuaji kupata manii.

"Mtu yeyote kuanzia wavulana wenye umri wa miaka 12 hadi watuw azima, wana weza kumwaga manii wakiwa usingizini. Sio jambo la kisayansi kusema kwamba kumwaga manii kwa njia hii ukiwa usingizini kunamfanya mwamnume kuwa na ugumba au kuwa an aidadi ndogo ya manii. Mwili wa binadamu hutengeneza manii mpya kila mwanamume anapomwaga manii. Kulala au kupiga punyeto hakuathiri uwezo wa mwanamume kuzalisha,' asema Dkt. Kamaraj.

Ni kwa nini unamwaga manii ukiwa usingizini?

"Manii inatyoengenezwa na mwanamume huhifadhiwa kwenye kilengelenge cha manii. Kiwango cha kutengeneza manii kinatofautiana kati ya kila mwanamume. Jinsi ambavyo maji yanatoka kwenye bomba la maji pipa lilikwa limejaa maji, ndivyo umwagikaji wa manii hutokea," asema John Bhupati.

Kamaraj anasema kwamba kumwaga manii ukiwa usingizini hakumaanishi kwamba kuan tatizo.

"Ijapokuwa kumekuwepo utafiti mbali mbali, za kinachochangia kumwaga manii ukiwa usingizini, hali hii haijaelwekea kikamilifu. Hutokea wakati ambapo mwanaume ana kuwa na ndoto za kujamiiana au akipatwa na mchangamsho wa ghafla akiwa kitandani. Hakuna Ushahidi kwamba hili linapungunza nguzu zake au kuathiri vibaya uwezo wake kushiriki tendo la kujamiiana.'

'Kumwaga manii, kupiga punyeto, au hata usingizi ni mojawapo ya vyanzo vya mwanamume kumwaga manii . Hasa, hii inaashiria kwamba mwili wa binadamu uko katika hali salama ya kawaida," asema Kamaraj.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Laillah Mohammed na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi