Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 22.08.2023

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Klabu za Bayern Munich na Liverpool zinamuwania kiungo wa Uingereza Kalvin Phillips, 27, kutoka Manchester City. (90min)

Manchester City wamefikia makubaliano ya kibinafsi na Jeremy Doku juu ya mkataba wa muda mrefu ambao ulikuwa wa thamani ya euro 60m (£51.3m) uliokubaliwa na Rennes kwa winga huyo wa Ubelgiji, 21. (Fabrizio Romano).

West Ham walikuwa wamefikia mkataba wa pauni milioni 85 na Manchester City kumuuza Lucas Paqueta kabla ya uhamisho huo kusambaratika kutokana na kiungo huyo wa Brazil, 25, kuchunguzwa kwa ukiukaji wa kanuni za kamari. (Mail)

Brighton wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 25 wa kiungo wa kati wa Lille raia wa Cameroon Carlos Baleba, 19. (Talksport).

Dominic Solanke

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Bournemouth Muingereza Dominic Solanke

West Ham wamewasilisha ombi rasmi la takriban £35m kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth Muingereza Dominic Solanke mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)

Paris St-Germain bado wana matumaini wanaweza kumshawishi Kylian Mbappe kuongeza mkataba wake baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 24, kukutana na maafisa wa kundi la umiliki wa klabu hiyo ya Qatar, licha ya mchezaji huyo kuhusishwa na kuhamia Real Madrid mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Diario AS - kwa Kihispania)

West Ham wanafanya mazungumzo na Sevilla kuhusu usajili wa mshambuliaji wao wa Morocco Youssef En-Nesyri, 26. (90min).

Chelsea wamekubali mkataba wa pauni milioni 14 kwa mlinda mlango wa New England Revolution wa Serbia Djordje Petrovic, 23. (Mail).

Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Fulham wanakabiliwa na changamoto mpya kumpata Callum Hudson-Odoi wa Chelsea baada ya Everton na Nottingham Forest kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili winga huyo wa zamani wa Uingereza, 22. (Standard).

Chelsea bado wapo kwenye mazungumzo kuhusu uhamisho wa Folarin Balogun wa Arsenal, licha ya mshambuliaji huyo wa Marekani, 22, kukubaliana kibinafsi na The Blues . (Football Transfers)

Fulham wako tayari kukabiliana na Tottenham katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Gift Orban, 21, kutoka Gent ya Ubelgiji. (Football Insider)

Callum Hudson-Odoi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Fulham wanakabiliwa na changamoto mpya kumpata Callum Hudson-Odoi wa Chelsea

Lazio wamerejelea tena mazungumzo na Tottenham kuhusu mpango wa kumnunua mlinda mlango wa Ufaransa Hugo Lloris mwenye umri wa miaka 36. (Sky Sports Italia - kwa Kiitaliano)

Aston Villa wameonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Ureno Nuno Tavares, 23, kutoka Arsenal. (90min)

Brentford wamefanya uchunguzi kuhusu uwezekano wa kumnunua winga wa Leeds United kutoka Colombia Luis Sinisterra, 24. (Football Insider)

Manchester City wanakaribia kukubaliana na winga wa Ureno Bernardo Silva, 29, na beki wa kulia wa Uingereza Kyle Walker, 33 kuhusu kandarasi mpya. (ESPN)

Thomas Tuchel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mkufunzi wa Bayern Munich Thomas Tuchel kuamua mustakabali wa mchezaji Ryan Gravenberch katika klabu hiyo.

Liverpool wanasubiri matokeo ya majadiliano kati ya kiungo wa Bayern Munich Ryan Gravenberch, 21, na mkufunzi Thomas Tuchel kuhusu mustakabali wa Mholanzi huyo. (Liverpool ECHO)

Manchester United wanataka kumsajili kiungo na mlinda mlango kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji lakini wanahitaji kupunguza kikosi chao kwanza. (ESPN)

Mshambuliaji Muingereza Mason Greenwood, 21, anatazamia kutafuta ofa nchini Uturuki au Italia baada ya pande zote kukubaliana kuihama Manchester United kufuatia uchunguzi wa ndani wa klabu hiyo. (Mail)