Sababu 5 za kutazama siku zijazo kwa matumaini

Muda wa kusoma: Dakika 7

Katika mwaka ulio na mizozo ya kivita, migawanyiko wa kisiasa, na uchumi unaoonekana kupendelea matajiri pekee, si rahisi kutazamia 2026 kwa matumaini.

Lakini, katikati ya kile kinachoonekana kuwa wimbi la habari na matukio ya kuvunja moyo, kuna sababu kadhaa za kuwa na matumaini.

Katika taarifa hii tunaangazia mambo matano, ambayo yanatukumbusha hatua ambazo tumepiga kwa miongo kadhaa katika nyanja tofauti.

Idadi ya watu maskini imepungua kwa kiasi kikubwa

Kuanzia mwaka 1990 hadi 2025, jumla ya idadi ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri duniani ilipungua kutoka bilioni 2.3 hadi milioni 831, kulingana na Kundi la Benki ya Dunia.

"Takwimu hizi zinamaanisha kuwa takriban watu bilioni 1.469 wameepuka hali hiyo, hasa kati ya 1990 na 2010, wakati uwiano wa kimataifa uliposhuka kutoka 47% hadi 10%," José Manuel Corrales, profesa wa Uchumi, Biashara na Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Ulaya, ameiambia BBC.

Kupungua kwa hali ya umasikini kunatokana kwa kiasi kikubwa na ukuaji ulioshuhudiwa katika eneo la Asia ya Mashariki na Kusini hususan katika nchi mbili: China na India, ambapo - profesa anaonyesha - ukuajii ulichochewa na uwazi wa kiuchumi na utekelezaji wa mageuzi ya soko.

"Ajira rasmi, uwekezaji katika miundombinu, elimu, afya na mifumo ya hifadhi ya jamii pia ulichangia pakubwa," anasema.

Ingawa takwimu hizi zinathibitisha maendeleo makubwa katika mapambano dhidi ya umaskini na kuhamasisha matumaini, hatuwezi kupoteza mtazamo wa watu milioni 831, 1 kati ya 10, ambao wanaishi chini ya dola 3 za Marekani kwa siku.

Je, kuna matumaini yoyote ya kuwatoa humo?

"Ndiyo, bila shaka kuna ishara za kutia moyo," Corrales anaonyesha. "Zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani sasa wanapokea aina fulani ya ulinzi wa kijamii, hatua ambayo inaimarisha ustawi wa jimii na kuwawezesha mamilioni ya watu kuepuka umaskini na kuhimili migogoro."

Kulingana na wataalamu uwekezaji katika mifumo ya elimu na afya ni muhimu ili kuendelea kupunguza idadi ya watu wanaoishi katika umaskini.

Na ni muhimu kuzingatia maeneo yaliyoathirika zaidi: "Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara ina zaidi ya 75% ya watu walio katika umaskini uliokithiri na wengine wamejilimbikizia."

Sera za umma zinazokuza sio tu ukuaji endelevu, lakini pia uchumi wa kijani, haki za binadamu, na usawa wa kijamii ni muhimu, anasema. Vinginevyo, "umaskini unaweza kudorora."

"Ukuaji wa uchumi pekee hautoshi: ulinzi thabiti wa kijamii na mikakati ya kina inahitajika ili kutokomeza umaskini."

Japo, Corrales anaafiki kupungua kwa kasi kwa idadi ya watu duniani wanaoishi katika umaskini uliokithiri, anaonya kwamba "kasi imepungua na, kulingana na makadirio, inaweza kukwama au hata kurudi nyuma baada ya 2030."

2. Maendeleo ya kisayansi dhidi ya saratani

Saratani ni moja ya sababu kuu za vifo ulimwenguni.

Mnamo 2020 iligharimu maisha ya takriban watu milioni 10, kulingana na Shirika la Afya Duniani(WHO).

Licha ya hayo, aina kadhaa za saratani zinaweza kutibiwa ikiwa zitagunduliwa mapema na kutibiwa ipasavyo. Hata katika hali ya juu, maendeleo yao yanaweza kupunguzwa.

Johns Hopkins Hospital, nchini Marekani, na kituo chake cha utafiti wa matibabu na mafunzo kwa zaidi ya miaka 125 ya historia.

"Tafakari ulimwengu usio na saratani." Hiyo ndiyo sentensi ya kwanza inayoonekana unapoingia kwenye tovuti ya kituo chao cha saratani, The Sidney Kimmel Comprehensive Cancer Center.

Katika mojawapo ya makala zake kuhusu tiba ya kinga na tiba ya usahihi, shirika hilo linatoa ujumbe wa matumaini: "Kwa bahati nzuri, katika nyakati hizi za maendeleo ya matibabu na uvumbuzi, saratani sio tena hukumu ya kifo."

Dk. Dani Skirrow, mmoja wa wasemaji wa kitengo cha utafiti wa shirika lenye makao yake makuu London la Utafiti wa Saratani, ambalo asili yake ni 1902, anakubaliana na wazo hili.

Ingawa inatoa takwimu zinazolenga Uingereza, ambapo kiwango cha saratani kimeongezeka maradufu katika miaka 50, ikimaanisha kuwa watu 2 kati ya 4 walio na saratani wanatarajiwa kuishi miaka 10 au zaidi kutokana na utambuzi huo, uzoefu wake nchini humo pia unatia matumaini.

"Kuna njia nyingi za kutibu saratani, hasa ikigunduliwa mapema, matibabu ni rahisi kabla ya kuenea. Kuigundua mapema kunawapa nafasi kubwa ya kufaulu," mtaalam huyo aliambia BBC.

Japo mtindo wa maisha ni wa msingi - kama vile kuepuka tumbaku, kula chakula bora, kukaa hai, kati ya mambo mengine - kwa sasa kuna ahadi za matibabu.

Kwa mfano, Skirrow anaonyesha, utengenezaji wa chanjo ambazo zinaweza kutolewa kwa watu walio katika hatari kubwa ya kupata aina fulani ya saratani ili kuwakinga wasiipate.

Lengo ni kuiwezesha mfumo wa kinga kutambua seli ambazo zinaweza kuwa saratani katika siku zijazo, lakini bado hazina saratani.

"Kinga itazigundua, kuziwinda na kuziaondoa mwilini kabla ya kupata nafasi ya kuwa saratani," aeleza.

Kulingana na daktari, matibabu ya saratani sasa yanaelekea kuwa sahihi zaidi na ya kibinafsi kuliko hapo awali.

"Miaka iliyopita, matibabu kimsingi yalijaribu kuondoa seli za saratani zinazokua kwa kasi, lakini hiyo inaweza kusababisha athari kadhaa."

"Sasa tunajua mengi zaidi kuhusu saratani. Tunaweza kuona maelezo ya seli maalum, njia, na michakato ya kibayolojia ambayo seli hizi za saratani hufanya ili kukua, jambo ambalo halifanyiki katika seli zenye afya. Kwa maelezo hayo, tunaweza kuunda dawa maalum za kuizuia."

3. Watoto wengi zaidi wananusurika leo kuliko hapo awali

Mojawapo ya mafanikio makubwa katika nyanja ya afya katika miongo ya hivi karibuni ni kupungua kwa vifo vya watoto wachanga.

Kufikia 2022, hatua ya kihistoria ilikuwa imepigwa kukabiliana vya vifo vya watoto na kwa kipindi hicho vilipungua chini ya milioni 5, idadi ambayo haijawahi kutokea, kulingana na Unicef.

Inabidi tu urudi 1990 ili kuona maendeleo ya ajabu. Mwaka huo, mtoto 1 kati ya 11 alikufa kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano, ikilinganishwa na 1 kati ya 27 mnamo 2023.

mwezi Machi, UNICEF ilibainisha kuwa idadi ya watoto duniani kote wanaofariki kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano ilikuwa chini kwa kiwango cha kuridhisha.

Tangu 2000, kiwango cha vifo vya watoto chini ya umri wa miaka 5 ulimwenguni kimepungua kwa 52%.

Nchini Cambodia, Malawi, Mongolia, na Rwanda, kiwango hicho kimepunguzwa kwa zaidi ya 75%.

Mnamo mwaka wa 2022, inakadiriwa vifo 152,000 vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 vilirekodiwa katika Amerika ya Kusini na Caribbean, ikiwakilisha punguzo la 60% tangu 2000.

Hatua kadhaa zimepiga ili kufikia takwimu hizi. Moja ya hatua hizo—kulingana na UNICEF, pamoja na wataalamu wengi—ni chanjo.

Jambo lingine muhimu limekuwa kuimarishwa kwa mfumo wa ufuatiliaji wa matibabu kwa akina mama wakati wa ujauzito na mtoto mchanga kwa siku na miaka yake ya kwanza.

4. Kuongezeka kwa nishati mbadala

"Nishati mbadala inaendelea na upanuzi wake wa haraka kote ulimwenguni," inasema ripoti ya World Energy Outlook 2025 ya Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA).

Hiyo ni habari njema huku kukiwa na juhudi za kimataifa za kupunguza utoaji wa gesi chafuzi, muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuzuia matukio mabaya ya hali ya hewa, kama yale ambayo yameathiri mamilioni ya watu katika miaka ya hivi karibuni.

Katika ulimwengu ambao una "kiu ya nishati", teknolojia mpya zinaendelea kuuniwa kwa kasi ya juu.

"Nishati mbadala ilivunja rekodi mpya za kupelekwa mwaka 2024 kwa mwaka wa ishirini na tatu mfululizo," ripoti hiyo inasema.

Inatia moyo kuona kwamba njia mbadala za kupunguza uzalishaji wa hewa chafu hazijulikani tu kwa upana, lakini pia, katika hali nyingi, ni za gharama nafuu.

Serikali, mashirika na makampuni mengi tayari yamejumuisha katika usimamizi wao hitaji la kuchunguza chaguo za kupata nishati.

Kwa hakika, kufikia nusu ya kwanza ya 2025, upepo, jua na vyanzo vingine.

Ingawa kiwango cha matumizi kinatofautiana kulingana na eneo, nishati mbadala, haswa kawi inayotokana na jua, "zinakua kwa kasi zaidi kuliko chanzo kingine chochote cha nishati," IEA inasema.

Hata hivyo, shirika hilo linakubali kwamba "hatua za kitaifa na kimataifa za kupunguza uzalishaji zimepoteza kasi."

Na hiyo inatia wasiwasi kutokana na ongezeko la mabadiliko ya hali ya hewa.

Mwaka wa 2024 ulishuka katika historia kuwa wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa na wa kwanza ambapo halijoto ya kimataifa ilizidi nyuzi joto 1.5 juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda.

Sasa 2025 inaonekana kuwa ulipita kwa ujumbe wazi: tunajua jinsi ya kupunguza hatari kubwa zaidi za mabadiliko ya hali ya hewa, hebu tufanye upya ahadi yetu ya kupigana nayo.

5. Wasichana hawako nyuma tena shuleni

"Duniani kote, wasichana wamepita wavulana katika viwango vya uandikishaji na kuhitimu shuleni," inabainisha ripoti ya UN Women "Gender Panorama 2025".

Huko nyuma mnamo 2024, Kundi la Benki ya Dunia liliangazia kile ilichoona kuwa moja ya mafanikio ya maendeleo ya msukumo wa miaka 50 iliyopita: maendeleo katika elimu ulimwenguni kote.

"Wasichana, ambao kihistoria walikuwa na viwango vya chini sana vya masomo na ambao mara kwa mara walibaki nyuma ya wavulana, sasa wanapokea elimu kwa viwango vya juu zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika historia."

Kulingana na shirika hilo, katika miongo ya hivi karibuni kumekuwa na maendeleo thabiti kuelekea usawa wa kijinsia katika uandikishaji wa shule, katika elimu ya msingi na sekondari.

Hata hivyo, viwango vya usawa duniani "hugubika" tofauti kati ya maeneo ya kijiografia, jambo ambalo UN Women pia imeonya.

"Wakati mapengo ya kijinsia yameondolewa katika ngazi zote za elimu duniani kote, tofauti katika elimu ya sekondari ya juu bado inaendelea kwa wasiwasi katika mikoa mitatu kati ya minane."

Kulingana na shirika hilo la Umoja wa Mataifa, kwa sasa wasichana milioni 119.3 hawaendi shuleni, milioni 124.7 idadi ambayo ni ya chini kuliko mwaka 2015.

Ingawa wasichana wengi zaidi wanamaliza masomo yao ya shule ni mwelekeo wa matumaini, shirika linaonya kwamba vikwazo vya maendeleo havikomei kwa wengi wao.

Kwa mfano, katika uchanganuzi uliojumuisha nchi 70, katika mataifa 65 kati ya hizo uwezekano wa wanawake kuwa walimu ulikuwa mkubwa zaidi kuliko uwezekano wa wao kuwa wakuu wa shule za upili.