Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 19.08.2022

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Cristiano Ronaldo hana mahali dhahiri pa kurejea huku akifikiria kuhusu mustakabali wake katika kilabu ya Manchester United, kulingana na timu ya podikasti ya BBC Radio 5 Live Euro Leagues.

Julien Laurens, Guillem Balague na Raphael Honigstein wamekuwa wakifikiria mustakabali wa Ronaldo - huku fowadi huyo mahiri akiwa hafichi kwamba anataka kuondoka Old Trafford ili kucheza Ligi ya Mabingwa.

United, wakiwa wameelezea wasiwasi wao kuhusu jinsi hali ya fowadi huyo mwenye umri wa miaka 37 inavyoathiri ari kambini, wako tayari kumwacha aende zake.(BBC SPORT)

Manchester City hawataki kumuuza kiungo wao Bernardo Silva, 28, licha ya Paris St-Germain na Barcelona kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno. (Sky Sports)

PSV Eindhoven haitakaribisha ofa kutoka kwa Manchester United kumnunua mshambuliaji wa Uholanzi Cody Gakpo, 23, hadi baada ya mechi yao ya mkondo wa pili ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa wakiwa nyumbani dhidi ya Rangers mnamo Agosti 24. (MailOnline)

Manchester United wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ubelgiji Yannick Carrasco, 28 kwa pauni milioni 25. (Telegraph - subscription required)

Everton walikuwa wakihusishwa na kiungo wa Tottenham Muingereza Harry Winks, 26, lakini mkufunzi wa Toffees Frank Lampard ameamua kuachana na mpango huo. . (Times - subscription required)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea itafikiria kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Christian Pulisic, 23, kwa Manchester United ikiwa nahodha huyo wa Marekani atakubali kuongezwa kwa mkataba wake wa sasa, ambao umebakiza miaka miwili kumalizika. (MailOnline)

Borussia Dortmund haitatafuta fursa ya kumsajili fowadi wa Manchester United Mreno Cristiano Ronaldo, 37, kwa sababu ya umri wake na mahitaji ya mshahara. (Bild - in German, subscription required)

Fulham wanajadiliana kuhusu ada na Roma baada ya kuafikiana na winga wa Uholanzi Justin Kluivert, 23. (Guardian)

West Ham wanafikiriwa kuwasilisha ombi jingine kwa kiungo wa Ubelgiji na Club Bruges Hans Vanaken, 29, baada ya ofa yao ya kwanza kukataliwa. (Sky Sports)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Watford wamekataa ofa ya pili kutoka kwa Newcastle kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji Joao Pedro, dau hilo linadhaniwa kuwa la £22m pamoja na £3m kuongeza nyongeza kwa Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 20. (The Athletic - subscription required)

Mlinzi wa Ufaransa na Lyon Malo Gusto, 19, amevutia Barcelona na Manchester United. (L'Equipe - in French)

AZ Alkmaar wamekataa ofa ya takriban euro milioni 15 kutoka kwa Bournemouth na Celta Vigo kwa Jesper Karlsson, 24, licha ya mshambuliaji huyo wa Uswidi kutaka kuondoka katika klabu hiyo ya Uholanzi. (De Telegraaf - in Dutch)

Mazungumzo bado yanaendelea kati ya vilabu vyote viwili licha ya zabuni ya pili kukataliwa. (Fabrizio Romano)